Tabora: Anayeidai TRA Milioni 986, Ramadhani Ntuzwe adaiwa 'kujiua kwa risasi'

Tabora: Anayeidai TRA Milioni 986, Ramadhani Ntuzwe adaiwa 'kujiua kwa risasi'

nimesoma huu uzi lakini cha kushangaza sijaona mahali labda kuna taarifa ya polisi, labda hospitali,ndugu au rafiki wa karibu. Watu siku hizi vichwani tuna mambo mengi mno. Nilichokiona mleta uzi ni kama vile anawarushia tra kesi hii bila kufatilia undani wa sababu. je kama mke wake kachit kashindwa vumilia? je kama anamaradhi ambayo kaona hawezi pona na yanamsumbua mno? je kama kadhulumu anatafutwa? tusiwe wepesi kutafuta sababu bila fanya utafiti na kupata majibu sahihi kwenye vyanzo sahihi. Wangapi wanaidai tra na wangapi wanadaiwa na tra na hujasikia wamejiua. kudai au kudaiwa ni kitu cha kawaida ulimwengu wa sasa hasa kwa nchi zetu hizi ukizingatia tunafanya biashara. Je kama kalogwa na nyumba ndogo ili achukue mali?
Siku hizi wahalifu huanza kutoa habari kwanza kabla ya wahusika wa uchunguzi kutoa taarifa...
 
Mfanyabiashara Ramadhani Ntuzwe ‘Babu Rama’ aliyekuwa akipaza sauti katika vyombo mbalimbali vya habari kwa takriba miaka saba kwamba anaida fidia ya Sh 986 milioni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), anadaiwa kujiua kwa risasi leo Jumatano Machi 6, 2024 nyumbani kwake Urambo mkoani Tabora.

Meneja wa mfanyabiashara huyo, Msifuni Myava amethibitisha kutokea kwa kifo cha bosi wake na kudai kuwa amejipiga risasi ya kichwa na kupoteza maisha akiwa amejifungia dukani kwake.

Mfanyabiashara huyo kwa mara ya kwanza aliwasilisha kilio chake tarehe 28 Februari 2019 katika kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wafanyabiashara wa Ilala ikiwa ni
miezi saba tangu alipokutana na mkasa huo tarehe 30 Oktoba 2016 alipokuwa akisafirisha mzigo wake kutoka Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma kuelekea Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Ntunzwe alieleza mikasa miwili iliyomkuta dhidi ya TRA; kwanza kushikilia mzigo wake kwa miaka mitatu kwa tuhuma za kukwepa kukodi huku yeye akidai
kukataa kutoa rushwa ya Sh2milioni na mkasa wa pili ni kuibiwa mali zake zenye thamani ya Sh986 milioni katika duka lililopo Kariakoo baada ya TRA kulifunga kwa madai ya kutotumia mashine ya EFD.

Chanzo: Mwanahalisi
Katika kikao hicho, Ntunzwe alieleza mikasa miwili iliyomkuta dhidi ya TRA; kwanza kushikilia mzigo wake kwa miaka mitatu kwa tuhuma za kukwepa kukodi huku yeye akidai
kukataa kutoa rushwa ya Sh2milioni na mkasa wa pili ni kuibiwa mali zake zenye thamani ya Sh986 milioni katika duka lililopo Kariakoo baada ya TRA kulifunga kwa madai ya kutotumia mashine ya EFD.
 
Nimefanikiwa kumsikiliza huyu mfanyabiashara akielezea namna ambavyo sakata lake limeanza mpaka mwisho,
Kuna watu katika taasisi za umma ni wakatili sana,na sheria kali ndio dawa pekee,wengine ni kunyonga ili kila mmoja na amheshimu mwingine,
Nimewahi kusikia pia kati ya hao wafanyabiashara wakubwa ukiingiza mali inayoshabihiana na biashara zao ama kushindana na bidhaa zao watafanya kila namna ili wakupoteze kwenye ramani ya biashara,sijui kama lina ukweli!!

Nimepatwa na ghadhabu sana,nimeandika zaidi ya mara mbili
 
Mwaka jana nilikua Urambo nilifika pale dukani kwake kununua bidhaa. alilipwa na TRA, na alikuwa ameexpand sana biashara yake ya bidhaa-duka la jumla likawa kubwa, akajenga warehouse, akawa na malori ya kusupply vijijini. Bado alikua na misuguano na maafisa wa TRA na walikuwa na mitego mingi, though jamaa alikuwa smart sana kulipa kodi na kutumia technology. Hii expansion ya biashara za bidhaa kwa pale Urambo, ilimpa maadui wapya-WAARABU WAFANYABIASHARA YA BIDHAA pale Urambo. Hawa waarabu wamejenga monopoly attittude kiasi huwa hawataki supplier mpya sokoni tena awe na bei za chini kuliko wao.

Kwa kweli nimemumizwa na habari za kifo cha Ntunzwe. Apumzike kwa amani. Biashara zake ndio zimefika mwisho. Inaumiza sana.
Dah ..uchawi.
 
HAIWEZEKANI UFE KWA STYLE HYO TENA UNA CHA MOTO,ANGEWAFUATA HUKO HUKO HAO WAZULAMAJI TRA WAFE NAO IKIWEZEKANA PIGAMOTO OFISI YOTE YA TRA KIGAIDI PAMOJA NAO NDANI NA IWE FUNDISHO KWA HAO MANYANGAU.PUMBAVUU KABISA.
Angekua ameondoka kishujaa sana
 
TRA ni matapeli wa walijivika mkaguzi mkuu CIG mwenyewe ni cha mtoto.ukipata kazi TRA sawa na wasiojulikana.
Mimi niliacha kufanya kazi ambazi nikiona kodi ni ya TRA naacha kabisa maana ni kutapeliana tu
 
Hii nchi kuwa mwekezaji mzawa tabu..kuwa tajiri bila kulamba makalio ya serikali tabu...yani ni tabu everywhere....
Ndio maana wengine tukila kiugali na mchicha basi🤲,
Hizo hela nazo ni tabu tu ukiwa nazo.
Uhai muhimu.
 
Huyu ndio yule Ambaye mpka nyumba yake ilikatiwa umeme?
TRA wakamfuata mpaka kwake usiku? Wakakamata na gari yake iliyokua na mzigo?

Kama ni kweli kajiua, amezingua, Sio kwa kujiua, ila kama imefikia mtu uamue kujiua, unaondokaje Mwenyewe uwaache watesi?

Kujiua tuu ni Dhambi huko uendako, Kuwaacha hai watesi hakupunguzi chochote, Zaidi angesaidia wengine unaowaacha..


Ila Amini, Kua Tajiri na huna connection na Serikali au ajira ya serikali nchi hii bado ni ndege aliekosa kiota,

Ndio naelewa, kwanini unakuta jitu lina pesa ndefu, ila haachi viajira vya serikali vyenye mshahara mdogo.
 
HAIWEZEKANI UFE KWA STYLE HYO TENA UNA CHA MOTO,ANGEWAFUATA HUKO HUKO HAO WAZULAMAJI TRA WAFE NAO IKIWEZEKANA PIGAMOTO OFISI YOTE YA TRA KIGAIDI PAMOJA NAO NDANI NA IWE FUNDISHO KWA HAO MANYANGAU.PUMBAVUU KABISA.
Hata Mimi ndio nilikuwa nawaza hivyo hivyo kwanini ajiue peke yake ?
Yaani Meneja na Meneja wa Kodi unawaomba kikao tena unawaambia kabisa tuje tuyaweke sawa hapo ofisini kwenu. Mnakaa wote meeting room unaanza kuwashona risasi za vichwa wote na Wewe unajimaliza tu. Amekufa Kinyonge sana huyu Jamaa.
 
Back
Top Bottom