Tabia ya wazazi kukataa wachumba kisa ukabila ikomeshwe

Tabia ya wazazi kukataa wachumba kisa ukabila ikomeshwe

Ili yasinitokee kama ya jamaa hapo juu kupewa mtoto asie wake. Mi kabla ya kuoa ni lazma nimchunguze kwa kina uyo mtoto wa kike ninaetaka kumuoa yaani ntatumia ujuzi wangu na pesa ikibidi. Walau ujue background yake na familia yake.

Hayo mambo ya kubebana bebana kisa "i love you" nyingi ndio matokeo yake hayo.

Wanawake ni mabingwa wa kupretend aisee hebu fikiria mtu anaweza kua haridhishwi na mpenzi/mume wale lakini bado anajifanya anampenda kwa muda hata miaka anamlia timing tu.
Kuna nyuzi humu wadada wanaelezda jinsi wanavowavulia wanaume wasiowapenda ila wameolewa nao tu na ni miaka kibao.
Tofauti kabisa na sisi wanaume huwa hatukopeshi aisee kwanza tu ukininyima tunda utaona tu nishaanza kukubadilikia mapemaa.

Ni vizuri kuelewana kabla ya ndoa hasa kwa sisi wakristo ambao tunaoa mke mmoja wa maisha. Hawa ndgu zetu wenyewe dini inawabeba kupiga chini na kuchukua vyuma hata vinne.
 
Siungi mkono wazazi kukupangia Mke. Ila pia ni vema kuwasikiliza na maamuzi yakabaki kwako.

Fuatilia ndoa nyingi ambazo zimesambaratika 80% ni wale waliooana kabila tofauti.

Ndoa za kabila moja suala la kuvumiliana ni kubwa, suala la kujaliana ni kubwa, suala la kuheshimiana ni kubwa, suala la kuhurumiana ni kubwa nk, yaani kunakuwa na Bond zaidi ya mke na mume.

Sisemi haya hayapo katika wana ndoa wa kabila tofauti, hapana, yapo lakini kwakiasi kikubwa ni kipindi cha neema ya mali, nafasi ya kazi na afya imara ambapo mke na ndugu zake watakuita majina yote mazuri(Tall hata kama upo kama Pierre).bali idadi kubwa mwisho unakuwa sio mzuri .

Mwanamke wa Kabila lako hawezi kumnyanyapaa Mume wake katika hali yoyote.

Refer kwenye Bible wakati Yakobo alipotaka kijana wake Isaka aoe mke, je ni kwanini aliagiza mke akachukuliwe kwa watu wa Jamii yake.

Kwa wenye umri kuanzi miaka 40 nadhani watanielewa zaidi kwani ndicho kipindi halisi cha kujua Rangi halisi ya Mke uliyenaye na backup ya ndugu zake.

Through my own experience katika umri huu miaka 56 sijawahi kushuhudia migogoro ya ndoa ama divorce kwa wana ndoa wa kabila Moja NINAPOFANYIA KAZI , But migogoro mingi niliyoshuhudia na ninayozidi kushuhudia ni za kabila tofauti.

Ninachoamini ndoa za kabila Moja wanakuwa na migogoro lakini ni rahisi kusitiriana ndani na ikizidi litaishia kwa wazazi au katika madhehebu yao. Lakini ndoa za kabila tofauti moto kidogo tu lazima ukolezwe na Petroli . Kesi za ndoa nyingi Mahakamani zinajieleza.

Hivyo Vijana nashauri wasikilizeni wazee wenu japo Maamuzi yabaki Kwenu
 
Haipendezi kabisa wawili wanapopendana wazazi kuingilia mahusiano yao.
 
Hahaaaaa hatari sana kijana wa watu kashapewa hadi mgongo leo hii eti mzazi anakataa thubutuuuuuu
 
Niite mshamba au jina lolote lkn siwezi kukubali mwanangu aolewe na mkuria , muha au msukuma. These three tribes are very primitive.
Hata awe kakulia Masaki, msukuma Ni msukuma tu.

Acha ukabila wewe, kwani wasukuma sio watu?
 
Niite mshamba au jina lolote lkn siwezi kukubali mwanangu aolewe na mkuria , muha au msukuma. These three tribes are very primitive.
Hata awe kakulia Masaki, msukuma Ni msukuma tu.
Mkuu wewe kabila gani ?
 
Ukiwa huna pesa unadharaulika tu haijalishi kabila gani, mbona Kina Ben pol, Lemutuz, Waziri wa mambo ya ndani, waziri wa katiba na wako wengi tu heshima juu. Ukiwa na pesa hata kabila yako huulizwi.
Lemutuz anaheshimiwa na nani ?
 
Kwakweli kwenye suala la kuoa hakuna mtu anaweza niamulia bali anaweza kunishauri tu, Suala la kuamua litakuwa langu mwenyewe, Ili nkilikoroga nilinywe mwenyewe habari yakuanza kulaumu wazazi wangu sitak kabisa na ili lisitokee siwapi nafasi ya kuniamulia
 
Kuna makabila hayaachi asili hata uwatie chumvi.
Mfano...
Mkuria anaamini bila kumpiga mke atadharaulika.
Muha anaamini bila ushirikina na kupinga kila kitu mambo hayaendi.
Mchaga bila kufanya zile Mila mambo hayatakaa sawa.
Mpare anaimani ubahili ndio Maisha ya kumfunza mtoto.
Mkinga anaamini kazi ya hela Ni kuhifadhiwa na sio kutumiwa.
Mnyakyusa especially wanawake wanaamini wao ndio watu Bora kabisa wakati shepu hawana.
Wazaramo tunaamini ngoma ndio msingi wa Maisha ndio maana huwezi kumkuta mzaramo mwenye stress hata awe maskini vipi.
Wasukuma matatizo yenu kila mtu anayajua.
Wahaya kwa misifa hamjambo, mhitimu wa VETA anaitwa injinia.
Wanyamwezi Ni shemeji zangu nawakubali sana
 
Back
Top Bottom