TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

Status
Not open for further replies.
Kitakachofuatia ni serikali kuomba mkopo wa dharura WHO kushirikiana na World Bank ili kuokoa maisha ya waathirika.
Hao waliokula fedha za Covid ndio waokoe Maisha, au hao waliouza dawa za aids zilizo expire ndio leo wawe na uchungu wa Maisha ya wa Tz?
 
Kashalijua hilo siku nyingi. Ameruhusu wale wa tiba za majani. Mbona tunazo nzuri tuu kuliko hizo ARV?
 
Jibu ni moja tu hizi dawa hazitibu ukimwi. Zinarefusha maisha. Kama zinarefusha maisha, tujiulize sisi waathirika hatuna nyege?. Kama tunanyege tunazimaliza vipi?, Je kwa kupiga nyeto au kwa kushiriki tendo?.

Tuache ujinga, narudia tena tuache ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah kama nilitamni hivi mkuu uendelee kufunguka , huwa najiuliza hivi ni kwanini ziwepo za kurefusha maisha lakini si kutibu kabisa au kuondoa tatizo.
 
Raisi mstaafu wa Afrika kusini aliwahi Sema Ukimwi unasababishwa na umasikini tuu.Kula vizuri ,ukimwi unapotea
 

Moshi. Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.

Taarifa hiyo imetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa Tacaids, Leonard Maboko kwenye ufunguzi wa wiki ya Ukimwi duniani uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mandela vilivyopo Kata ya Pasua, Moshi mjini.

Hata hivyo, alisema mfuko ulioanzishwa na tume hiyo (AIDS Trust Fund) ulioanzishwa mwaka 2015 utasaidia kuziba pengo litakalokuwepo kwa miaka miwili.

“Wafadhili wameendelea kupungua nchini lakini huu mfuko wa ndani utasaidia kupunguza haya mapengo,” alisema Maboko.

Sasa hivi, alisema wafadhili wanatoa dawa za ARV lakini dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi wamejitoa.

Alisema mfuko huo utawasaidia Watanzania wanaohitaji dawa zilizokuwa zinatolewa na wafadhili waliojitoa.

Kwa upande wake, mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema takwimu zinaonyesha maambukizo ya Ukimwi yamepungua mkoani humo kutoka asilimia 7.2 mwaka 2004 mpaka asilimia 2.6 mwaka 2018.

Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua hali za afya zao na kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

Kilele cha siku ya Ukimwi duniani ni Desemba mosi.

Chanzo: Mwananchi
Kama ni kweli basi kifuatacho ni Gesti kulalwa na wageni tu,Rate ya ndoa kupungua maana wengi watakuwa wanaogopa kupima VVU,Mzunguko wa pesa kupungua kwa sababu rate ya kuhonga na udangaji itapungua kwa kasi,Tz kuendelea kushikilia rekodi ya watu wasio na furaha kwa sababu ya kujiuliza swali "nitaishije".Ruksa kuweka nyongeza!.Hata hivyo neno langu siyo sheria.Yamkini yule aliyesema amebadilisha uwanja wa mapambano maybe ndo kama hivi.
 
Bora wajiondoe tu, ni wakati wa kupiga mitishamba na kutumia lishe bora asilia. Watu hawajui tu kuwa hayo madawa ni zaidi ya bomu/sumu.
 
Nina wasi wasi na hiyo takwimu.

Hadi sasa bado dawa za malaria tu ni changamoto,unawezaje kuzungumzia ARV ambazo si chini ya elfu 30 kwa dozi za mwezi mmoja kwa kila mgonjwa?

Hakuna mtu atapukutika,,bajeti ya haya madawa haifiki hata bilioni 50,,nchi haiwezi kosa bilioni 50 banah...[emoji134][emoji134]
 
Na kwa hesabu za haraka iwapo wastani wa bei ya dawa utakuwa elfu 30,000/= kwa mwezi,basi tutahitaji kwa wagonjwa waliopo wanaokadiriwa kufikia 1.7M kiasi cha pesa ifuatayo;

30,000 x 12 kwa mwaka x 1.7 = 612Billion

Bado hujanunua vipimo na reagent zake kufuatilia maendeleo ya mgonjwa au athari za dawa.
Wakati huo huo hujanunua dawa za magonjwa mengine.
 
Nina wasi wasi na hiyo takwimu.

Hadi sasa bado dawa za malaria tu ni changamoto,unawezaje kuzungumzia ARV ambazo si chini ya elfu 30 kwa dozi za mwezi mmoja kwa kila mgonjwa?
mkuu cio arv. hizo bado ztaendelea kuletwa. walizokata ni za magonjwa nyemelez
 
Kulikuwepo na tetesi kwamba Benjamin mkapa foundation watachukua nafas zitakazoachwa
 
ARV --- Antics to Reinforcing the Virus

Without these free ARVs, VVU cases would have been cut & reduced by a lot muda mrefu tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom