Tabia ya kumtext mtu au kuanza mazungumzo kurupu anasema nipange au niambie huwa inakera sana

Tabia ya kumtext mtu au kuanza mazungumzo kurupu anasema nipange au niambie huwa inakera sana

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Moja kwa moja..

Huu mtindo umeshamiri haswa kwa vijana unakuta mtu ameanza kukutext au wewe umeanza kumsalimia baada ya kujibu text yake inayofuata "nipange "au "niambie" mimi mara nyingi hapo huwa mwisho wa kuchat isipokuwa kwa wachache ambao ninawajua kuwa bado Wana utoto.

Leo hii mshikaji wangu nimemchana live uvumilivu umenishinda kaja na namba ngeni yeye ndiye kanitafuta halafu anasema nimpange hiyo inakuja kweli ?
Screenshot_2022_0927_194907.jpg

#UziTayari
 
Aisee mimi na wewe tupo sawa katika hili. Huwa sipendi tena na huwa sijibugi kitu baada ya kuanzisha mazungumzo kwa maneno hayo.
Pia wanaotumia X baada ya S, utakuta anasema xaxa au xx baada ya sasa.
 
Moja kwa moja..

Huu mtindo umeshamiri haswa kwa vijana unakuta mtu ameanza kukutext au wewe umeanza kumsalimia baada ya kujibu text yake inayofuata "nipange "au "niambie" mimi mara nyingi hapo huwa mwisho wa kuchat isipokuwa kwa wachache ambao ninawajua kuwa bado Wana utoto.

Leo hii mshikaji wangu nimemchana live uvumilivu umenishinda kaja na namba ngeni yeye ndiye kanitafuta halafu anasema nimpange hiyo inakuja kweli ?View attachment 2369912

#UziTayari
mimi huwa najibu "sina cha kukupanga"
 
Aisee mimi na wewe tupo sawa katika hili. Huwa sipendi tena na huwa sijibugi kitu baada ya kuanzisha mazungumzo kwa maneno hayo.
Pia wanaotumia X baada ya S, utakuta anasema xaxa au xx baada ya sasa.
Xamtaim kipadi zinakuwa ngumu neno s hulipati
 
Anakera yule ambaye umekaa zako kimya,anakutafuta yeye alafu anakwambia "niambie"...
sasa ningekuwa na cha kukwambia si ningekutafuta mimi.
Leo ndio imenitokea hivyo afadhali ningekuwa nimemtafuta mimi inge make sense kusema nipange au niambie .
 
Yaaan mii ukijikoroga ukaniita katika meseji uwa nina majibu ma3 tu..

1. Abee
2. Sema
3. Nipange / niambie

Hiyo Abee siku hizi nimeipunguza kwa baadhi ya watu kuanzia pale kuna mtu ananiita, naitika abee.. anakuja niambie nikiitika hivyo anafeel kuwa loved na mm. Lol

Depal…. Sema/ nipange
🤣🤣 ukiona sipangiki ukichukia piga simu ‘kwenye simu at least uwa naongea vizuri.
 
Back
Top Bottom