Mwaka jana nilikuwa Urambo nilifika pale dukani kwake kununua bidhaa. Alilipwa na TRA, na alikuwa ameexpand sana biashara yake ya bidhaa-duka la jumla likawa kubwa, akajenga warehouse, akawa na malori ya kusupply vijijini.
Bado alikua na misuguano na maafisa wa TRA na walikuwa na mitego mingi, though jamaa alikuwa smart sana kulipa kodi na kutumia technology. Hii expansion ya biashara za bidhaa kwa pale Urambo, ilimpa maadui wapya-WAARABU WAFANYABIASHARA YA BIDHAA pale Urambo. Hawa waarabu wamejenga monopoly attitude kiasi huwa hawataki supplier mpya sokoni tena awe na bei za chini kuliko wao.
Kwa kweli nimemumizwa na habari za kifo cha Ntunzwe. Apumzike kwa amani. Biashara zake ndio zimefika mwisho. Inaumiza sana.