ivunya
JF-Expert Member
- Sep 18, 2015
- 2,290
- 2,220
Ndo maana unaposimama kwenye Maombi unatakiwa kuomba msamaha kwa Mungu, dhambi zote tulizofanya.Mungu anasemee DhambiTukisema tuombe tukiwa hatuna dhambi hapa tutajidanganya wenyewe kwa sababu Biblia inasema wote ni wadhambi.Hakuna anayeweza kusimama mbele za Mungu na kusema yeye hana dhambi.
Kitu tunachoweza kujivunia ni kuwa Yesu ametufanya tuhesabiwe kuwa ni wenye haki mbele za Mungu kupitia damu yake iliyomwagika msalabani.Kumwamini Kristo kunatupa uhalali wa kusogea karibu na Mungu tukiwa na ukaribu wa baba na mwana.Na hii ni hakika kuwa maombi yetu yanafika.
Tusiwatishe watu na mambo ya uwe hauna dhambi.Hakuna atakayesimama kuomba kama hicho kikiwa ndo kigezo cha maombi kumfikia Mungu.
1 Yoh 1:8 SUV
Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
Isaya 1: 18
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”
Mathayo 5: 23-24 - Kwa hiyo ikiwa unatoa dhabihu kwenye madhabahu ndani ya Hekalu na unakumbuka kwa ghafla kuwa mtu ana kitu dhidi yako, aacha dhabihu yako huko kwenye madhabahu. Nenda na ufanane na mtu huyo. Kisha kuja na kutoa sadaka yako kwa Mungu
Kwa nini Yesu anasema tuache sadaka kutoa kwa Mungu twenda tukapatana na mtu tuliyekosana naye?
Kwa nini huyu mtu asiendelee kutoa sadaka kwa Mungu wakati kuna dhambi kafanya. Je akiomba huyu mtu Mungu atajibu Maombi Yake?