Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

Mbaga uko vizuri, sisi tulilazimisha matangazo ya Kila siku ( yaliyozoeleka) yawekwe kwenye ubao wa matangazo, lakini hali kuwa jambo dogo! Tuitwa wasaliti. Hio ilikuwa Moro usharika wa kora.
Kuna wale wafia ibada hawawezi kuelewa, ukisema hayo wanakuona una mapepo
 
Yaan mpaka saa 5 Katoliki tushasali ibada nne hapo 😂😂 !
Aah wapi mambo ni yale yale. Kuna kipindi mtu alinambia wako smart sana kwenye muda. Sasa nikaja kuishi naye siku ya J2 nampeleka na kumfata yaani kuna siku namsubiri nje 1hr, mara 30min mara 15min hakuna muda maalum haya makanisa yote viongozi kuna namna wanapaswa kujirekebisha uhuru wao umezidi.
 
Saaa 1hr utafananisha na kushinda kanisani kama mnavyofanya? Na hilo hutokea mara chache sana labda kuna ugeni n.k...
Kuzidisha 15 mnt au 30 kuna ubaya gani...
 
Habari wakuu,

Mimi dhehebu langu ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),

Kanisa letu lina utaratibu wa kufuata kalenda ya mwaka, ni jambo zuri, Lakini kuna haja ya kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya vitu ili kuendana na dunia ya leo

Usomaji wa matangazo ya week,

Kwa dunia ya sasa kuna namna nyingi matangazo kuwafikia waumini, Unakuta mzee wa kanisa kamaliza kusoma matangazo, mchungaji naye anakuja kutolea ufafanuzi wa matangazo yale yale

Ibada binafsi kuunganishwa na ibada za jumapili,

Mfano issue za ubatizo watoto zingefaa zipangiwe muda wa kipekee, Kama ilivyo ibada ya kufunga Ndoa,n.k

Muingiliano wa ratiba nyingi katikati ya ibada unapekea waumini wengi kushindwa kuvumilia kukaa mpaka mwisho, matokeo yake mchungaji akimaliza neno utaona idadi kubwa ya waumini wanaondoka kabla ya Ibada kuisha, hii sio ishara nzuri sana, kama kanisa inabidi kutafakari hili kwa kina

Wote tunajua lengo kuu la ibada ni Kusifu, kuabudu na kupata chakula cha kiroho (Neno la Mungu)
Ibada kuwa ndefu sio tatizo ,ila inategemea ime base upande gani, haya ni mawazo yangu binafsi,

Asanteni
Mimi ni RC, nilidhani hili ni tatizo huku kwetu tu. Ukweli ibada ndefu ni chukizo kwa wakati huu. Jumapili ni mapumziko kwa alie jitosheleza (yupo? Hata yesu alifanya kazi siku ya sabato). Nyimbo, maombi kwa marehemu na matangazo zinachukua muda mrefu sana. Mabadiliko ni muhimu.
 
Hapo hujataja kushiriki Sakrameti ya chakula cha bwana (Ekaristi)...Ibada inaweza enda mpaka saa 8
 
Wakatoliki wajanja. Matangazo na michango tele vipo kwenye jumuiya. Ukileta malalamiko unasemwa kwa paroko na unaweza tengwa kabisa. Yaani nidhamu ya pale ni sawa na ile ya mkutano mkuu wa ccm awamu ya kumteua samia
Ibada ya katoriki
Misa ya kwanza saa 12 :00
Saa 11:45 sala za asubuh na maungamo
12:00 padri kasha anzisha misa iyooo mpka saa mbiki kasoro misa imeisha unarudi nyumbani kunywa chai na kulala padri hana matangazo ya kukazia labda kama kuna ugeni na kama kuna ugeni kutoka redio maria inatangazwa juma pili moja kabla ya wageni kufika
 
Wakatoliki wajanja. Matangazo na michango tele vipo kwenye jumuiya. Ukileta malalamiko unasemwa kwa paroko na unaweza tengwa kabisa. Yaani nidhamu ya pale ni sawa na ile ya mkutano mkuu wa ccm awamu ya kumteua samia
Parokia gani iyo?
 
Back
Top Bottom