Tafiti mpya yabainisha ubora wa kinywaji kijulikanacho kama mbege!

Tafiti mpya yabainisha ubora wa kinywaji kijulikanacho kama mbege!

Unakumbuka ile kijana ukitaka kuoa unajenga kwanza, unaandaa sherehe alafu yule binti unaemtaka unaongea na mashoga zake unawapanga waje nae lakini wasimshtue... Mziki ukikolea ikifika jioni au usiku unaenda alipokaa bint mhusika unasaidiwa na marafiki zake au marafiki zako wa kiume anabebwa juujuu hadi ndani kwako, wao wanaondoka wanafunga kwa nje mnaachwa huko hata siku 2 inakua ndio umeoa hivo.
Yani mkishafungiwa hata bint apige kelele hatoki,, sanasana wazazi ndio watakua wanaleta chekula na dirishani alafu asubuh wazazi wanaenda kwa wazazi wa binti kutoa taarifa kwamba mtoto wenu yupo kwetu... Kiutamaduni hii inakua imeisha mnaaza mipango ya ndoa 😁😃😃
Hata kwa Wahaya ipo hiyo.
 
Huku mjini twanywa uji wa uleziii na kuona wa muhimu

Kule kijijini wanaloweka ulezi na ukishaanza ota wananika na kuusaga kisha kuchanganya na juice ya ndizi na kutengeneza mbege ..... = nguvu > extra plus
 
Ngoja niseme kitu,

Mbege ni product au kinywaji kitokanacho na zao kuu la ndizi, ikichanganywa na ulezi na unga wa mseseve/we kupunguza ukali wa sukarii ya ndizi na ulezi....

Ndizi ni ndizi ambazo zimeiva vzr hutumika kuandaa mbege,

Vifaa vya kuchemshia na ndoo kuwekea zinabidi ziwe safi haitakiwi ipate mchanganyiko wa kitu kama sabuni, magadi, chumvi au mfanano wa vitu hivyo huharibu mbege Jumla.


Mbege itachemshwa na kutiwa maji safi hasa ukizingatia kule maji ni ya asili ambayo hayana chumvi au magadi au maji yaliyovunwa ya mvua,

Ikichemshwa itaiva kabisa na kuepuliwa kwetu tulikuwa tukichemsha jumanne basi alhamisi tutaikamua kwa mfuko safi, usiwe contaminated na vitu km sabuni, chumvi, magadi na mfanano wa vitu hivyo,


Tukishaikamua inatiwa kwenye pipa, au dramu, ndoo safi theni unatia unga wa ulezi kulingana na ujazo wa pipa linachukua ndoo ngapi ikiwa utatumia ndoo kujaZa kwenye pipa,

Then ijumaa yake itasongwa au kupika ule unga wa ulezi uive fresh wata ongezea siku ya kunywa ile jumamosi au jumapili, lkn ya kupika ulezi sio lzm sana ni baadhi ya watu wanafanya hayo....


Kuna hii inapikwa ya unga wa mahindi nadhani maeneo mengi inapikwa sio Moshi pekee....

Ambapo wengine wanakanda unga wa mahindi na maji safi na ukiwa tyr unahifadhi kwenye vyombo safi, nimesahau muda

Lkn ukianza kuonyesha kubadilika hivi, wanaukwangua layer ya juu vzr, then kilichopo ndani wanaeka kwenye kifaa flani kwa ajili ya kuipika kiaina ambapo itapikwa fresh mpk iive,

Utaepua na ikipoa utaeka kwenye pipa au chombo kingine then unaeka maji unaicha, utaongezea ulezi, utakamua inakuwa tyr kwa kunywa inachukua siku moja plus masaa kwa kutumika toka kupikwa

Ambapo wengine wata mix na mbege sasa au kunywa yenyewe bila mbege au mbege pekee,

Mbege inakuwa afya hasa ukizingatia kula chakula ndipo unywe mbege, chakula ni muhimu kwenye mwili wa binadamu hata unywe soda kama huli ni tatizo,

Ukipata msosi wako vzr, ndizi, makande, kitawa, machalari au ugali ukinywa mbege Haina tatizo,

Tatizo ni baadhi ya watu kunywa bia, spirits mwingine wine, ana mix hiyo ni changamoto

So far mbege bado ni kinywaji Bora kwangu nakuheshimu sana.... Imewatoa watu wengi kwenda shule, kupata bills za kutimiza kwenye maisha ya kila siku, wengine mtaji inategemea na ukubwa wa biashara yako,
Kitawa ,ummetisha mkuu ummenikumbusha mpka mate yametoka
 
Kitawa ,ummetisha mkuu ummenikumbusha mpka mate yametoka
Karibu sana meku, watu wengi hawali chakula wakashiba ndo ttzo na kuisingizia pombe

Kingine kiasi kwenye utumiaji wake pia...

Mfn tumchek jamaa yetu janabi hanywi pombe eeh unamwonaje ? Japo umri umeenda

Kupata lishe nzuri ukapata na kitochi chako kimoja aaah safi kabisa
 
Mimi ninachoona mbege zote kule uchagani ni nzuri ukutane tu na anaejua kuitengeneza... Nikienda nyumbani wananishangaa namnunulia mtu bia alafu mimi nakunywa mbege ambayo inauzwa Tsh 5oo kwa lita
Yeah! Kupanga ni kuchagua. Mbege ni the best local brew maeneo yale Ila wapo wachakachuaji ujue. Wanaongeza ugoro -ukinywa kiu haiishi. Wanachanganya na spirit ile ya kuwashia karabai - Ukinywa kitochi kimoja tu wewe chali.
 
Lazima uipulize kidogo kuweka kilemba pembeni😃 machali zangu wametoka KLM mountain wakichamba koo taratibu...
Screenshot_20250406-204653~2.jpg
 
Back
Top Bottom