Tafiti mpya yabainisha ubora wa kinywaji kijulikanacho kama mbege!

Tafiti mpya yabainisha ubora wa kinywaji kijulikanacho kama mbege!

Hii sio kweli sababu zamani mbege ilikua kama bure tu alafu kila jumapili kulikua na sherehe ya mbege na nyama kwa siku 2-3

Kipindi safari kubwa inauzwa 700 mbege ilikua Tsh 100 kwa lita. Leo safari kubwa ni 2000 mbege ni 500.
Kwahiyo ulichokiandika ni uongo mkubwa kabisa
ukiambiwa ulevi uliwashusha nguvu kiuchumi na afya hadi sasa kupokea kichapo kwa wake zao haimanishi mbege ilikua ghali, bali ulevi huambatana na umalaya ukiambiwa mtu kamaliza kilabuni elifu hamsini sio kanunua mbege pekee za hiyo pesa bali na umalaya kauingiza ndani meku
 
Mangi kuna Ulanzi..aisee kitu moja baridi mno😀😀..
Mambo ya asili raha sana,mbege uweke na kanyagi kwa mbaaali..ewaaa..
Kuna togwa lile sijui haya mambi yameishi wapi..
Watu wanakufa na Energy😀😀😀😀
 
Nimeishi Moshi muda mrefu bila kuonja pombe ya mbege. Niliishia kunywa juisi yake tu kabla haijageuka kuwa pombe, kwa hiyo sijui ladha ya pombe ya mbege ikoje
 
Yani vibe la nyumbani ni la kipekee ,kula mbege choma nyama na kucheza mziki😄 ,hapo bado hatuchafua meza na bia 😁
Unakumbuka ile kijana ukitaka kuoa unajenga kwanza, unaandaa sherehe alafu yule binti unaemtaka unaongea na mashoga zake unawapanga waje nae lakini wasimshtue... Mziki ukikolea ikifika jioni au usiku unaenda alipokaa bint mhusika unasaidiwa na marafiki zake au marafiki zako wa kiume anabebwa juujuu hadi ndani kwako, wao wanaondoka wanafunga kwa nje mnaachwa huko hata siku 2 inakua ndio umeoa hivo.
Yani mkishafungiwa hata bint apige kelele hatoki,, sanasana wazazi ndio watakua wanaleta chekula na dirishani alafu asubuh wazazi wanaenda kwa wazazi wa binti kutoa taarifa kwamba mtoto wenu yupo kwetu... Kiutamaduni hii inakua imeisha mnaaza mipango ya ndoa 😁😃😃
 
ukiambiwa ulevi uliwashusha nguvu kiuchumi na afya hadi sasa kupokea kichapo kwa wake zao haimanishi mbege ilikua ghali, bali ulevi huambatana na umalaya ukiambiwa mtu kamaliza kilabuni elifu hamsini sio kanunua mbege pekee za hiyo pesa bali na umalaya kauingiza ndani meku
Hii si kwa mbege uchagani sasa hivi kuna pombe nyingi za hovyo , ambazo vijana na wazee wa sasa wametumbukia huko , ila mbege imetoa vichwa ambavyo vimeweka legacy ya mchaga duniani.
 
Unakumbuka ile kijana ukitaka kuoa unajenga kwanza, unaandaa sherehe alafu yule binti unaemtaka unaongea na mashoga zake unawapanga waje nae lakini wasimshtue... Mziki ukikolea ikifika jioni au usiku unaenda alipokaa bint mhusika unasaidiwa na marafiki zake au marafiki zako wa kiume anabebwa juujuu hadi ndani kwako, wao wanaondoka wanafunga kwa nje mnaachwa huko hata siku 2 inakua ndio umeoa hivo.
Yani mkishafungiwa hata bint apige kelele hatoki,, sanasana wazazi ndio watakua wanaleta chekula na dirishani alafu asubuh wazazi wanaenda kwa wazazi wa binti kutoa taarifa kwamba mtoto wenu yupo kwetu... Kiutamaduni hii inakua imeisha mnaaza mipango ya ndoa 😁😃😃
Ila hii mpaka wazee wachungulie ukoo wake kwanza 😄
 
Mbona sasa kuna watu wanainywa mchana na jioni hawaugui?
Kimwili ndio NI kweli kuugua NI nadra Sana NI Kama haya makomoni tunayonywesha na CCM Tangu 1961 unaambiwa yanapikwa Kwa vidonge image pombe ndani inadawa kabisa. But ukija kwenye Afya ya akili kusema kweli Akili mnembe ifanyiwe maboresho zinapatikana na hardware wachaga na wapare wawe wanafungiwa Kwa vichwa vyao .
 
Bibi yangu mzaa baba ana 112 yupo na yupo fiti ,kila siku lazima apate kitochi/ bohora moja, yeye babu kafa na 95 , tafiti weka kapuni😁
Kinachoharibu vijana kule sio mbege bali ni hizi pombe za viwandani... Vijana kule wanakunywa mbege nyingi wakiona hawalewi wanasema ngoja wakapige kali ili kichwa kiwake
 
Sasa hao watafiti wangesema haifai unadhani wangeishije hapo moshi?

Hata hapa jf tukipinga wee unadhani wachaga watatuelewa basi?

haya mbege nzuri baraa
 
Nasikia kuna pombe za kienyeji kama pombe ya nyanya, miwa, lade na zingine za ajabuajabu. Kama mbege ina afya basi hata pombe zingine za kienyeji kama mtukuru, komoni, kangara na wanzuki zitakuwa na afya, sema tu watafiti hawajazifanyia utafiti
 
Back
Top Bottom