DOKEZO Tabora Mjini hali tete, mafuta hakuna! Maji hakuna

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ngoja uzi huu tum tag Lucas mwashambwa
Maana yuko karibu na mfumo,ataufanyia kazi matatizo yenu huko

Ova
 
Ngoja uzi huu tum tag Lucas mwashambwa
Maana yuko karibu na mfumo,ataufanyia kazi matatizo yenu huko

Ova
Wawe na subiri maana serikali yao ipo kazini muda wote ,hailali wala kusinzia hata sekunde moja katika kuhakikisha inawapatia watanzania huduma bora zitakazo kidhi mahitaji yao. Serikali ya mama inafanya kazi ya kuhakikisha kuwa inamfikia kila mtanzania popote pale alipo.Ni serikali ya kazi,ni serikali ya kuwafuta watu machozi,ni serikali ya kuwapa watu matumaini hai,ni serikali ya kuwapatia watu Tabasamu,furaha na vicheko na ni serikali ya kuwatua watu mizigo ya kero na changamoto mbalimbali.

Waendelee kuiamini serekali yao na kumwamini Mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan.
 
Wakuu, binafsi sijui nchi inapo elekea. Tangu jana nimezunguka vituo vyote vya mafuta "fuel stations" wanasema mafuta yameisha, lakini kimtazamo inaonekana wazi kuna shida mahali ambayo imepelekea wafanya biashara hao kuamua kugoma kuuza mafuta.

Kwakweli sijui tunaelekea wapi hii nchi, maana hadi naandika uzi huu nimetoka kuzunguka mji mzima wa Tabora manispaa kila kituo wanasema mafuta yamekwisha. Ikiwa mimi binafsi nimejikuta natumia garama ya karibu shilingi 12,000 kuzunguka kutafuta maguta na bodaboda mji mzima.

Leo nimeshindwa kuwapeleka wanangu shuleni.
Nimeshindwa kumpelekea mgonjwa chakula hospitali.
Nimeshindwa kumpeleka wife kazini.
Nimeshindwa kufuata maziwa ya kiziwanda.
Nimeshindwa kwenda kwenye michongo yangu down town.

Na sijui jioni nitarudije home nikisha piga mtungi, maana kwenda nitaenda polepole kwa miguu.

Jamani wenye mamlaka ebu mtusaidie kwa hili maana kama mimi nimepata shida hizo, je, vipi wananchi wenzangu kwao imekuaje?
 
Ukiona hivyo ujiandae kusikia Ewura wametangaza bei mpya leo mafuta yanapanda kesho fuel station hizo hizo kesho utashangaa mafuta wanayo na utauziwa mafuta kwa bei ya juu ni mwendo wa super profit, kwa Dar wenye tabia hiyo sana ni Total.

Ningekuwa na mamlaka ningelitumia Jeshi kukomesha tabia hii nchi nzima, unaanzisha msako wa filling station zote ambazo wanasema hawana mafuta wanasachi visima vyote atakayekutwa amefungia mafuta anafutiwa Leseni hapohapo na mmiliki anawekwa ndani kwa uhujumu uchumi, ukiwafanyia demo watu kadhaa tu hii tabia ingekoma.
 
Tabora ni pa hovyo sana. Nilipata kufanya project moja kwa miezi miwili, ila niliona kama nimekaa mwaka.

Turudi kwenye mada;
Poleni sana. Hii janja janja ya Wafanyabiashara ikomeshwe.

Vumilieni, mpaka kesho jioni mafuta bwerere.
Hadi muda huu hakuna mafuta mji mzima
 
Mkurugenzi EWURA anamhujumu rais Dkt Samia. Afukuzwe haraka sana. Kinachotokea kuna watu ndani ya EWURA wanatoa taarifa. Ninashauri ili abaki na cheo chake safari hii ashushe bei ili kuwakomoa wanaofungia mafuta.
 

Hizi harakati aliziweza jpm,huyu wa sasa na genge lake la wahuni huwezi sikia hilo.
 
Kwamba wahuni wameficha [emoji849][emoji848]
100% wameficha mkuu.
Maana haiwezekani vituo vyote viseme vimeishiwa kwa siku moja na utofauti ni kidogo sana.
Wafanya biashara wamefucha mafuta mkuu.
 
Acha ngonjera wewe , unakaa tabora ipi ambayo hakuna maji
Hakuna maji ndio yametoka jana kwa masaa tu baada ya kukaa zaidi ya week nzima. Hata Leo hakuna maji.... Kote kidatu,Ipuli yoteee. Maji yanatoka maeneo ya ofisi za mkoani na pale brigedi
 
Wamegoma kuuza mafuta kisa mtetezi wao Makamba kaondolewa kwenye wizara nyeti ya nishati.
 
Nye CCM, wanyamwezi wamewakosea nini? mbona ni watiifu kuwapa ushindi wa kishindo japo hamuwajali baada ya matokeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…