Tabia ya wadada/wanawake kutosalimia huku Duniani mjiandae kwa mrejesho

Tabia ya wadada/wanawake kutosalimia huku Duniani mjiandae kwa mrejesho

Na ukipendeza huwa wanajifanya kuangalia pembeni kama hakuoni vile kumbe anakuangalia kiaina tena kwa jicho baya na makasiriko kibao.
Kwa nini hasa huwa hivyo? Kwa nini ukijipenda na ukiwa smart SANA wanakuwa wanakuchunia, hawaitikii salamu n.k? Na hasa ukiwa handsome?
 
Naomba wahenga na wadau wa masuala ya jinsia na mshikamano kwenye jamii mtusaidie, hii tabia inayokuwa Kwa kasi ya wadada/ wanawake kutosalimia mzizi wake ni nini.

Binadamu Hazina yake kubwa ni utashi wa kusalimiana. Kusalimia sio kutongozwa, na haimanishi ndio unajenga masndalizi ya kutongozwa Bali ni kuishi utu na Mungu na imani za ubinadamu katika jamii.

Baadhi yetu hatunaga shobo na kiu za kipuuzi tunajali utu na ubinadamu zaidi.

Katika maisha sisi binadamu ni madaraja ya aina mbalimbali katika nyanja mbalimbali za maisha.

Weka Hazina katika safari yako ya maisha popote ulipo.

Matokeo yake.
1. Nimempa lift kisha baada ya mita 20 nimegeuza gari nikamshusha nikamwambia we huna adabu unanikumbuka et eeeh toka kwenye gari yangu. Imeisha hio.

2. Kanikuta ofisi nyeti moja Dodoma, akanichangamkia huyu jini mnaso, nikamuuliza nini shida, akaeleza nikamwambia lete bahasha ntakusaidia. Sijajisumbua dakika 10 tu nimechana bahasha na kila kitu.

3. Aliibiwa simu Iphone halafu mpelelezi wa kesi classmate wangu wa A'level baada ya kuniona nae kaja kuniomba kipereso pereso nisaidie, nikamwambia tafuta laki2 nikala Laki na mwana laki, badaye nikasepa zangu nyamisati kupeleka mchele bado jau anakoma.

Ndio narudi nshapoteza huruma na hawa viumbe. Ntasaidia wenye utu na ubinadamu basi, wengine sina huruma nao.

Ishi na watu vizuri tulio na vijipesa vya kula bata na kujimudu tuna madharau kama yote.

Sio kesi bati bati

😀😀

Wanawake ndivyo walivyo haswa wakiwa katika umri Kati ya kubalehe 15-25
Usiwachukie ni hulka tuu pengine hawakupenda kuwa hivyo.

Ni umri wa wao kujiona wanatamani na kufurahia utukufu na uzuri wao ambao Kwa umri huo ndio wananawiri, baada ya hapo wanakuwa watu wazuri tuu😀

Ni ishu ya ukuaji Mkuu.
Take it Easy.

Sisi wengine huwaga tunawachokoza kabisa maana tunajua wao Kwa umri huo wanajiona wanaimiliki dunia, wapo katika ndoto. Tena wakitutukana ndio tunafurahia😊😊 na inafurahisha Sana.

Kuwaendekeza wanawake WA umri huo ni kutokujiamini tuu. Wengi hawafanyi Kwa utashi au Akili zao.
Ila akiwa above 27 na ana-act hivyo basi jua huyo anamatatizo na ndiye unapaswa umuadhibu.
 
1,2,3....zote umejichora namna moyo wako ulivyo.Jifunze kuwa sikuzote wema hufunika ubaya,lakini pia ubaya hufunika wema....ungemtendea wema ule ubaya aliofanya ungemfunza wema kutokana na wema wako,lakini unaporudisha baya,hajifunzi kitu zaidi kutambua kuwa kumbe nawe una roho mbaya.....Kinachotengenezwa hapo ni chuki....hujatengeneza amani.Tushirikiane kuifanya dunia ni sehemu ya amani na siyo visasi na machafuko
Mh ndugu yangu umeongea kitu mpaka nimejihisi kuhukumiwa asubuhi hii

Shida kuna wengine ni wanaume kama wanawake ila sawa lesson has taken , ahsante.
 
Kusalimia ni kwa wote, kama mtu anategemea yeye ndiye asalimiwe halafu yeye hanisalimii, amegonga mwamba, kwa Sababu ni kitu cha bure.
 
Hapo nawakingia kifua wadada, me kweli pia sipendezwi na tabia yao ya kujikuta kwamba wao ndo wa kuanzwa kwenye kila kitu ila dah! Men asilimia kubwa ndo tunawaharibu hawa viumbe ki-saikolojia hadi kufikia wao kuhisi kila mwanaume ndo ana tabia hizo mbovu za kutongoza kila akionacho mbele.
 
Back
Top Bottom