Tabia ya kukoroma inanivunjia ndoa yangu

Tabia ya kukoroma inanivunjia ndoa yangu

Wewe unajuaje kama mtoa mada hana mapungufu mengine ambayo mkewe hayavumilii, mbona umeassume kama jamaa ni mkamilifu hana mapungufu mengi zaidi ya kukoroma, ndio maana nikasema binadamu tunatofautiana katika mambo yanayotukera, kwangu jambo linaweza kuwa dogo ila kwa mwingine ni kubwa, usikute huyo mke anavumilia mengi tu ya mumewe ila hilo la kukoroma ndio ameshindwa
Sijafika huko na sijataka ku assume kwakua mdau hapo kwanza kajieleza mapungufu yake kwakhiyo hata kama yapo mengine pia ,tayar mwamba anaonekana humble kujiweka bayana asaidiwe.
Tujikite kwenye yalio andikwa na sio yasioandikwa maana tutakua tuna guese tu na that is not proper
 
Na ndiyo maana nimesema, mke achague aidha kitambi alafu usiku alale kwa amani au kitambi kisiwepo ila akubali jamaa akaorome usiku kwa sababu ya uchovu wa mazoezi.
 
Mkuu suala la binadamu kuwa na mapungufu wala halihitaji kujieleza kwa sababu it is obvious, hakuna binadamu mkamilifu kila mtu ana mapungufu yake tena siyo madogo, yawezekana mtoa mada ametaka asaidiwe hilo sababu anaona ndilo linaloenda kumvunjia ndoa yake
 
Na ndiyo maana nimesema, mke achague aidha kitambi alafu usiku alale kwa amani au kitambi kisiwepo ila akubali jamaa akaorome usiku kwa sababu ya uchovu wa mazoezi.
Kwamba umeona sababu kubwa ya jamaa kukoroma ni kufanya mazoezi, kwahiyo kila anayefanya mazoezi pamoja na majukumu mengine ni lazima akilala akorome, kwani kufanya mazoezi ni suala la kumfurahisha mke (kiasi cha kutaka mke achague moja) au ni kwa manufaa yake mwenyewe
 
1: Kulingana na jamaa, sababu ya yeye kukoroma ni uchovu uliosababishwa na mazoezi + majukumu yake. ( Hatuongelei watu wengine, tunazungumza kuhusu jamaa na madhaifu yake aliyoleta)

2: Kulingana na maelezo ya jamaa, ameanza mazoezi ili kupunguza kitambi ambacho mke wake amekuwa akimsimanga.

Note: Mke achague moja, jamaa afanye mazoezi apunguze kitambi na usiku akorome AU jamaa aache kufanya mazoezi, usiku asikorome ila kitambi kiwepo.
 
Pole sana mkuu hilo tatizo lina mwarubaini wake kabisa.
Tena huna haja yakutumia fedha yoyote kununua dawa.
Kitaalamu sina muda wakulielezea sana hapa kwakua namda mchache.
Ila tiba yake fanya meditation👈
Ya pumzi👈
kuhusu meditation kwaujumla unaweza kujiunga na groups zangu za meditation WhatsApp.
Anza kwakufanya hivi.
Mkao utakao kufanya uwe relax sana nyoosha mgongo wako vizuri sana.
Vuta pumzi ndefu kujaza kifua kabisaa kisha ishikilie pumzi huku ukihesabu namba moja mpaka 30 kimoyo moyo
(Ndani kwandani)
Kisha itoe pumzi yote kabisa nj'e.
Hivo hivo tena huku ukipanda hesabu kidogo kidogo hadi kufikia hesabu ya 60+120 kwamuda wawiki1 tatizo lako utakua umepona kabisaa.
Ila meditation usiache baada yakupona walau ×1 baada yasiku2.
🙏🙏🙏
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Wakuu,

Kwa kuanza, mimi ni kijana wa makamu, umri 35+, mfupi, kibonge, mweusi tiiiiiiii!

Nimeajiriwa kwenye NGO moja ya wazungu, alhamdulilah familia inaenda chooni. Nimebahatika kuwa na watoto wa3 kila mmoja na mama yake na nashukuru wanangu wanaishi vizuri lakini sikubahatika kuoa wazazi wenza kwa sababu ya tabia zao za midomo midomo na uswahili mwingi.

Nilikuwa nikiishi single na muda mwingi niliutumia nikiwa na jamaa zangu Jeffu na Bakari ambao tulikuwa tukifanya kazi pamoja.

Basi siku moja rafiki zangu Jeffu na BeKa wakanishauri ninyoe upara kwa madai eti utanipendeza kutokana na kujaaliwa na udevu kama brush la kupakia chachandu kwenye mihogo.

Kweli bwana nikaamua kuwasikiliza swahiba zangu Beka na Jeffu nikafunga safari mpaka kwa kinyozi wangu kevii aliyezoea kuninyoa mnyoo wangu wa pank la kiaskari, siku hii alishangaa sana kusikia nataka kunyoa upara, hakuwa na budi kwakuwa mteja ni mfalme.

Nilipata tabu sana wakati wa mwanzo, sikuzoea kabisa kuwa na kipara. Basi ni kipindi hiki ndio nilikutana na wife wangu wa sasa, huyu alikuwa bestie yake na mke wa swahiba yangu bakari (beka) weekend moja nilimtembelea Beka kwake na nilimkuta peke yake huku akidai mkewe kaenda kicoba, basi baada ya muda shemeji alirudi akiwa na huyo rafiki yake (wife wangu wa sasa)

Baada ya siku kadhaa nilitafutwa na namba ngeni ambapo baada ya kujitambulisha niligundua ni yule rafiki wa shemeji basi tukaanza ukaribu na kuwa marafiki, huyu dada alipenda sana kunisifia upara wangu, na kunifanya nijute kwanini nilichelewa kunyoa dongo.

Muda ukapita, siku, wiki, miezi ukaribu ukazidi na akawa mtu wangu rasmi (beka na mkewe wote walijua) ukiacha upara wangu, huyu bibie alikuwa akiniheshimu na kunishukuru sana nilipokuwa namuokoa na pesa za marejesho na vicoba kwani alikuwa na michezo zaidi ya 15 sijui alikuwa anapeleka wapi hizi pesa.

Penzi likakolea na bibie wote tukakubaliana kufunga ndoa na tafrija fupi iliyokutanisha watu wachache tu, wazazi, marafiki zetu wakina beka na Jeffu pamoja na wana kikundi wenzake wa kikoba.

Hii siku ya ndoa hakika nilipendeza sanaa, nilimwambia kinyozi wangu kevii ahakikishe anakwangua haswaa upara wangu ili nimfurahishe mke wangu kwenye harusi yetu. Harusi ilifana sana, watu walikula na kunywa.

Maisha ya ndoa yakaanza...............:.!

Itaendelea.....

View attachment 3117210
Ukimaliza utunzi wa hii hadithi, utaniuzia
 
1: Kulingana na jamaa, sababu ya yeye kukoroma ni uchovu uliosababishwa na mazoezi + majukumu yake. ( Hatuongelei watu wengine, tunazungumza kuhusu jamaa na madhaifu yake aliyoleta)

2: Kulingana na maelezo ya jamaa, ameanza mazoezi ili kupunguza kitambi ambacho mke wake amekuwa akimsimanga.

Note: Mke achague moja, jamaa afanye mazoezi apunguze kitambi na usiku akorome AU jamaa aache kufanya mazoezi, usiku asikorome ila kitambi kiwepo.
Ndio maana nikakuuliza kwani jamaa kufanya mazoezi ni kwa faida ya mke au ya kwake mwenyewe, yani kufanya mazoezi nalo ni suala la kucompromise eti kisa ni mkewe ndiye aliyemuambia, bila shaka hata jamaa anajua faida ya mazoezi ndio maana hajamuambia mkewe achague moja
 
1: Kwa maelezo ya jamaa, ameanza kufanya mazoezi ili kupunguza kusimangwa na mke wake.

2: sawa, jamaa anajua faida ya mazoezi ndiyo maana hajamwambia. Je mke yeye hajui faida ya hayo mazoezi? Kwanini aseme ndoa itamshinda kisa jamaa anakoromoa? Je hajui kukoroma kunatokana na hayo mazoezi ya kupunguza kitambi?
 
Ndio maana nikasema huwezi kumpangia binadamu jambo lipi limfurahishe na lipi limkere, kama mke anaona kwake kukoromewa ni kero hatuwezi kumlazimisha avumilie, na mke anajua kukoroma siyo udhaifu wala ugonjwa na kikawaida hakusababishwi na kufanya mazoezi na ni tabia ambayo inawezekana kuacha
 
Jamaa amesema, kufanya mazoezi + majukumu yake inasababisha kuchoka hivyo usiku kukoroma. Wewe kwanini unabishana na mtoa mada kwamba hakusababishwi na kufanya mazoezi?

NB: Mtoa mada kasema.
 
Jamaa amesema, kufanya mazoezi + majukumu yake inasababisha kuchoka hivyo usiku kukoroma. Wewe kwanini unabishana na mtoa mada kwamba hakusababishwi na kufanya mazoezi?

NB: Mtoa mada kasema.
Kukoroma ni tabia ambayo inawezekana kuacha bila kuathiri ratiba ya mazoezi, na ndio maana hata yeye mwenyewe hajachukua uamuzi wa kuacha mazoezi bali kaja jf kutafuta solution ya kuacha kukoroma, narudia suala la jamaa kufanya mazoezi siyo la kucompromise na mkewe hata kama ni yeye ndiye aliyemuambia
 
Kabla ya mazoezi, hakuwa anakoroma. Kwahiyo ni aidha aache mazoezi, au amwambie mke wake avumilie mpaka kitambi kiishe.
 
Kabla ya mazoezi, hakuwa anakoroma. Kwahiyo ni aidha aache mazoezi, au amwambie mke wake avumilie mpaka kitambi kiishe.
Solution ya yeye kuacha kukoroma siyo kuacha mazoezi, ndio maana nikakuambia mtoa mada alikuwa na uwezo wa kufanya maamuzi hayo ya kuacha mazoezi, lakini hakufanya hivyo badala yake akaamua kuja jf kutafuta solution ya kuacha kukoroma
 
Kipara ngoto..

Mwwnye kufahamu hili jina lilianzia wapi anisaidie. Kulikuwa na kawimbo fulani utotoni kanajijia kwa mbali kwenye akili yangu.
Kipara ngoto songa ugali tule hapo unasikia paaa ukiwa na upara
 
Jamaa ako Jefu na Beka mbona kama wanakuzoom kwa mbali..hawaingilii kabisa ndoa yako kwa msaada wakati wao ndio walikupa mke! Skiliza KP...fanya haya utanishkuru
1.kata kabisa malipo yoyote ya kikoba au michezo
2.Hama chumba
3.Acha mazoezi..kula zako kitimoto ukija lala zako

Fanya hivi wiki tu...na utakuja unipe serengeti mbili na rosti kavu...na ndizi mbili
 
Back
Top Bottom