DOKEZO Tabora Mjini hali tete, mafuta hakuna! Maji hakuna

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yale maji ya kutoka ziwa Victoria yameyeyuka.
 
Wameficha wanasubiri bei chaajabu mkoa una viongozi wote mpaka maaafisa wa usalama wamekaa hapo na wanalipwa mishahara na serikali.
 
Jumanne ya kwanza ya kila mwezi ni tangazo la bei mpya za mafuta! Wameyaficha wakisubiri Jumanne ijayo yapande. Hizo ni indicators we are shitholes! Nchi ya kipumbavu kabisa.
Wanasubiri jumatano bei mpya
 
Kwasasa Tabora kuna shida ya maji, na yanatoka kwa mgao walau masaa matatu kila siku.
Hata umeme pia ni patashika kwasasa umekua wa mgao.
Nilikua tabora siku mbili zimepita hakuna shida ya maji, suala la umeme ni la kitaifa

Nilikua maeneo ya national
 
Hakuna maji ndio yametoka jana kwa masaa tu baada ya kukaa zaidi ya week nzima. Hata Leo hakuna maji.... Kote kidatu,Ipuli yoteee. Maji yanatoka maeneo ya ofisi za mkoani na pale brigedi
Nilikua national maji yapo ya uhakika
 
Hili la mafuta Dr. Biteko atoe maelekezo haraka sana hali ni mbaya.
 
Naweza nikaelewa ukosefu wa mafuta lakini maji kwanini yawe changamoto wakati yanatoka hapo hapo na watu wapo tayari kuyalipia bei yeyote wayapate? nimekaa sana nchi za nje na niliwahi kufanya kazi kwenye city utilities divison, maji yalikuwa safi hata kwa kunywa moja kwa moja kutoka bombani na sikuwahi kuona maji yakatike hata siku moja, na walikuwa hawana hata mto, maji yao yalikuwa ya underground (aquifer) na budget yao haikuwa kubwa sana na walikuwa wanapata faida na bill za maji ilikuwa ni karibu na bure, kuna kitu cha ovyo tunafanya ndio maana hatuna maji, hizi halmashauri inabidi zitafute solution za uhakika sio visingizio kila siku, watu wanalipa kodi na bill za maji pia, ujinga uishe
 
Kizimkazi Hana muda na haya kabisa. YY ni kuteua na kutengua tu.Anacho weza
 
Mbunge ana uwezo gani kwenye umeme na maji?
Mbunge kama ni mfuatiliaji mzuri na marafiki kule juu anaweza kufanya lobbying serikalini ili wilaya yake ipate pesa za mradi, kuna fund nyingi sana za maji zinaishia kwa wajanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…