Tabora: Anayeidai TRA Milioni 986, Ramadhani Ntuzwe adaiwa 'kujiua kwa risasi'

Tabora: Anayeidai TRA Milioni 986, Ramadhani Ntuzwe adaiwa 'kujiua kwa risasi'

Ramadhani Ntunzwe kwa maelezo yake kwenye video clip ambazo zipo Youtube Mwaka 2019 alieleza kuwa Kesi yake ilifika hadi Ikulu na kujadiliwa, pia alisema alifikisha kwa Katibu Mkuu CCM dodoma wakati huo Dr Bashiru Ally.

Jambo moja la kushangaza ni kuwa Kesi ikiwa Mahakamani alidai kuwa anatishiwa kuuawa.

Sasa kisa hiki cha kujiua kinatia mashaka sana.
Nchi hii ni ya ajabu sana

Ova
 
Mfanyabiashara Ramadhani Ntuzwe ‘Babu Rama’ aliyekuwa akipaza sauti katika vyombo mbalimbali vya habari kwa takriba miaka saba kwamba anaida fidia ya Sh 986 milioni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), anadaiwa kujiua kwa risasi leo Jumatano Machi 6, 2024 nyumbani kwake Urambo mkoani Tabora.

Meneja wa mfanyabiashara huyo, Msifuni Myava amethibitisha kutokea kwa kifo cha bosi wake na kudai kuwa amejipiga risasi ya kichwa na kupoteza maisha akiwa amejifungia dukani kwake.

Mfanyabiashara huyo kwa mara ya kwanza aliwasilisha kilio chake tarehe 28 Februari 2019 katika kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wafanyabiashara wa Ilala ikiwa ni
miezi saba tangu alipokutana na mkasa huo tarehe 30 Oktoba 2016 alipokuwa akisafirisha mzigo wake kutoka Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma kuelekea Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Ntunzwe alieleza mikasa miwili iliyomkuta dhidi ya TRA; kwanza kushikilia mzigo wake kwa miaka mitatu kwa tuhuma za kukwepa kukodi huku yeye akidai
kukataa kutoa rushwa ya Sh2milioni na mkasa wa pili ni kuibiwa mali zake zenye thamani ya Sh986 milioni katika duka lililopo Kariakoo baada ya TRA kulifunga kwa madai ya kutotumia mashine ya EFD.

Chanzo: Mwanahalisi
binafsi yangu siwezi nikaamini uyu mtu kajimaliza mwenyew na mikono yake,hata mwenda wazimu hawezi kuamini ili swala,hapa tuliachie jeshi la polisi kwa uchunguzi wa kina RIP
 
07 March 2024
Urambo, Tabora

Habari za kina kutoka Urambo Tabora

AFARIKI KWA MADAI YA KUJIPIGA RISASI - RAMADHAMI NTUNZWE MFANYABIASHARA MKUBWA URAMBO


View: https://m.youtube.com/watch?v=CVpgD89KkHc
umati wa watu mbele ya Supermarket ya Ramadhani Ntunzwe

mfanyabiashara mkubwa wa bidhaa za jumla na rejareja wilayani urambo mkoani Tabora Bw. Ramadhani Ntunzwe katika kitongoji cha sanjenti Yohana kata ya Kiyungi Urambo Tabora Tanzania zilizowashitua watu wengi huku umma wa watu wakitiririka kwa kasi kuelekea eneo la tukio lilopo Jengo la biashara la Supermarket ya Bw. Ramadhani Ntunzwe...

Bw. Sudi Sadiki Mgalula mwenyekiti wa kitongoji cha Sajenti Yohana Uyui Urambo Tabora anaelezea jinsi alivyotaarifiwa tukio hilo la simanzi na kufika katika la mfanyabiashara baada ya kutaarifu polisi ...

Sudi Sadiki Mgalula anasema baada ya kufiki na polisi waliongea na shemeji wa marehemu Ramadhani Ntunzwe kuwa cha kusikitisha kulipatika taarifa asubuhi kutoka Kalinzi Kigoma kuwa kuna msiba kaka yake bw. Ramadhani Ntunzwe hivyo walikuwa wamejipanga kufunga kwa muda leo biashara na maduka kutokana na msiba wa Kigoma ndipo baadaye Bw . Ramadhani Ntunzwe alijifungia ndani ya Supermarket .....

Naye chifu Nyangoma Lubungira mfanyabiasha wa soko kuu Urambo Tabora ambaye ni binamu wa marehemu Ramadhani Ntunzwe anaeleza kuwa marehemu walianza biashara naye Urambo Tabora miaka mingi kisha marehemu Ramadhani Ntunzwe kuamua kuhamia Dar es Salaam kuendelea na biashara kabla ya kurudi na kuwekeza tena nguvu Tabora ....

Taarifa za msiba wa Kalinzi Kigoma pia Ramadhani Ntunzwe alizipata mapema asubuhi hivyo pamoja na foreman wa shughuli zake za biashara ambaye ni ndugu yake Bw. Shabaha Hamisi Ntunzwe na wafanyakazi wengine waliamua kujitayarisha jinsi ya kusimamia shughuli kabla ya kwenda kuhani msiba wa Kigoma.

Jamii ya wana Urambo imestushwa na pia kusikitika kwa kuwa marehemu alikuwa na mipango mikubwa ya kuibadilisha Urambo hususan katika sekta ya kibiashara ...

Source : COH - STUDIO
 
Ngumu kumeza ,mtu alilalamika kwamba wanataka kumuua na yeye aksema kwamba hawamuwezi ,lakini unaambiwa kajipiga risasi wakati alikuwa bado anafauatilia mpunga wake.

WILD-CE hawashindwi kitu hao jamaa.
 
Taarifa ya kifo ni sahihi lakini sababu ya kifo inaleta mashaka makubwa
nimesoma huu uzi lakini cha kushangaza sijaona mahali labda kuna taarifa ya polisi, labda hospitali,ndugu au rafiki wa karibu. Watu siku hizi vichwani tuna mambo mengi mno. Nilichokiona mleta uzi ni kama vile anawarushia tra kesi hii bila kufatilia undani wa sababu. je kama mke wake kachit kashindwa vumilia? je kama anamaradhi ambayo kaona hawezi pona na yanamsumbua mno? je kama kadhulumu anatafutwa? tusiwe wepesi kutafuta sababu bila fanya utafiti na kupata majibu sahihi kwenye vyanzo sahihi. Wangapi wanaidai tra na wangapi wanadaiwa na tra na hujasikia wamejiua. kudai au kudaiwa ni kitu cha kawaida ulimwengu wa sasa hasa kwa nchi zetu hizi ukizingatia tunafanya biashara. Je kama kalogwa na nyumba ndogo ili achukue mali?
 
Ngumu kumeza ,mtu alilalamika kwamba wanataka kumuua na yeye aksema kwamba hawamuwezi ,lakini unaambiwa kajipiga risasi wakati alikuwa bado anafauatilia mpunga wake.

WILD-CE hawashindwi kitu hao jamaa.

Inawezekana aliyefariki huko Kalinzi Kigoma naye alikuwa karibu sana kibiashara na marehemu Ramadhani Ntunzwe hivyo msiba wa Kalinzi Kigoma ukawa ni pigo jingine kubwa katika mipango aliyokuwa nayo.

Yote kwa yote uchunguzi wa kiPolisi utatupa picha sahihi ya tukio hili kubwa la Urambo Tabora.
 
Mwaka jana nilikua Urambo nilifika pale dukani kwake kununua bidhaa. alilipwa na TRA, na alikuwa ameexpand sana biashara yake ya bidhaa-duka la jumla likawa kubwa, akajenga warehouse, akawa na malori ya kusupply vijijini. Bado alikua na misuguano na maafisa wa TRA na walikuwa na mitego mingi, though jamaa alikuwa smart sana kulipa kodi na kutumia technology. Hii expansion ya biashara za bidhaa kwa pale Urambo, ilimpa maadui wapya-WAARABU WAFANYABIASHARA YA BIDHAA pale Urambo. Hawa waarabu wamejenga monopoly attittude kiasi huwa hawataki supplier mpya sokoni tena awe na bei za chini kuliko wao.

Kwa kweli nimemumizwa na habari za kifo cha Ntunzwe. Apumzike kwa amani. Biashara zake ndio zimefika mwisho. Inaumiza sana.
Hajalipwa.
Kuna mahojiano ya ndugu na kiongozi wa wafanyabiashara wa eneo husika amesema bado.
Mahojiano na chombo Cha habari kwa njia ya simu yamefanyika baada ya kifo cha huyu mdau.
 
Inawezekana aliyefariki huko Kalinzi Kigoma naye alikuwa karibu sana kibiashara na marehemu Ramadhani Ntunzwe hivyo msiba wa Kalinzi Kigoma ukawa ni pigo jingine kubwa katika mipango aliyokuwa nayo.

Yote kwa yote uchunguzi wa kiPolisi utatupa picha sahihi ya tukio hili kubwa la Urambo Tabora.

Watuhumiwa ndiyo wachunguze mkuu? Hapo case closed ,mission accomplished.
 
Mwaka jana nilikua Urambo nilifika pale dukani kwake kununua bidhaa. alilipwa na TRA, na alikuwa ameexpand sana biashara yake ya bidhaa-duka la jumla likawa kubwa, akajenga warehouse, akawa na malori ya kusupply vijijini. Bado alikua na misuguano na maafisa wa TRA na walikuwa na mitego mingi, though jamaa alikuwa smart sana kulipa kodi na kutumia technology. Hii expansion ya biashara za bidhaa kwa pale Urambo, ilimpa maadui wapya-WAARABU WAFANYABIASHARA YA BIDHAA pale Urambo. Hawa waarabu wamejenga monopoly attittude kiasi huwa hawataki supplier mpya sokoni tena awe na bei za chini kuliko wao.

Kwa kweli nimemumizwa na habari za kifo cha Ntunzwe. Apumzike kwa amani. Biashara zake ndio zimefika mwisho. Inaumiza sana.
Kweli kabisa yaani huo mkoa umetawaliwa na wafanyabiashara wakiarabu na kama wamemiliki mkoa, kuna jamaa tu Sikonge mafuta yanasumbua mpaka utembee km 18 ndio ukute kituo cha mafuta yaani basi tu
 
Miaka zaidi ya mitatu kushughulikia tatizo TRA walishindwa kweli? Au kuna kingine?
Sio miaka 3..uyu kaporwa bidhaa zake na t.r.a toka 2016,,then 2017 t.r.a hao hao wakaliweka duka lake chini Yao na Yale makufuli Yao na mlinzi wao..siku anakuja kukabidhiwa duka lake anakuta million sitini na hazipo na dola elfu 17 za kimarekan hazipo...

Plus mzigo wa shiling million mianane na.....
 
Nchi hii ni ya ajabu sana

Ova
Huyu jamaa kuna uwezekano ameuawa. Mimi ni mmoja ya watu waliokuwa wanafuatilia sakata lake kwa muda mrefu. Kwenye maelezo yake mengi alikuwa anasema jinsi anavyowindwa na jinsi alikuvyokuwa anaitwa na wahusika kwenye mazingira ya kutatanisha na kukoswa koswa. Itakuwa ni lile kundi lilimlia timing likamuua kwa risasi halafu wakazusha kuwa amejiua mwenyewe.
 
Back
Top Bottom