Tabia njema wakati wa kula chakula

Tabia njema wakati wa kula chakula

Mjamaa1

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
7,596
Reaction score
6,023
Salamu.

Tusichoshane hapa, Katika jamii iliyo staarabika kuna kanuni za kufuata kabla, wakati na baada ya kula chakula, sasa kanuni hizo ndiyo inaleta tabia njema wakati wa kula, sasa zifuatazo ni tabia njema kabla, wakati na baada ya kula.

Kabla ya kula chakula zingatia kunawa mikono kwa maji safi na sabuni. Rejea Kipindi cha Korona.
Wakati wa kula chakula zingatia yafuatayo.

1. Kaa vizuri kwa unyoofu ili kuepuka kudondosha ovyo chakula. Pia unaweza kusali kabla ya kula chakula.

2. Pakua chakula unachoweza kukimaliza, pia zingatia idadi ya watu wanaotakiwa kula chakula hicho, maana wengine hupakua chakula na kusahau wengine wanaotakiwa kula chakula hicho.

3. Weka kinywani chakula cha kutosha, epuka kujaza kinywa kwani unaweza kupaliwa, kukabwa au kutokwa na chakula wakati wa kutafuna, sio ustaarabu.

4. Tafuna chakula polepole bila kupanua kinywa (hapa wengi wanafeli) unapotafuna hakikisha umetulia na huzungumzi bila sababu.

5. Ni vyema kula chakula kwa kadri, epuka kushiba kupita kiasi.
6. Epuka kujikuna wakati wa kula, especially kichwani.
7. Funika mdomo kwa mkono au kitambaa endapo utapata chafya au kuhoa wakati wa kutafuna chakula.
8. Epuka kunywa maji wakati una chakula mdomoni kwani unaweza kupaliwa.
9. Acha uchoyo, tabia ya uchoyo au ulafi si nzuri.
10. Shukuru baada ya kula, kisha nawa mikono vizuri kwa maji safi na sabuni.

Baada ya kula, epuka kutoa masalio ya chakula kwenye meno mbele za watu kwani sio ustaarabu.

Pia epuka kukaa na kijiti cha kutolea masalio ya chakula mdomoni kwa muda mrefu kwani ni uchafu kiafya na unaweza kujiumiza au kukimeza.

Regards.
👉DonC
Picha kwa hisani ya Google

images.jpeg-5.jpg
images.jpeg-4.jpg
images.jpeg-2.jpg
images.jpeg-3.jpg
images.jpeg-1.jpg
 

Attachments

  • images.jpeg.jpg
    images.jpeg.jpg
    39.9 KB · Views: 4
No.1 ni muhimu sana sio unaweza kusali, lazima usali .
 
Hiyo picha no tatu huyo mwamba lazima atakua amelewa hajui mdomo upo wapi.
 
Dah mimi inabidi nizingatie hizi kanuni. Kuishi kisela muda mrefu imeniharibu sana eneo hilo.

Yaani nimeshazoea nakaa kwenye sofa, mguu m'moja naweka kwenye Arm rest, mwingine dirishani halafu msosi naweka sakafuni natafuna huku nimejilaza nachezea simu huku natazama kideo.

Maisha yenyewe haya yalivyo magumu na kero kibao wacha tu nijipe raha.

Nikimaliza najilaza sakafuni nadigest msosi wangu tumboni taaratibu, mkono m'moja kwenye Boxer mwingine unachezea simu naperuzi.
 
Back
Top Bottom