Niendee moja kwa moja kwenye mada husika!
Mkoa wa Tabora hivi sasa ninapoandika uzi huu, uko kwenye taharuki kubwa ya kukosa mafuta!
Hali ni mbaya hapa mjini, petro station moja tu mji mzima inatoa huduma ya mafuta!
Hakuna kiongozi yoyote wa chama (CCM) au serikali ambaye ametoa ufafanuzi wowote!
Mkoa huu wa kishu'shu'shu na KI'CCM hali ni tete..! Mkoa umebaki mtupu hakuna mtetezi!
Nikumbushe kuwa jumatano ijayo ya mwanzo wa mwezi kwa fununu zilizopo EWURA wanatangaza bei mpya za mafuta, kitu ambacho kinatarajiwa, ni mafuta kupaa zaidi bei.
Nikumbushe pia mwezi mmoja uliopita ilitokea taharuki kama hii ya sasa, na kuonekana baadhi ya wafanyabiashara wakificha mafuta na baada ya wiki moja na nusu mafuta yakapaa kwa bei ambayo haijawahi kushuhudiwa kwa kizazi hiki cha miaka 30 iliyopita!
SHIDA YA MAJI
Maji pia yamekuwa shida, zaidi ya wiki sasa maji hayapatikani...!
Hali ni mbaya tumefika pabaya!!