Tabia ya wadada/wanawake kutosalimia huku Duniani mjiandae kwa mrejesho

Na ukipendeza huwa wanajifanya kuangalia pembeni kama hakuoni vile kumbe anakuangalia kiaina tena kwa jicho baya na makasiriko kibao.
Kwa nini hasa huwa hivyo? Kwa nini ukijipenda na ukiwa smart SANA wanakuwa wanakuchunia, hawaitikii salamu n.k? Na hasa ukiwa handsome?
 

😀😀

Wanawake ndivyo walivyo haswa wakiwa katika umri Kati ya kubalehe 15-25
Usiwachukie ni hulka tuu pengine hawakupenda kuwa hivyo.

Ni umri wa wao kujiona wanatamani na kufurahia utukufu na uzuri wao ambao Kwa umri huo ndio wananawiri, baada ya hapo wanakuwa watu wazuri tuu😀

Ni ishu ya ukuaji Mkuu.
Take it Easy.

Sisi wengine huwaga tunawachokoza kabisa maana tunajua wao Kwa umri huo wanajiona wanaimiliki dunia, wapo katika ndoto. Tena wakitutukana ndio tunafurahia😊😊 na inafurahisha Sana.

Kuwaendekeza wanawake WA umri huo ni kutokujiamini tuu. Wengi hawafanyi Kwa utashi au Akili zao.
Ila akiwa above 27 na ana-act hivyo basi jua huyo anamatatizo na ndiye unapaswa umuadhibu.
 
Mh ndugu yangu umeongea kitu mpaka nimejihisi kuhukumiwa asubuhi hii

Shida kuna wengine ni wanaume kama wanawake ila sawa lesson has taken , ahsante.
 
Kusalimia ni kwa wote, kama mtu anategemea yeye ndiye asalimiwe halafu yeye hanisalimii, amegonga mwamba, kwa Sababu ni kitu cha bure.
 
Hapo nawakingia kifua wadada, me kweli pia sipendezwi na tabia yao ya kujikuta kwamba wao ndo wa kuanzwa kwenye kila kitu ila dah! Men asilimia kubwa ndo tunawaharibu hawa viumbe ki-saikolojia hadi kufikia wao kuhisi kila mwanaume ndo ana tabia hizo mbovu za kutongoza kila akionacho mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…