Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

Dah kuna picha natizama tulipiga kundi aisee kuna walio tangulia mbele za haki Kwa kufata miaka tofauti na wengine kuwa maadui
 
Ebu Tafsir hiyo@Mshana Jr
20181221_075658.jpg
 
Black civil rights leaders kwenye picha ya pamoja mwaka 1963, John Lewis amefariki Friday juzi kwenye picha ni wa Kwanza/mwisho kushoto. Ndiye pekee aliyekua amaebaki hai , Luther alikua wa kwanza kufa.
Screenshot_20200718_094223_com.guardian.jpg
 
Ebu tupeni picha ya pamoja walio piga marais wa Tanzania hivi karibuni tuje tutafsiri picha katika ulimwengu wa roho.
 
Picha ni sehemu ya mwili wako iliyo nje yake wachawi na waganga huroga katika baadhi ya matukio kwa kutumia picha na kinacholeta uhai uhalisia na mawasiliano ya kiroho ni sura.
Katika kitu huwa sipendi kupiga picha ,toka primary hadi sasa ,picha nilizopiga hazifiki 50
 
Picha zinaongea, picha zinaishi picha zinatoa ujumbe maalum usioonekana kwa macho ya kawaida mpaka wakati ufike

Ukipata muda chukua album yako ya picha pitia picha za zamani ulizopiga na marafiki ndugu jamaa na hata watu usiowafahamu

- angalia mpangilio wa jinsi watu walivyosimama au kukaa nk
- angalia mpangilio wa rangi au mavazi
- angalia body language

Kwa mshangao wa ajabu utakuta kwenye picha fulani watu fulani waliosimama pamoja siku huyo au kuchuchumaa au kuvaa nguo za aina moja nk

- wote wamekufa
- wote ni matajiri
- wote wameoa/wameolewa nyumba moja
- wote tabia zao zinafanya nk

Kwa mshangao mkubwa angalia body language utajikuta unaona kabisa hao

- walikuja kuoana
- walikuja kuwa maadui wakubwa
- walikuja kuwa marafiki wa damu nk

Tunapojipanga tupige piga na kubadili badili mikao na nafasi si kwa akili zetu bali kuna nguvu nje ya ufahamu wetu nguvu ya kiroho ndio inafanya kazi

Ni nguvu hiyo inayoamua:

Usimame wapi na kwa nini
Ukae wapi na kwa nini
Ufuatane na nani na kwa nini
Umtazame nani na kwa nini

Ni nguvu ya uvutano kwenye ulimwengu wa roho inayotengeneza matukio yote haya na huja kudhihirika baada ya kipindi fulani kupita...haya yanatokea si kwa utashi wetu wala uamuzi wetu wala nguvu zetu

Sijapata picha nyingine lakini naomba kuweka hii

- angalia mfanano wa rangi za mavazi
- body language
- nafasi kwenye kusimama
- umbali na ukaribu

Unafikiri walipanga kwa makusudi huu mkao?

Kweli
 
Kwa kweli pindi mzee wetu Mengi alipotutoka nakumbuka siku ya mwisho kumuona kwa Tv moyoni lilikuja wazo tu kama kuna kitu ila sikujua ni nini baada ya muda tu likatokea jambo, pia kwa mzee wetu nakumbuka siku ya mkutano mkuu ilinitokea kama vile vile alikuwa mtu wapekee kati ya wote nilio kuwa nawaangali ila sikujua kwa nini, ila nimejifunza kitu, tuwe makini sana na sauti zinazotujia kwa nadra sana, huwa zinataarifa muhimu sana. Watch out.
 
Back
Top Bottom