Tafadhali usirudie tena kuwaombea wafu. It's a waste of time

Tafadhali usirudie tena kuwaombea wafu. It's a waste of time

Subiri kwanza uwe mfu ndio uje na hizi ngonjera zako
Kila amwaminiye Yesu ajapokufa anakuwa hai. Hivyo nikifa, usihangaike kuniombea.
Yohana 11:25
Yesu akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi."
 
Katika pita pita zangu mitandaoni, nimekutana na video zinazoonesha misa au ibada za kuwaombea Marehemu. Kama na wewe huwa unashiriki misa hizo, sikulaumu, nafikiri ni kwa kutokujua kwako ukweli huu:

Kuwaombea watu waliofariki ili Mungu awalaze mahali pema, ni kupoteza muda. Mtu akifa, sekunde hiyohiyo ama anaenda peponi kwenye raha au kuzimu kwenye mateso yasiyokoma. Mtu ambaye tayari yuko kuzimu kwenye mateso, hawezi kutolewa huko na kuingizwa peponi kwa sala zetu, hata tukimuombea kwa kulia sana na kuomboleza na kugaragara chini. Maandiko yanasema wazi kabisa baada ya kifo ni hukumu (Waebrania 9:27).

Kwa habari zaidi kuhusu hoja hii, soma kisa cha tajiri na Lazaro katika Luka 16:19-31 utaona wazi kwamba walioko kuzimu hawawezi kuhamia peponi and vice versa.

Kama kweli unampenda mtu, muombee sasa, akiwa bado hai. Ukiona anaishi maisha ya dhambi, muombee Mungu amsamehe, apate wokovu na aishi maisha yanayompendeza Mungu. Usisubiri azikwe ndio uanze kumlilia Mungu amuweke mahali pema. Utakuwa unapoteza muda wako bure.

Kuliko utenge muda wako kuwaombea wafu, heri ushike jembe ukalime!
Kuna hekima na kuna kinyesi cha hekima ... mleta uzi kama lengo lako ni la kuelimisha basi wewe ni kinyesi cha hekima ...maana muda ulioleta hii mada siyo sahihi kwa sababu unaonekana lengo lako ni kuunga mkono mauaji ya Oct 29 ...swali la logic kwa nini hii hoja unaileta siku za maombolezo ya mauaji ya Oct 29 ...viongozi wa kidini wamekuwa wakitumika kuombea wafu hata kwenye matukio ya kitaifa mfano ni ajali ya MV BUKOBA NA VIFO VYA MARAIS NK
 
Wewe ukiwa unatenda dhambi zako mbona hauniiti nije nikushauri ikiwa umeona umuhimu wa kunishauri mimi niache dhambi ya kuombea wafu wangu?

Au msabato wewe mwenzetu ndiyo umeshamaliza dhambi tena hautendi!
Rafiki, mimi niliishatubu dhambi. Nimeokoka. Nimezaliwa upya.
1 Yohana 3:9
Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.
 
Kuna hekina na kuna kinyesi cha hekima ... mleta uzi kama lengo lako ni la kuelimisha basi wewe ni kinyesi chahekima ...maana muda ulioleta hii mada siyo sahihi kwa sababu unaonekana lengo lako ni kuunga mkono mauaji ya Oct 29 ...swali la logic kwa nini hii hoja unaileta siku za maombolezo ya mauaji ya Oct 29 ...viongozi wa kidini wamekuwa wakitumika kuombea wafu hata kwenye matukio ya kitaifa mfano ni ajali ya MV BUKOBA NA VIFO VYA MARAIS NK
Umeingia moyoni mwangu ukaona lengo langu ndio hilo?
Yesu ameniagiza kuhubiri Injili wakati wowote. Iwe kuna msiba au arusi. Any time is a good time to share the gospel.
2 Timotheo 4:1-2
"Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu watu walio hai na wafu, na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme: Hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wa kufaa au wakati usiofaa), karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivu wote."
 
Huyo yesu asiyejua hata maana ya maneno yake mwenyewe ni yesu wa jalapeño...Yesu hajui hata 666ni nini?
 
Ukifa ndo imeisha hiyo. Uombe usiomba hakuna kinacho badilika
 
Kuna wimbo aliimba Apostle Kyande unasema “wachungaji”🎶

Weka pema peponi, weka pema peponi🎼
 
kuanzia tarehe moja mwezi WA kumi na moja Kila mwaka ni mwezi wa kuwaombea na ni mwezi wao marehemu.
unaalikwa muamini wowote kutumia nafasi yako ukiwa hapa duniani kuwaombea walioko toharani,
Raha ya milele uwape eeh bwana na mwanga wa milele uwaangazie.
Marehemu wote wa starehe kwa amani.Amina🙏
 
Huyo yesu asiyejua hata maana ya maneno yake mwenyewe ni yesu wa jalapeño...Yesu hajui hata 666ni nini?
Tubu hizo dhihaka zako mapema. Vinginevyo utalia na kusaga meno siku ya kuja kwa Yesu
Ufunuo 1:7-8
“Tazama! Anakuja na mawingu,” na “kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma”; na makabila yote duniani “yataomboleza kwa sababu yake.” Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen. “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
 
Ukaachana na hao waebrania wanavyosema kuhusu kuwaombea wafu, katika ukoo wenu babu wanasemaje kuhusu kuwaombea wafu
 
kuanzia tarehe moja mwezi WA kumi na moja Kila mwaka ni mwezi wa kuwaombea na ni mwezi wao marehemu.
unaalikwa muamini wowote kutumia nafasi yako ukiwa hapa duniani kuwaombea walioko toharani,
Raha ya milele uwape eeh bwana na mwanga wa milele uwaangazie.
Marehemu wote wa starehe kwa amani.Amina🙏
Pole sana MgosiMnubi. Maandiko niliyoyanukuu bado tu hujayaelewa?!
 
Ukaachana na hao waebrania wanavyosema kuhusu kuwaombea wafu, katika ukoo wenu babu wanasemaje kuhusu kuwaombea wafu
Acha stori za mababu, utapotea. Maandiko niliyokutajia sio ya Waebrania. Ni Maandiko ya Mungu mwenyewe.
2 Timotheo 3:16
Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha ya adili
 
Tubu hizo dhihaka zako mapema. Vinginevyo utalia na kusaga meno siku ya kuja kwa Yesu
Ufunuo 1:7-8
“Tazama! Anakuja na mawingu,” na “kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma”; na makabila yote duniani “yataomboleza kwa sababu yake.” Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen. “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
Wapuuzi mnamsingizea sana Yesu ....na hizo injili zenu feki
 
kasome tena ayo maandiko na utafakari pia, happy sabath mkuu
Yesu aliivunja Sabato, wewe bado tu unaisherehekea?!
 
Wapuuzi mnamsingizea sana Yesu ....na hizo injili zenu feki
Injili ninayohubiri sio feki. Ushahidi huu hapa
 
Yesu aliivunja Sabato, wewe bado tu unaisherehekea?!
marko2 :27-28 happy sabath dada
 
Hakika!!! Kila mtu atalipwa kwa kadri ya matendo yake... Kama ni mema au mabaya.
Ufunuo 22:10-12
Tena akaniambia, “Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia. Kwa sasa anayetenda mabaya na aendelee kutenda mabaya, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu. Mwenye kutenda mema na azidi kutenda mema, na aliye mtakatifu na azidi kuwa mtakatifu.” “Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na ujira nitakaomlipa kila mmoja kulingana na matendo yake.
 
Back
Top Bottom