Tafakuri ya FaizaFoxy 9: Ushauri kwa Rais Samia, Dr. Hussein Mwinyi na Watanzania wote kuhusu Uchumi wa Bandari wenye tija

Kukusoma wewe huwa ngumu kidogo, hata wakati unapotulizana hivi.

Hapana.
Wazo lako binafsi sikubaliani nalo hadi hapo Muungano utakapokuwa umerekebishwa na kutufanya sote tuwe nchi moja.

Kwa hali ilivyo sasa, Tanganyika kwenda kuitegemea Zanzibar yenye madaraka kamili, huku waTanganyika wakiwa ni wageni wanapoingia nchi ile, hilo litakuwa wazo la kijinga kabisa (samahani kwa lugha hii, lakini huo ndio ukweli wenyewe..

Hata hivyo, ninakubaliana na wazo lako la kuwa na Bandari kubwa kabisa mwambao wa Tanganyika, na siyo lazima iwe Bagamoyo au Dar es Salaam. Tanga ni sehemu nzuri sana ya kuwa na Bandari kama hiyo, kwa sababu hapo hata Uganda tutakuwa tumemuingiza kwenye himaya yetu, na DRC ndiyo itakuwa tumemshika sehemu zote, juu na chini.

Ukiwa umetulizana namna hii, inapendeza kidogo kukusoma.
Kwa mara ya kwanza kabisa, acha nikupe 'like'. Hii ni zawadi ya kipekee kabisa toka kwangu kuja kwako. Nategemea huu utakuwa mwanzo wa kuelewana vizuri kati yetu.
 
Na Tanganyika haihitaji Zanzibar katika mambo ya Bandari. Uchumi si siasa za Muungano! ni namba

Tuna Bandari na maeneo ya kujenga Bandari, wazo la kupeleka Bandari Zanzibar halina maana.

Kwamba tuingie gharama za kuvusha makontena badala ya kuyashusha Dar, Tanga, Mtwara au Bagamoyo!
Nchi za jirani zitatuona wehu! Lakini pia hawataki Muungano waacheni waende zao.
Tunahitaji Kariakoo zaidi
 
Hakuna kosa Kama kumpa mswahili mtu wa pwani madaraka makubwa. Unampa mlima tembele Urais.

Hawa jamaa akilima tuta moja la tembele na mti mmoja wa kisamvu yy maisha ameyapatia.

Nb: Sipingani na wazo lako as long as kufanya hivyo Ni maendeleo. Tatizo linakuja Ni uchumi km utaruhusu,japo sijui gharama za mradi wenyewe.

Japo sijajua gharama za hiyo barabara na hiyo reli ya chini ya maji.ili kuona km linaweza kufanyika Jambo kubwa zaidi ya hiyo barabara.

UTAKUBALIANA NA MM KWAMBA MARA NYINGI SISI WATZ SI WATU WA MALENGO MAKUBWA.TUNAFANYA MIRADI MINGI KWA AJILI YA LEO TU.na ni kutokana kuweka siasa mbele zaidi.Siasa imeathiri Mambo mengi Sana.
 
Kwann isijengwe Zanzibar bandari kubwa iwe Freeport kama ya Dubai
Kwanini isijengwe bandari kubwa ya bagamoyo iwe freeport km ya Dubai.

Mizigo ikatoka china direct to bagamoyo. Na nchi zetu zikahudumiwa kwa urahisi zaid.

Nb:Naona mnaanza kuhamisha wazo la ujenzi wa bandari y bagamoyo kupeleka Zanzibar.
 
Kwanini isijengwe bandari kubwa ya bagamoyo iwe freeport km ya Dubai.

Mizigo ikatoka china direct to bagamoyo. Na nchi zetu zikahudumiwa kwa urahisi zaid.

Nb:Naona mnaanza kuhamisha wazo la ujenzi wa bandari y bagamoyo kupeleka Zanzibar.
Diaspora wamesema watajenga daraja toka Zanzibar hadi Dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…