Tafadhali usirudie tena kuwaombea wafu. It's a waste of time

Katika pita pita zangu mitandaoni, nimekutana na video zinazoonesha misa au ibada za kuwaombea Marehemu. Kama na wewe huwa unashiriki misa hizo, sikulaumu, nafikiri ni kwa kutokujua kwako ukweli huu:

Kuwaombea watu waliofariki ili Mungu awalaze mahali pema, ni kupoteza muda. Mtu akifa, sekunde hiyohiyo ama anaenda peponi kwenye raha au kuzimu kwenye mateso yasiyokoma. Mtu ambaye tayari yuko kuzimu kwenye mateso, hawezi kutolewa huko na kuingizwa peponi kwa sala zetu, hata tukimuombea kwa kulia sana na kuomboleza na kugaragara chini. Maandiko yanasema wazi kabisa baada ya kifo ni hukumu (Waebrania 9:27).

Kwa habari zaidi kuhusu hoja hii, soma kisa cha tajiri na Lazaro katika Luka 16:19-31 utaona wazi kwamba walioko kuzimu hawawezi kuhamia peponi and vice versa.

Kama kweli unampenda mtu, muombee sasa, akiwa bado hai. Ukiona anaishi maisha ya dhambi, muombee Mungu amsamehe, apate wokovu na aishi maisha yanayompendeza Mungu. Usisubiri azikwe ndio uanze kumlilia Mungu amuweke mahali pema. Utakuwa unapoteza muda wako bure.

Kuliko utenge muda wako kuwaombea wafu, heri ushike jembe ukalime!
Wakatoliki ndo wenye ibada za namna hiyo kumbe ni kupoteza muda kwa mujibu wa bible basi ni heri kushika majembe wakalime kuliko kupoteza muda
 
Acha UONGO.
Uombezi Kwa wafu inaruhusiwa na MUNGU anawapunguzia adhabu zao.
Ndo maana waislam uwa tunarehemu na kugombea Dua marehemu zetu na inaruhusiwa.
Ndo maana katika amali njema unazotakiwa kuacha ni sadaka inayoendelea na mtoto mwema anayekuombea Dua baada ya kufariki
Kama unaongea ukweli, basi badilisha hilo jina lako mjingamimi
 
Katika pita pita zangu mitandaoni, nimekutana na video zinazoonesha misa au ibada za kuwaombea Marehemu. Kama na wewe huwa unashiriki misa hizo, sikulaumu, nafikiri ni kwa kutokujua kwako ukweli huu:

Kuwaombea watu waliofariki ili Mungu awalaze mahali pema, ni kupoteza muda. Mtu akifa, sekunde hiyohiyo ama anaenda peponi kwenye raha au kuzimu kwenye mateso yasiyokoma. Mtu ambaye tayari yuko kuzimu kwenye mateso, hawezi kutolewa huko na kuingizwa peponi kwa sala zetu, hata tukimuombea kwa kulia sana na kuomboleza na kugaragara chini. Maandiko yanasema wazi kabisa baada ya kifo ni hukumu (Waebrania 9:27).

Kwa habari zaidi kuhusu hoja hii, soma kisa cha tajiri na Lazaro katika Luka 16:19-31 utaona wazi kwamba walioko kuzimu hawawezi kuhamia peponi and vice versa.

Kama kweli unampenda mtu, muombee sasa, akiwa bado hai. Ukiona anaishi maisha ya dhambi, muombee Mungu amsamehe, apate wokovu na aishi maisha yanayompendeza Mungu. Usisubiri azikwe ndio uanze kumlilia Mungu amuweke mahali pema. Utakuwa unapoteza muda wako bure.

Kuliko utenge muda wako kuwaombea wafu, heri ushike jembe ukalime!
Umenena vyema.

Ila hiyo ya Luka 16 kilikuwa kisa tu kikionesha namna gani ukishakufa hukumu Yako inaamdikwa. Na haiwezi badilishwa.

Ukweli ni kwamba, ukifa unarudi mavumbini na sio kuzimu Wala peponi. Roho Yako inamridia MUNGU Hadi ule mwisho utakapo fika wafu watafufiliwa
 
Piganeni hadi muuane sisi tutawasaidia kuwahifadhi kaburini
 
Sasa mpendwa wangu, tangu uanze kuwaombea wafu wanaokuhusu, Mungu ameishakujibu kwamba ameishawahamishia eneo jingine?
Still haikuhusu vyema ku-stick na unachoamini wewe!

Kwanini usiulize nilipoomba afya njema alinipa au hakunipa?vyote tunaomba kwa imani that's why anayeomba sana anaumwa asiyehangaika kusali mzima kama kisiki usijikute mkamilifu!
 
Janja unawaonea wivu hadi wafu
Nani huyo, mimi? Kwangu mimi wivu ni dhambi. Na dhambi hazina nafasi moyoni mwangu.
"Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya... uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda... watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu (Galatia 5:19-21)
 
Katika pita pita zangu mitandaoni, nimekutana na video zinazoonesha misa au ibada za kuwaombea Marehemu. Kama na wewe huwa unashiriki misa hizo, sikulaumu, nafikiri ni kwa kutokujua kwako ukweli huu:

Kuwaombea watu waliofariki ili Mungu awalaze mahali pema, ni kupoteza muda. Mtu akifa, sekunde hiyohiyo ama anaenda peponi kwenye raha au kuzimu kwenye mateso yasiyokoma. Mtu ambaye tayari yuko kuzimu kwenye mateso, hawezi kutolewa huko na kuingizwa peponi kwa sala zetu, hata tukimuombea kwa kulia sana na kuomboleza na kugaragara chini. Maandiko yanasema wazi kabisa baada ya kifo ni hukumu (Waebrania 9:27).

Kwa habari zaidi kuhusu hoja hii, soma kisa cha tajiri na Lazaro katika Luka 16:19-31 utaona wazi kwamba walioko kuzimu hawawezi kuhamia peponi and vice versa.

Kama kweli unampenda mtu, muombee sasa, akiwa bado hai. Ukiona anaishi maisha ya dhambi, muombee Mungu amsamehe, apate wokovu na aishi maisha yanayompendeza Mungu. Usisubiri azikwe ndio uanze kumlilia Mungu amuweke mahali pema. Utakuwa unapoteza muda wako bure.

Kuliko utenge muda wako kuwaombea wafu, heri ushike jembe ukalime!
Watu mliowaua 29.10.2025 sio wafu, ni watakatifu, kamwe hatutaacha kuwaombea, labda huyo mwanamke mmuuaji awaamuru mje mtuue na sisi ndipo ibada zatakapokoma
 
Duh, umeingiza mambo yasiyohusiana na mada.
 
Still haikuhusu vyema ku-stick na unachoamini wewe!

Kwanini usiulize nilipoomba afya njema alinipa au hakunipa?vyote tunaomba kwa imani that's why anayeomba sana anaumwa asiyehangaika kusali mzima kama kisiki usijikute mkamilifu!
No, inanihusu kwa sababu wewe ni binadamu mwenzangu. Kwanini nikuone unapoteza muda halafu nikuache tu bila kukushauri.
 
Kama ni hivyo basi na nyinyi muache mara moja kutupigia makelele ya kufukuza mapepo.
Ndugu yangu, Yesu mwenyewe ndiye aliyetuamuru tuyafukuze mapepo.
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo..." (Marko 16:17)
Mapepo sio mazuri. Yanaonea watu, yanatesa watu, yanasababisha magonjwa yasiyoeleweka, nk
Kwahiyo tunapoyafukuza, furahi kwa sababu ni njia ya kuwafanya watu wawe huru.
 
Kwahiyo kuwaombea wafu ni kupoteza muda, vipi muda tunaotumia kwenye uzinzi, Ulevi, masengenyo n.k?

Tuwaache watu wajipe faraja kwa kuwakumbuka marehemu zao

Ndiyo njia pekee ya kuwakumbuka wapendwa wao
Rafiki, kama unatumia muda wako kwenye uzinzi na ulevi, hiyo ni zaidi ya kupoteza muda; ni kujipeleka mwenyewe jehanam kwenye moto wa milele.
1 Kor 6:9-10
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.
 
Nimetoa observation yangu kwenye kupoteza muda rafiki
 
Waliotuambia tufanye hivyo ni hao hao walotuletea hicho kitabu ulichotumia kutudanganya hapa, ushawahi jiuliza kama sio wao hiyo biblia ungekuwa nayo leo? so unajiona wewe ndio unaijua kuliko wao waliotuletea? wafu lazima waombewe penda usipende, tutawaombea TU hakuna namna
Walikuambia kwa kunukuu vifungu gani. Vitaje hapa
 
No, inanihusu kwa sababu wewe ni binadamu mwenzangu. Kwanini nikuone unapoteza muda halafu nikuache tu bila kukushauri.
Wewe ukiwa unatenda dhambi zako mbona hauniiti nije nikushauri ikiwa umeona umuhimu wa kunishauri mimi niache dhambi ya kuombea wafu wangu?

Au msabato wewe mwenzetu ndiyo umeshamaliza dhambi tena hautendi!
 
Back
Top Bottom