Tabora: Anayeidai TRA Milioni 986, Ramadhani Ntuzwe adaiwa 'kujiua kwa risasi'

Tabora: Anayeidai TRA Milioni 986, Ramadhani Ntuzwe adaiwa 'kujiua kwa risasi'

Duh kichwa cha mtu kina mengi yaani sijui naonaje mtu anafikiria Mpaka kujiua
Nililetaga thread hapa nikilaani wasaliti, wadhulumati na waonevu nikadhihakiwa na kukejeliwa sijui nimerukwa na akili sijui bange wakati bange ni msaada sana mwangu. Ila sasa hivi Mungu kunisaidia kanipa faraja nimemuachia nakusahau.

Watu8 adriz Accumen Mo Mufti kuku The Infinity
 
Nililetaga thread hapa nikilaani wasaliti, wadhulumati na waonevu nikadhihakiwa na kukejeliwa sijui nimerukwa na akili sijui bange wakati bange ni msaada sana mwangu. Ila sasa hivi Mungu kunisaidia kanipa faraja nimemuachia nakusahau.

Watu8 adriz Accumen Mo Mufti kuku The Infinity
Kumbe ilikuwa ni kweli sio bange ! tatizo haukufunguka zaidi halafu mods wameweka jukwaa la jokes ule Uzi ndio maana watu tukakudhihaki , anyway liwalo na liwe .
 
Mwaka jana nilikua Urambo nilifika pale dukani kwake kununua bidhaa. alilipwa na TRA, na alikuwa ameexpand sana biashara yake ya bidhaa-duka la jumla likawa kubwa, akajenga warehouse, akawa na malori ya kusupply vijijini. Bado alikua na misuguano na maafisa wa TRA na walikuwa na mitego mingi, though jamaa alikuwa smart sana kulipa kodi na kutumia technology. Hii expansion ya biashara za bidhaa kwa pale Urambo, ilimpa maadui wapya-WAARABU WAFANYABIASHARA YA BIDHAA pale Urambo. Hawa waarabu wamejenga monopoly attittude kiasi huwa hawataki supplier mpya sokoni tena awe na bei za chini kuliko wao.

Kwa kweli nimemumizwa na habari za kifo cha Ntunzwe. Apumzike kwa amani. Biashara zake ndio zimefika mwisho. Inaumiza sana.
Alikuwa na biashara zipi na zipi?
 
Bora kupata hasara ila dhulma ,hata shilling elfu 10 roho inauma kinoma.
Ramadhani Ntunzwe kwa maelezo yake kwenye video clip ambazo zipo Youtube Mwaka 2019 alieleza kuwa Kesi yake ilifika hadi Ikulu na kujadiliwa, pia alisema alifikisha kwa Katibu Mkuu CCM dodoma wakati huo Dr Bashiru Ally.

Jambo moja la kushangaza ni kuwa Kesi ikiwa Mahakamani alidai kuwa anatishiwa kuuawa.

Sasa kisa hiki cha kujiua kinatia mashaka sana.
 
Kalalamika kwa waziri bila bila
Kalalamika kwa waziri mkuu(ikaishia suala lako litafanyiwa kazi)bila bila
Vyombo vyote vya sheria bila bila
Nchi hii watu wana dhuluma sana
Naona sahv hai anaowadai wanacheka tu

Ova
Ukifatilia video zake kule Youtube anaeleza vizuri sana hatua kwa hatua ameshirikisha Swala lake kwa Vigogo wengi wa serikali.

Cha kushangaza hakuwa anapata majibu ya kuridhisha, Walikuwa wanakubali kuwa anastahili fedha zake zirudi hadi wakapanga namna ya malipo.....Kidogo kidogo.

Sasa kama ameamua kujiua pengine ni sababu nyingine lakini hili swala lake nila kiuchunguzi zaidi.
 
Back
Top Bottom