Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

😍😍😍😍
 
Wewe huwezi kabisa kusali haya makanisa ya manabii wa mwendokasi mana Ibadan inajulikana muda wa kuanza ila muda wa kumaliza haujulikani na apo katikati mambo kibao mara sijui shuhuda na zingine za uongo Aya saa ya kupakwa mafuta ya upako n.k
 
Amen Mtumishi, kama kuna mahali nimepotoka, Mungu aniongoze πŸ™πŸ»
 
Umeongea jambo msingi sana makutupora
 
Asante kwa hoja hii, suala la muda linaweza likawa gumu kwa watu wanaoingia ibadani kutimiza wajibu.
Unahudhuria ibada kwa wiki mara moja, alafu unakerwa na matangazo, Neno la Mungu, kwaya, unataka ufanye ibada nusu uondoke!?

Unaondoka ibadani unaishia kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii, kuongea na marafiki, kulala, kuangalia mpira, Movies, tamthilia, kukaa vijiwe vya kahawa, kukaa kwenye mahoteli.

Kurudiwa matangazo naona sio Jambo baya, huo ni mkazo, kwenye ma TV, ma radio, tunaona tangazo moja linarudiwa kwa siku mara nyingi, mengine yanaenda MIEZI ya kutosha.

Tunapaswa kujiuliza kwanini tunakereka kwa mambo ya ibada, nini kimetukuta, kwanini tusione Jambo jema kukaa kanisani siku ya ibada hasa jumapili?

Muhimu hapa ni kila kitu kwenda kwa utaratibu na mpangilio mzuri, kama vitu havina mpangilio mzuri hapo tuna haja ya kushauri. Wapo wazee wa kanisa au mashemasi kuwafikishia ujumbe wa maboresho vile tunaona inafaa. Tukiona hao hawatafikisha kwa usahihi tuombe kuonana na wachungaji/maaskofu.

Asante
 
Ndo maana kkkt wengi sasa hivi wanajiunga na Wasabato wanajifunza ukweli wa Bibilia wamechoka kudanganywa huko
 
Ndugu zangu katika imani walutheri wenzangu, biblia inasema tusiharakishe kutoka nyumbani mwa BWANA.
Mhubiri 8:3
[3]Usifanye haraka kutoka mbele ya uso wake; usiendelee kufanya lililo baya; maana yeye hufanya lo lote limpendezalo.
Pia kiongozi wetu mkuu Martin Luther, alikuwa ni mtu wa sala na ibada sana,kila siku alisali si chini ya masaa mawili, ndio maana mpaka leo kanisa letu ni moja ya makanisa imara duniani. Hivyo tuendelee kuwa wavumilivu, tusiondoke ibadani kabla ya wakati.
Tufurahie kukaa nyumbani mwa BWANA.
Zaburi 122:1

[1]Nalifurahi waliponiambia,
Na twende nyumbani kwa BWANA.
 

Attachments

  • Screenshot_20250224-090421_1.jpg
    334.6 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…