TABORA: Watu 9 wakamatwa kwa tuhuma za mauaji na kuuza viungo vya binadamu, damu ya mtu inauzwa Tsh 600,000

TABORA: Watu 9 wakamatwa kwa tuhuma za mauaji na kuuza viungo vya binadamu, damu ya mtu inauzwa Tsh 600,000

Waganga afrika ndio chanzo cha matatizo yote, thus Ulaya waliwaua wote wakapata Jamii isiyoamini ushirikina kuishi.
Waganga ndio chanzo cha ujambazi, vibaka, makahaba, utengano wa familia, mivurugano yote kwenye Jamii. Hawa watu ni haramu nashangaa anaesapoti uchief zama hizi. Huwezi kupewa uchief kama ujaua sana.
 
... hivi Ulaya na Marekani kuna waganga wa kienyeji hasa wapiga ramli? Ifike mahali itungwe sheria kupiga ramli iwe kosa la jinai! Mpiga ramli/mganga kifungo kisichopungua miaka 10 jela; mpigiwa ramli jela miaka 2.
Ni ngumu kutunga sheria endapo watunga sheria kwa sehemu kubwa ni wateja wa ramli!!
 
... hivi Ulaya na Marekani kuna waganga wa kienyeji hasa wapiga ramli? Ifike mahali itungwe sheria kupiga ramli iwe kosa la jinai! Mpiga ramli/mganga kifungo kisichopungua miaka 10 jela; mpigiwa ramli jela miaka 2.
Nani atunge sheria? Watunge wakati wao ndiyo wateja wao wakubwa ?
 
Lindi hakuna mauaji? Au hakuna waganga?
Waganga wapo ila hawana mambo ya hovyo kiasi hiki.
Imagine umuue mtu kisha damu yake uuze chupa sh.laki sita tu.
Huyo anayeuza laki sita kanunua kwa wauaji ambao sijui walimuuzia sh.laki 3
 
Kuna best yangu alifungua mgahawa, daaaahhh, waliroga mpaka akafulia.
Siku nyingine moto hauwaki mpaka jirani amalize kuhudumia chai ya asubuhi kwa wateja.
Siku nyingine supu aliyopika alfajiri asubuhi anakuta funza ishaharibika
Wasukuma na kanda hizo wanaamini sana mambo hayo.
 
Waganga wapo ila hawana mambo ya hovyo kiasi hiki.
Imagine umuue mtu kisha damu yake uuze chupa sh.laki sita tu.
Huyo anayeuza laki sita kanunua kwa wauaji ambao sijui walimuuzia sh.laki 3
Sidhani kama unajua unachoongea,
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limekamata mtandao wa watu 9 ambao wametajwa kuhusika na tuhuma za mauaji pamoja na kuendesha biashara ya mauziano ya viungo mbalimbali vya sehemu ya mwili wa binadamu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, ACP. RICHARD ABWAO amesema mtandao huo umekamatwa ikiwa ni siku chache tu baada ya kutokea mauaji ya kinyama ya binti mmoja huko wilayani Sikonge Mkoani Tabora.

Amesema kufuatia tukio la mauaji hayo watu watatu walikamatwa baada ya kutiliwa mashaka ambapo walimtaja mganga wa kienyeji ambaye amekuwa akinunua viungo vya mwili ikiwemo sehemu za siri za jinsia zote pamoja na matiti.

Aidha, mganga huyo ambaye hakutajwa jina lake kutokana na sababu za kiuchunguzi alikiri kuhusika na tuhuma hizo huku naye akimtaja mtu ambaye amekuwa akimuuzia viungo hivyo vya mwili ambaye pia alihojiwa na kukubali kufanya hivyo pamoja na kutekeleza matukio mengine ya mauaji ya kinyama yaliyo ambatana na kukinga damu katika chupa ambayo amekuwa akiiuza kwa kiasi cha shilingi laki 6.
Ushirikina na laana zake. Na unakuta watu wazima wanajisifia sababu ya kushiriki au kufanya mambo ya kishirikina. Toka lini uchawi unamsaidia mtu?
 
Back
Top Bottom