Ngoja tuangalie kwa perspective tofauti na watu waliotangulia.
Huwa inasemwa kuwa mtu akikasirika anatoa nguvu hasi na mtu ukiwa kwenye utulivu au amani ya moyo unakuwa unatoa nguvu chanya. Nguvu chanya ni kwa ajili ya ulimwengu wa mwanga na nguvu hasi ni kwa ulimwengu wa giza. Kwa viumbe wa giza moja ya chakula chao kikubwa ni hizo nguvu hasi ambazo bin-adam anazitoa kama matokeo ya kupitia adha au mateso ya kidunia, na ndio maana hawa viumbe wa giza hawaachi kusababisha kila aina matatizo ilimradi tu bin-adam asikae kwa utulivu kwenye dunia, maana akikaa kwa utulivu wao watakosa chao.
So jichunguze vizuri huenda kuna kiumbe kinakutumia kufanya hayo yote bila wewe kujijua. Auuuu, inawezekana wewe sio wewe kama unavyojihisi wewe ni wewe...
Ila usiogope, inawezekana ni tabia ya kawaida au labda ni 'genye' kama walivyo sema waliotangulia.