Tabora: Anayeidai TRA Milioni 986, Ramadhani Ntuzwe adaiwa 'kujiua kwa risasi'

Tabora: Anayeidai TRA Milioni 986, Ramadhani Ntuzwe adaiwa 'kujiua kwa risasi'

Mwaka jana nilikua Urambo nilifika pale dukani kwake kununua bidhaa. alilipwa na TRA, na alikuwa ameexpand sana biashara yake ya bidhaa-duka la jumla likawa kubwa, akajenga warehouse, akawa na malori ya kusupply vijijini. Bado alikua na misuguano na maafisa wa TRA na walikuwa na mitego mingi, though jamaa alikuwa smart sana kulipa kodi na kutumia technology. Hii expansion ya biashara za bidhaa kwa pale Urambo, ilimpa maadui wapya-WAARABU WAFANYABIASHARA YA BIDHAA pale Urambo. Hawa waarabu wamejenga monopoly attittude kiasi huwa hawataki supplier mpya sokoni tena awe na bei za chini kuliko wao.

Kwa kweli nimemumizwa na habari za kifo cha Ntunzwe. Apumzike kwa amani. Biashara zake ndio zimefika mwisho. Inaumiza sana.
Weka ushahidi kuwa alilipwa.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna atakaelipa. The government belongs to nobody. Siku utakayojua serekali ni karatasi ndio utajua

Nadhani wewe hukijui kisasi Cha Mungu, haki ya mtu haipotei mtalipa tena kwa machozi. Hadi uje ujue kwanini unaumia kilio kitakuwa chako tutosha. Ombi tu Mungu aturehemu na iwe kifochake isiwe sababu za kibiashara.
 
Mfanyabiashara Ramadhani Ntuzwe ‘Babu Rama’ aliyekuwa akipaza sauti katika vyombo mbalimbali vya habari kwa takriba miaka saba kwamba anaida fidia ya Sh 986 milioni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), anadaiwa kujiua kwa risasi leo Jumatano Machi 6, 2024 nyumbani kwake Urambo mkoani Tabora.

Meneja wa mfanyabiashara huyo, Msifuni Myava amethibitisha kutokea kwa kifo cha bosi wake na kudai kuwa amejipiga risasi ya kichwa na kupoteza maisha akiwa amejifungia dukani kwake.

Mfanyabiashara huyo kwa mara ya kwanza aliwasilisha kilio chake tarehe 28 Februari 2019 katika kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wafanyabiashara wa Ilala ikiwa ni
miezi saba tangu alipokutana na mkasa huo tarehe 30 Oktoba 2016 alipokuwa akisafirisha mzigo wake kutoka Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma kuelekea Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Ntunzwe alieleza mikasa miwili iliyomkuta dhidi ya TRA; kwanza kushikilia mzigo wake kwa miaka mitatu kwa tuhuma za kukwepa kukodi huku yeye akidai
kukataa kutoa rushwa ya Sh2milioni na mkasa wa pili ni kuibiwa mali zake zenye thamani ya Sh986 milioni katika duka lililopo Kariakoo baada ya TRA kulifunga kwa madai ya kutotumia mashine ya EFD.

Chanzo: Mwanahalisi
Amejiua au AMEUAWA ili kuondoa kero ya kudaiwa??????
 
Kukata tamaa ni kosa kubwa sana, pigana mpaka mwisho ili haki ipatikane. Hawa waheshimiwa wa TRA wanajisikiaje na hicho kifo?
 
Na ni kafsnya uchunguzi kuwa kajiua? Kama, ni polisi wetu hawa! Ambao, hudai maabusu kajinyonga kwa kamba ya, kufungia viatu! I, smell fishy, its faul play,!
Kwa, mpunga ule acha kabisa,
Kuna polisi, wapo, maahabusu kwa kuua kwa sababu ya milioni 30 tu, sembuse billions kasoro!
 
Mfanyabiashara Ramadhani Ntuzwe ‘Babu Rama’ aliyekuwa akipaza sauti katika vyombo mbalimbali vya habari kwa takriba miaka saba kwamba anaida fidia ya Sh 986 milioni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), anadaiwa kujiua kwa risasi leo Jumatano Machi 6, 2024 nyumbani kwake Urambo mkoani Tabora.

Meneja wa mfanyabiashara huyo, Msifuni Myava amethibitisha kutokea kwa kifo cha bosi wake na kudai kuwa amejipiga risasi ya kichwa na kupoteza maisha akiwa amejifungia dukani kwake.

Mfanyabiashara huyo kwa mara ya kwanza aliwasilisha kilio chake tarehe 28 Februari 2019 katika kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wafanyabiashara wa Ilala ikiwa ni
miezi saba tangu alipokutana na mkasa huo tarehe 30 Oktoba 2016 alipokuwa akisafirisha mzigo wake kutoka Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma kuelekea Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Ntunzwe alieleza mikasa miwili iliyomkuta dhidi ya TRA; kwanza kushikilia mzigo wake kwa miaka mitatu kwa tuhuma za kukwepa kukodi huku yeye akidai
kukataa kutoa rushwa ya Sh2milioni na mkasa wa pili ni kuibiwa mali zake zenye thamani ya Sh986 milioni katika duka lililopo Kariakoo baada ya TRA kulifunga kwa madai ya kutotumia mashine ya EFD.

Chanzo: Mwanahalisi
Karibu Africa, Bara ambalo huwezi kupambana na serikali, chaajabu wanatuambia tulipata uhuru! Ni uhuru au ukoloni wa watu weusi?
 
Back
Top Bottom