Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
- Thread starter
- #81
Rafiki, kwanza hongera sana kwa kuandika comment yako kisomi. Hiyo seminari yako naona ina walimu wazuri wa communication. Wape maua yao.Samahani Kiongozi naomba nitoee kidogo maoni kuhusu mada yako ni kweli logic ya mawazo yako yanapaswa yapewe heshima sababu ni mawazo binafsi na mtazamo wako haujawa mbaya at all but ukiichunguza biblia vizuri kwa kusoma unaona kitabu cha wamakabayo ambacho kinatumika katika Catholic side na Orthodoxy ambacho ni vya Deutekeranoni lakini kuna mtu awali alisema kitabu hicho hakikuvuviwa na Roho Mtakatifu basi tuangalie kitabu cha timotheo
Bwana na amjalie Onesiforo rehema kuiona siku ile; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuionea haya minyororo yangu... Bwana na amjalie kuona rehema kwa Bwana siku ile." — 2 Timotheo 1:16, 18
(Hapa Paulo anaombea rehema kwa ajili ya Onesiforo, na mapokeo ya Kikristo ya kale yanaonyesha Onesiforo alikuwa ameshafariki wakati huo).
Hoja yako naiheshimu na iko logical but nahisi imebase zaidi kwenye protestant sides ambavyo ni views zao kwa wingi kwenye Self salvation na Sola Scriptura lakini kwa Kanisa kama Catholic Sisi Tunafundishwa Intercessions kwamba unaweza mwombea mtu as A friend na Mungu akafanya kitu kwa ajili yake kutokana na Sala zako mfano Mama zetu wanapotuombea makazini tupate riziki Mungu anaweza tupatia kutokana na ile sala ya Mama yako(ni mfano tu) hivyo kwa imani yako if it is okay kuto pray kwa ajili ya Marehemu its okay ila in Us kama Catholic side tunafundishwa kuna Purgatory(toharani)hivyo ni vyema zaidi kuwaombea waliopo huko waende mbinguni…Though ukiangalia hata kwenye Islamic side kwenye Holy Qur’an inasemwa hivyo nikitoa ushahidi kutoka kwenye kitabu Hicho Kitukufu
Surat Al-Hashr (59:10):
"Na wale waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotangulia kutupokea katika imani, wala usiweke roho zetu chuki yote kwa wale walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mwenye huruma, Mwenye kurehemu."
Hapa, dua ya kuombea waliotangulia (wafu) inatajwa moja kwa moja kama sifa njema ya waumini wa kweli.
Although naweza pokea Critics but nawasilisha hii sio kupinga hoja yako bali kuonesha ukweli unaotakiwa kuonekana wazi na yes i am a seminarian hivyo teaching faith ni moja ya jukumu langu
Asante.
Haya, turudi kwenye mada. Andiko ulilonukuu la 2 Timotheo 1:16, 18 halisemi kwamba Onesiforo alikuwa amekufa. Na wewe mwenyewe umekiri kwamba mapokeo ya Kikristo ya kale ndiyo yanayoonesha kwamba Onesiforo alikuwa ameshafariki wakati huo. Sasa tumfuate Kristo au tufuate mapokeo? Hatupaswi kufuata mapokeo. Angalia hapa jinsi Paulo anavyoonya kuhusu mapokeo:
Wakolosai 2:8
Angalieni, basi, mtu asiwapotoshe kwa udanganyifu mtupu wa hekima ya kibinadamu, ambayo chanzo chake ni mafundisho ya mapokeo ya watu... na wala si Kristo mwenyewe!
Sasa tukimfuata Yesu Kristo, tutazingatia sana yale aliyoyasema kuhusu Tajiri na Lazaro (Luka 16:19-31).
Angalia mstari wa 26, Ibrahimu anamwambia yule tajiri aliyekuwa kwenye mateso:
"Na zaidi ya hayo yote, kati yetu sisi na ninyi kuna bonde kubwa, ili wale wanaotaka kutoka huku kwenda kwenu wasiweze, wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu."
Mstari huu unaonesha kuwa mara baada ya kifo, hatima ya mtu aliye peponi na aliye kuzimu inakuwa imefungwa kabisa. Hakuna "daraja" au nafasi ya kuhama kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Kwa msingi huo, maombi ya walio hai hayawezi kumvusha mtu kutoka upande wa mateso kwenda upande wa faraja.
Kumbuka tena, maombi ya tajiri hayakujibiwa. Tajiri akiwa kuzimu aliomba msaada mara mbili: kwanza aletewe tone la maji (mstari wa 24) na pili akaomba Lazaro atumwe duniani kuwaonya ndugu zake (mstari wa 27). Maombi yake yote mawili yalikataliwa. Kwa mantiki hiyo kwakuwa maombi yanayofanywa na watu waliopo kuzimu hayajibiwi, basi ni dhahiri hata walio hai wakiwaombea wafu, maombi yao hayajibiwi.
Wakati tajiri alipoomba ndugu zake walioko duniani wasaidiwe ili wasiende kule matesoni, Ibrahimu alimjibu: "Wanao Musa na manabii; na wawasikie hao" (mstari wa 29). Jibu hilo linasisitiza kuwa fursa pekee ya mtu kubadili hatima yake ipo duniani wakati akiwa hai kwa kutii Neno la Mungu (Musa na manabii). Mtu akishakufa, fursa hiyo inatoweka kabisa, hivyo hakuna msaada wowote wa kidini (iwe sala au sadaka) unaoweza kufanywa na ndugu waliopo duniani utakaobadili hatima yake.