Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

Habari wakuu,

Mimi dhehebu langu ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),

Kanisa letu lina utaratibu wa kufuata kalenda ya mwaka, ni jambo zuri, Lakini kuna haja ya kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya vitu ili kuendana na dunia ya leo

Usomaji wa matangazo ya week,

Kwa dunia ya sasa kuna namna nyingi matangazo kuwafikia waumini, Unakuta mzee wa kanisa kamaliza kusoma matangazo, mchungaji naye anakuja kutolea ufafanuzi wa matangazo yale yale

Ibada binafsi kuunganishwa na ibada za jumapili,

Mfano issue za ubatizo watoto zingefaa zipangiwe muda wa kipekee, Kama ilivyo ibada ya kufunga Ndoa,n.k

Muingiliano wa ratiba nyingi katikati ya ibada unapekea waumini wengi kushindwa kuvumilia kukaa mpaka mwisho, matokeo yake mchungaji akimaliza neno utaona idadi kubwa ya waumini wanaondoka kabla ya Ibada kuisha, hii sio ishara nzuri sana, kama kanisa inabidi kutafakari hili kwa kina

Wote tunajua lengo kuu la ibada ni Kusifu, kuabudu na kupata chakula cha kiroho (Neno la Mungu)
Ibada kuwa ndefu sio tatizo ,ila inategemea ime base upande gani, haya ni mawazo yangu binafsi,

Asanteni
Wewe huwezi kabisa kusali haya makanisa ya manabii wa mwendokasi mana Ibadan inajulikana muda wa kuanza ila muda wa kumaliza haujulikani na apo katikati mambo kibao mara sijui shuhuda na zingine za uongo Aya saa ya kupakwa mafuta ya upako n.k
 
Mungu akusaidie utambue kuwa wale ni makuhani wamewekwa na Mungu kutimiza kazi yake. Suala la muda wa ibada kuwa mrefu ni jambo ambalo unaweza kufika ofisi ya mchungaji kiongozi ukatoa ushauri kuliko kuja hapa kulalamikia jambo ambalo wengi wa unaowalalamikia ni ama wa mlengo mwingine au si watu hata wanaoamini uwepo wa Mungu. Pia ufahamu suala la ibada ni nyeti na ni la kiroho kwa hiyo kuhani wa zamu anaweza kutumia muda wa ziada akifundisha au kuombea kwa kadri Roho wa Mungu atakavyomuongoza. Jambo la msingi la kujihoji wewe binafi ni kwa jinsi gani unapoingia ibadani unamwabudu Mungu katika Roho na kweli au unaenda kutimiza desturi tu. Mungu sio wa mazoea.
Amen Mtumishi, kama kuna mahali nimepotoka, Mungu aniongoze 🙏🏻
 
Unajua maisha yako hivi!

Nakupa tafakari yangu ya siku! Huwaga Nina utaratibu wa kuwa thought au wazo la siku la kulitafakari.

Na wazo Hilo Huwa nataka siku zote liwe linanikosoa ili kuniboresha!

Sasa wazo langu la Leo ni hili ... Kila kitu unachotumia muda wako mwingi kuhusiana nacho, kinakufanya ufananane nacho

"Whatever you spend a lot of time with makes you become like it."

Muda wako mwingi unatumia kusoma, kuangalia Nini? Utakuwa Hiko!

Ukipata nafasi ya kuhudhuria semina katikati ya wiki ... Hiyo nafasi ukiwa nayo ... Fanya!

Inakufanya uwe mwepesi kunyaka vitu vya Rohoni na kumsikia na kumuelewa Mungu kwa wepesi sana!

Sio kama Mungu hasemi na sisi, ila nafsi zetu na mioyo yetu imejaa karokoro mengi yenye sauti kubwa sana kuliko Neno la Mungu ndani yetu

Kwa sababu tu hatuna au hatujampa Kipaumbele na muda wa kutosha Katika maisha yetu
Umeongea jambo msingi sana makutupora
 
Asante kwa hoja hii, suala la muda linaweza likawa gumu kwa watu wanaoingia ibadani kutimiza wajibu.
Unahudhuria ibada kwa wiki mara moja, alafu unakerwa na matangazo, Neno la Mungu, kwaya, unataka ufanye ibada nusu uondoke!?

Unaondoka ibadani unaishia kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii, kuongea na marafiki, kulala, kuangalia mpira, Movies, tamthilia, kukaa vijiwe vya kahawa, kukaa kwenye mahoteli.

Kurudiwa matangazo naona sio Jambo baya, huo ni mkazo, kwenye ma TV, ma radio, tunaona tangazo moja linarudiwa kwa siku mara nyingi, mengine yanaenda MIEZI ya kutosha.

Tunapaswa kujiuliza kwanini tunakereka kwa mambo ya ibada, nini kimetukuta, kwanini tusione Jambo jema kukaa kanisani siku ya ibada hasa jumapili?

Muhimu hapa ni kila kitu kwenda kwa utaratibu na mpangilio mzuri, kama vitu havina mpangilio mzuri hapo tuna haja ya kushauri. Wapo wazee wa kanisa au mashemasi kuwafikishia ujumbe wa maboresho vile tunaona inafaa. Tukiona hao hawatafikisha kwa usahihi tuombe kuonana na wachungaji/maaskofu.

Asante
 
Habari wakuu,

Mimi dhehebu langu ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),

Kanisa letu lina utaratibu wa kufuata kalenda ya mwaka, ni jambo zuri, Lakini kuna haja ya kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya vitu ili kuendana na dunia ya leo

Usomaji wa matangazo ya week,

Kwa dunia ya sasa kuna namna nyingi matangazo kuwafikia waumini, Unakuta mzee wa kanisa kamaliza kusoma matangazo, mchungaji naye anakuja kutolea ufafanuzi wa matangazo yale yale

Ibada binafsi kuunganishwa na ibada za jumapili,

Mfano issue za ubatizo watoto zingefaa zipangiwe muda wa kipekee, Kama ilivyo ibada ya kufunga Ndoa,n.k

Muingiliano wa ratiba nyingi katikati ya ibada unapekea waumini wengi kushindwa kuvumilia kukaa mpaka mwisho, matokeo yake mchungaji akimaliza neno utaona idadi kubwa ya waumini wanaondoka kabla ya Ibada kuisha, hii sio ishara nzuri sana, kama kanisa inabidi kutafakari hili kwa kina

Wote tunajua lengo kuu la ibada ni Kusifu, kuabudu na kupata chakula cha kiroho (Neno la Mungu)
Ibada kuwa ndefu sio tatizo ,ila inategemea ime base upande gani, haya ni mawazo yangu binafsi,

Asanteni
Ndo maana kkkt wengi sasa hivi wanajiunga na Wasabato wanajifunza ukweli wa Bibilia wamechoka kudanganywa huko
 
Ndugu zangu katika imani walutheri wenzangu, biblia inasema tusiharakishe kutoka nyumbani mwa BWANA.
Mhubiri 8:3
[3]Usifanye haraka kutoka mbele ya uso wake; usiendelee kufanya lililo baya; maana yeye hufanya lo lote limpendezalo.
Pia kiongozi wetu mkuu Martin Luther, alikuwa ni mtu wa sala na ibada sana,kila siku alisali si chini ya masaa mawili, ndio maana mpaka leo kanisa letu ni moja ya makanisa imara duniani. Hivyo tuendelee kuwa wavumilivu, tusiondoke ibadani kabla ya wakati.
Tufurahie kukaa nyumbani mwa BWANA.
Zaburi 122:1

[1]Nalifurahi waliponiambia,
Na twende nyumbani kwa BWANA.
 
Attachments

  • Screenshot_20250224-090421_1.jpg
    Screenshot_20250224-090421_1.jpg
    334.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom