Tabia ya wanaume kuvaa pens na kuzurura mitaani, ni ukosefu wa Maadili

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam,Shalom!!

Hizi TABIA za kuiga Kila kitu ni mbaya sana, zamani pens na vest za mikono wazi ilikuwa MARUFUKU kuonekana mzazi amevaa nje ya chumba chake,

Hivi sasa mnaangalia kwenye movies na trends za kidunia na kuanza kuvaa vikaptula na kuzurura barabarani, mnaudhi sana.

TABIA za ukosefu wa Maadili huanza Polepole, baba mzazi au kaka mwenye dada zako unapozurura na pens juu ya magoti, utapata wapi ujasiri wa kumwambia dadako au mwanao ajisitiri Kwa mavazi ya Heshima?

Yaani unakuta Mwanaume kavaa kipens juu ya magoti, kimebana nyeti zote, makalio yamejichoraaaa!!!

Acheni TABIA hizi mara Moja Ili mjitofautishe na MASHOGA.

NB: Wanawake piteni kimya, maana hiki ni kikao Cha kiumeni , tunarekebishana.

Ni hayo tu!!
 
Unampangia Nani maamuzi ?! Kila mtu ana maamuzi yake
 
Ni upotofu sana.Haina tofauti na kujitwika taulo kiunoni kwenye nyumba yenye wakazi wengi na watoto.Stupidity of all the time!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…