Angalau umeandika jambo inagwa badala ya kusema serikali izingatia ushauri kama upo, umepanga tena zitumike mbinu za kukabiliana nazo! Sasa kama ni makabiliano tunaazia Hapa Hapa tulipoishia Kwa namna ya taratibu Wala isiyotumia nguvu. Invisible powe ! Huyo jamaa uliyemnukuu ni mfuasi wala sio mwanaccm kwani haijui CCM hata kidogo anaijua Kwa kuona rangi zake )kuwa za kijani na propaganda kama za akina Mwashambwa!
Hoja zijibiwe Kwa hoja na serikali ifanye marekebisho! Hakuna tatizo katika Hilo!
Kingine ni k amba Kuna watu tayari walishatongozwa na DP 🌎 Kwa njia ya misaada ya kibinaadamu wasijue mwarabu alikua atakataliwa hivyo akaandaa kundi la kumtetea
View: https://youtu.be/D2POHltursg
Lakini Kwa taarifa na tetesi zilizopo aliwapa fedha nyingi sana watawala (rushwa) ili wamkubalie ndio mana unaona Mbarawa na PM walitofautiana ni namna Gani DP alipatikana kama mzabuni Kwa kukiuka sheria ya manunuzi.
Ushahidi mwingine ni wabunge wote Kwa pamoja kuwa na sauti Moja ya kuidalalia dP Kwa kuuliza maswali chokonozi kinafki katika vikao vya bunge, huku wajumbe wa Kamati ya miundo mbinu wakiwa na ukwasi wa kutosha ghafla mara baada ya ziara ya Dubai.
Waandishi na wasaini kupelekwa Dubai na baadae wao Kuja kuhubiri nchi nzima na kuwananga wanaokosoa mkataba huku wakila maisha ya Fahari na Anasali, Maulid na wenzie aibu!
Ulifuatilia mgogoro wa Djibouti na DP world ni mamlaka kuilalamikia DP Kwa vitendo vya Rushwa na mkataba unaotoshia amani na usalama wa nchi.
Ni kusikitisha zaidi Chama Cha Mapinduzi na viongozi wa serikali wameegemea kuielezea mafaida ya mkataba na kuacha kujibu hoja za msingi kabisa za kisheria na za kimkataba. Hii ni dalili kwamba Kuna mazingira ya Rushwa ambayo kurejesha fedha ni ngumu isipokua kuwakandamiza wanaokosoa ili mradi mwarabu apewe bandari kama mwekezaji binafsi (Dr mwambukusi et al)
Kuna provisions katika hiyo IGA inasema kuwa IGA ikishasainiwa haibadiliki tena na serikali Haina uwezo wa kufanya hivyo na ikifanya hivyo itashtakiwa na kutakiwa kulipa. Hii ni hofu kubwa Kwa watawala kwamba yunarudi kule kule kwenye MIGA ambapo sasa sehemu kubwa ya mapato yetu yanatumika kuservice deni linalotokana na uzembe huo huo!
Magufuli aliliomba bunge mwaka 2017 litunge Sheria za usimamizi wa Maliasili ya Taifa. Leo hii njama zimeshafanyika na bunge lnaenda kubadili Sheria hiyo ili kukidhi mahitaji ya mwarabu badala ya mkataba ubadilishwe kukidhi mahitaji ya Mtanzania.