Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 15,954
- 35,415
Inategemea unakula wapi na uko na nani!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Really?Surely and you cant even snipe him..he is so smart[emoji205][emoji112]
💯 PercentReally?
kuna picha Mzee fulani anakula ugali nyama na KIKWETE yule mzee bila aibu wala uoga anachukua nyama kabla ya RAIS 😅 😄Inategemea unakula wapi.
Si vizuri kuwasema watoto wakati wa kula au kuongea wakati wa kula.Salamu.
Tusichoshane hapa, Katika jamii iliyo staarabika kuna kanuni za kufuata kabla, wakati na baada ya kula chakula, sasa kanuni hizo ndiyo inaleta tabia njema wakati wa kula, sasa zifuatazo ni tabia njema kabla, wakati na baada ya kula.
Kabla ya kula chakula zingatia kunawa mikono kwa maji safi na sabuni. Rejea Kipindi cha Korona.
Wakati wa kula chakula zingatia yafuatayo.
1. Kaa vizuri kwa unyoofu ili kuepuka kudondosha ovyo chakula. Pia unaweza kusali kabla ya kula chakula.
2. Pakua chakula unachoweza kukimaliza, pia zingatia idadi ya watu wanaotakiwa kula chakula hicho, maana wengine hupakua chakula na kusahau wengine wanaotakiwa kula chakula hicho.
3. Weka kinywani chakula cha kutosha, epuka kujaza kinywa kwani unaweza kupaliwa, kukabwa au kutokwa na chakula wakati wa kutafuna, sio ustaarabu.
4. Tafuna chakula polepole bila kupanua kinywa (hapa wengi wanafeli) unapotafuna hakikisha umetulia na huzungumzi bila sababu.
5. Ni vyema kula chakula kwa kadri, epuka kushiba kupita kiasi.
6. Epuka kujikuna wakati wa kula, especially kichwani.
7. Funika mdomo kwa mkono au kitambaa endapo utapata chafya au kuhoa wakati wa kutafuna chakula.
8. Epuka kunywa maji wakati una chakula mdomoni kwani unaweza kupaliwa.
9. Acha uchoyo, tabia ya uchoyo au ulafi si nzuri.
10. Shukuru baada ya kula, kisha nawa mikono vizuri kwa maji safi na sabuni.
Baada ya kula, epuka kutoa masalio ya chakula kwenye meno mbele za watu kwani sio ustaarabu.
Pia epuka kukaa na kijiti cha kutolea masalio ya chakula mdomoni kwa muda mrefu kwani ni uchafu kiafya na unaweza kujiumiza au kukimeza.
Regards.
[emoji117]DonC
Picha kwa hisani ya Google
View attachment 2614281View attachment 2614282View attachment 2614283View attachment 2614284View attachment 2614285
Good for you, dear[emoji817] Percent
Thank you Gentleman 😊👋Good for you, dear