Tafadhali CCM tusiwachukulie poa TEC. Kuwakabili hawa ni tofauti na CHADEMA

Tafadhali CCM tusiwachukulie poa TEC. Kuwakabili hawa ni tofauti na CHADEMA

Kwani kanisa Catholic la DRC lina muundo tofauti na hili la bongo kwenye kuwasiliana na waumini?

Martin Fayulu alikuwa mgombea wa kanisa uchaguzi uliopita na kampeni alipigiwa hadi kanisani na kanisa likawa hadi na kituo cha kujumlisha kura ila holaa,wakayakataa matokeo bado holaa.

NB: DRC ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya waumini wa kanisa Catholic Africa na top 10 duniani with 50M+.
 
Kwa dhati kabisa ninawasihi wanaCCM tusije tukafanya kosa la kuwafananisha TEC na CHADEMA. Nimeona uzi wa ndugu Sir John Roberts akidai wanaCCM tuachiwe TEC kukabiliana nao. Naheshimu mawazo yake kama mwanaCCM mwenzangu ila siungi mkono hoja yake kwa 100%. Sir John labda haijui kiundani TEC akadhani nao pia watajibiwa kirahisi kama tunavyowajibu chama cha Mbowe.

Kanisa katoliki kama ilivyo CCM nalo limeenda hadi ngazi ya shina.. na linaongoza kwa kuwa na waumini wengi zaidi hapa nchini na duniani kwa ujumla. Wanaposema waraka wao utasomwa kwenye jumuiya ina maana hadi wananchi wa vijiji vya ndani huko Buhigwe au Kalambo wataamshwa usingizini. CHADEMA wao mambo yao huishia tu mijini na Twitter kwahiyo damage yao ni ndogo kulinganisha na hiki wanachofanya TEC.

Kingine kinachoogopesha ni hii tabia ya wakatoliki kuwa wakimya. Mapadre na maaskofu ni wasomi ambao tangu shuleni walikuwa ni vipanga yaani hawabahatishi. Wao wakishasema lao huwa hawahagaiki sana kubishana kitu kinachotia hasira mno. Ingekuwa CHADEMA hadi muda huu ungekuta Lema au Heche kashajitokeza na kuropoka pumba. Sasa hao TEC toka Padre Kitime aongee sijasikia kiongozi mwingine yeyote akiongea. Ni watu hatari. Hata tukisema CCM tuishambulie TEC kwa maneno bado itakua sawa na kujishambulia wenyewe kwasababu kuna wanaCCM wengi ambao ni wakatoliki. Kutakuwa na upinzani wa ndani.

Ikumbukwe pia hawa TEC hadi kutamka tayari wana mawasiliano na kiongozi wao mkubwa yaani Papa. Kwa msiojua nguvu ya papa mkasome kisa cha Papa Gregory VI na King Henry IV ndo mtaelewa vizuri. Mfalme alikalishwa kwenye baridi siku 3 akisubiri kuonana na papa amwombe msamaha. Haikuwa poa. Katoliki pia limekuwa likihusishwa na siasa za nchi nyingi duniani. Kwenye story ya vita ya Biafra huko Nigeria hili kanisa lilitajwa kufadhili waasi.

Wito wangu ni kuwasihi wasomi na wataalamu wa diplomasia & siasa ndani ya chama na serikali kukaa chini na TEC ili kumalizana nao. Kama kuna mbinu nyingine ambazo sio za kidiplomasia lakini zinaweza kutuliza hali ya hewa nazo pia zitumike.
Mbinu rahisi ni kuwapa kesi ya uhaini tu. Wakikaa lupango miezi sita, wataomba poo wenyewe
 
TEC watumie busara zaidi maana hiki chama chakavu hakikawii kuwaita BAKWATA ili mgogoro wa kuligawa Taifa uanze.

Kuna kundi la UVCCM linawakusanya Mashehe huku TMK ni kusambaza sumu za Udini

Umoja wetu wa Kitaifa ni TUNU ya kujivunia.
Mashehe hawana madhara.
 
Tatizo la TEC wasipojibiwa nao huwa hawaongezi hoja ila wanachukulia kudharauliwa wanaenda next steps ambazo huwa ni siri utaona impact
 
wawakusanye kujibu hoja, wakija kivingine ndio itasaidia anguko la chama dola
CCM ni Kikundi cha Wapika majungu na Fitna au huwajui watatumia vuguvugu hili la Bandari ili kutuchonganisha na kutugawa sisi wananchi Zanzibar kuna watu hawasalimiani
 
Wewe huna msimamo na hauelewi usimamie nini na usimamie wapi. Hofu yako na uoga wako usitake kuwapa na kuwaambukiza wengine,. Wewe simama mwenyewe na uoga wako. Usikitishe chama wala serikali.serikali itaendelea kuongoza nchi kwa mujibu wa katiba nasiyo kwa mujibu wa nyaraka. Ukiwa mtu wa hofu na uoga lazima uwe na unafiki ndani yako na kutaka watu wote wawe wanafiki kama wewe.
Mpaka Hapa serikali imeshavunja katiba Hilo hulioni? Unashuka mavi yanakunukia unaanza kuuliza watu nani kajinyea?

Juzi umesimama na watawala Mjomba wako Mwambukusi anyongwe Kwa uhaini pamoja Na Dr Slaa na ukaandaa machapisho kushadadisha hoja yako.

Kwabahati mbaya tulipobonyeza na kuitangazia Dunia kwamba Tanzania Kuna uhaini tukisaidiana na niniyi na vyombo vya dola, mama Yako akaona ni aibu Kwa Taifa kuenda sanjari na watu kama ninyi! Mashtaka yakabadilika ghafla na yakawa ya uchochezi na fedha za umma zikatika kuwarudisha mjini!
Huoni ni kuvuliwa nguo?
 
Sisi CHADEMA tunataka mikataba yote ya ilioingiwa na Serikali ya CCM iwekwe wazi tuikadili na tunawaomba Watanzania wa Dini zote watuamini ili tuionoe CCM na majizi yake Madarakani
CHADEMA subirini hadi 2215
 
Kwani kanisa Catholic la DRC lina muundo tofauti na hili la bongo kwenye kuwasiliana na waumini?

Martin Fayulu alikuwa mgombea wa kanisa uchaguzi uliopita na kampeni alipigiwa hadi kanisani na kanisa likawa hadi na kituo cha kujumlisha kura ila holaa,wakayakataa matokeo bado holaa.

NB: DRC ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya waumini wa kanisa Catholic Africa na top 10 duniani with 50M+.
Mkuu unazungumzia siasa hapa tunazungumzia rasilimali za nchi
 
Una nukuu yoyote kwamba kardinali pengo alitangaza kutokumuunga mkono Niwemugizi?
Ukimya wa Kadinali Pengo kwenye sakata la Niwemugizi lilikuwa tosha wewe ni mtu mzima lazima uelewe
 
MamaSamia2025 leo umeongea ukweli wa moyo.. Uhalisia kabisa pengine bila kujua..
Umenikumbusha mchawi anapokata roho anavyoweweseka! [emoji23] ila wewe sio mchawi[emoji1544][emoji1550][emoji3]
Serikali ya CCM itawapangua TEC kisayansi hamtaamini. Wewe mkuu wa wachawi utashangaa Padri Kitime anafanya Press ya kusifu DP World.
 
Wewe huna msimamo na hauelewi usimamie nini na usimamie wapi. Hofu yako na uoga wako usitake kuwapa na kuwaambukiza wengine,. Wewe simama mwenyewe na uoga wako. Usikitishe chama wala serikali.serikali itaendelea kuongoza nchi kwa mujibu wa katiba nasiyo kwa mujibu wa nyaraka. Ukiwa mtu wa hofu na uoga lazima uwe na unafiki ndani yako na kutaka watu wote wawe wanafiki kama wewe.

Nitaendelea kusimama upande wa Rais samia , serikali ,chama na Taifa langu kwa kuwa huo ndio upande ambao muda wote na wakati wote ambao Rais samia amekuwa akipigania kuhakikisha kuwa Taifa hili linasonga mbele na kupiga hatua za kimaendeleo.

Watu aina yako wanaopenda kuambukiza hofu kwa watu wengine huwa ni wengi na hawakosekani katika jamii. Muoga hufa mara nyingi lakini jasiri hufa mara moja tuu.wewe ni muoga na hivyo lazima uwe mnafiki.
Mkuu umesahau kuandika namba yako ya simu kwenye hii comment. Pia umesahau kusema wewe ni kijana mzalendo unayeipenda nchi yako.
 

“2025 hakuna wa kuchukua fomu ya Urais ya kumpinga Samia Suluhu Hassan labda mambo yaharibike sana”- Dr Kikwete​

 
Back
Top Bottom