Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

Hapana si lazima iwe hivyo ila kachukue album uangalie picha zote za zamani zile za watu wengi utagundua matukio mengi ya ajabu na ya kushangaza yaliyokuja kutokea baadae

Ni kweli kabisa mkuu! Kuna kitu mie nilishawahi kujiuliza haya maelezo yako ni kama umegongea muhuri!
 
duuh tafsiri ya picha zangu itakuwa na utata maana si kwa selfie hizi 50 kwa siku
lin hizo ni zako pekeyako nazungumzia zile zenye watu wengi japo pia nazo hizo selfie zaweza kucapture images ambazo tafsiri yake itakuja baadae sana.
 
Picha zinaongea, picha zinaishi picha zinatoa ujumbe maalum usioonekana kwa macho ya kawaida mpaka wakati ufike

Ukipata muda chukua album yako ya picha pitia picha za zamani ulizopiga na marafiki ndugu jamaa na hata watu usiowafahamu

-angalia mpangilio wa jinsi watu walivyosimama au kukaa nk

-angalia mpangilio wa rangi au mavazi

-angalia body language

Kwa mshangao wa ajabu utakuta kwenye picha fulani watu fulani waliosimama pamoja siku huyo au kuchuchumaa au kuvaa nguo za aina moja nk

-wote wamekufa

-wote ni matajiri

-wote wameoa/wameolewa nyumba moja

-wote tabia zao zinafanya nk

Kwa mshangao mkubwa angalia body language utajikuta unaona kabisa hao

-walikuja kuoana

-walikuja kuwa maadui wakubwa

-walikuja kuwa marafiki wa damu nk

Tunapojipanga tupige piga na kubadili badili mikao na nafasi si kwa akili zetu bali kuna nguvu nje ya ufahamu wetu nguvu ya kiroho ndio inafanya kazi

Ni nguvu hiyo inayoamua

Usimame wapi na kwa nini

Ukae wapi na kwa nini

Ufuatane na nani na kwa nini

Umtazame nani na kwa nini

Ni nguvu ya uvutano kwenye ulimwengu wa roho inayotengeneza matukio yote haya na huja kudhihirika baada ya kipindi fulani kupita...haya yanatokea si kwa utashi wetu wala uamuzi wetu wala nguvu zetu

Sijapata picha nyingine lakini naomba kuweka hii

-angalia mfanano wa rangi za mavazi

-body language

-nafasi kwenye kusimama

-umbali na ukaribu

Unafikiri walipanga kwa makusudi huu mkao?

View attachment 390085
Kaka umeongea kitu kimenigusa sana...kuhusu mambo ya Picha na matukioa yajayo[emoji122] [emoji122] umenifikirisha sana..
 
mh,sijaelewa bado katika hiyo picha mshana jr inamaana lipu na dr inawezekana kuwa kuna kitu nyuma ya pazia kimewalazimu kufanya waliyoyafanya?
Ukimsoma vzr Mshana Jr kwenye maelezo yake ya mwanzo utaelewa hiyo picha inaonyesha SLAA na LIPUMBA wanamuaga MBATIA ingawa kimwili walikuwa wote kwenye UKAWA lkn nguvu ya ziada inaonyesha hawako pamoja ndio maana unaambiwa hata ugonjwa kwa kawaida unaanzia mbali kwenye Ndoto usipuuzie ndoto zinamaana kubwa sana so alichoandika huyu jamaa nikiangalia hiyo picha nimeelewa vzr
 
Usiwe na wasiwasi kama hukuelewa au kama fikra zinakupeleka kwenye ushirikina.... vitu vimgine vinahitaji akili kubwa kuelewa..
Wakati Mshana Jr alipokuwa anaandika Mambo yanayohusu Uwepo wa uchawi na Ushirikina Bongo lala na wakurupukaji wote wakawa wanatokwa povu Mtu kitu hakielewi badala yakutulia aelewe analeta ubishi wakijinga Sasa kule aliibuka jamaa 1anaitwa Mtu mzito yule jamaa hakubakisha kitu ..Viwavi wote waliukimbia ule Uzi...nikawaida bongolala kujifanya wajuaji kumbe upuuzi tu
 
Wakati Mshana Jr alipokuwa anaandika Mambo yanayohusu Uwepo wa uchawi na Ushirikina Bongo lala na wakurupukaji wote wakawa wanatokwa povu Mtu kitu hakielewi badala yakutulia aelewe analeta ubishi wakijinga Sasa kule aliibuka jamaa 1anaitwa Mtu mzito yule jamaa hakubakisha kitu ..Viwavi wote waliukimbia ule Uzi...nikawaida bongolala kujifanya wajuaji kumbe upuuzi tu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] dolevaby umemsahau na jichawi
 
Naona kama lipumba na slaa na wengine watajiunga chama moja au kuanzisha chama.tusubiri
 
1472582131558.jpg

Hakika picha zinaongea, hii ina picha ndani ya picha......akhsante mkuu Mshana
 
Uko juu kiongozi, kuhusu picha ngoja nikakague za kwangu za zaidi ya miaka 20 iliyopita, ila nishahisi kuna kitu ntagundua

Usisahau mrejesho tafadhali mi nakuonyesha moja.

1472582226492.jpg

Hawa ni jamaa zangu hapo ni South Africa mwaka 1996 hiyo picha nilipiga mimi huyo wa katikati ni marehemu kwa sasa na hao wengine wako Ulaya.
 
Mshana uko vizuri sana kwenye psychology na Buddhism philosophy. Vipi kuhusu meditation ya mshumaa inayofanywa usiku saa sita au saa tisa.
 
Nilikuwa naifanya zamani around 1995 mpaka 1998 ila baadae nikaona inakuwa kama uchawi flani maana nilikuwa tofauti sana
Duu usingeacha iko very powerful..mimi nilianza 1996
 
Back
Top Bottom