DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ulishawahi kuona mtoto wa bilionea anaajiriwa hovyo hovyo ?.

Ukiuliza huyo Bon anafanya biashara gani na analipa kodi iasi gani utabaki kushangaa na kusikitika.
Leo hii hakuna trafic asiyekuwa na usafiri wa uhakika,nyumba nzuri kwasababu ya rushwa za barabarani,jiulize kwanini askari anyelinda bank hana hata baskeli !.

Nchi yetu inahitaji viongozi watakao kuwa tayari kupambana na mifumo ya rushwa.
Acha nchi ifunguliwe
 
Kama umeishi US ndio huyo aliyesoma HGL akiamua anaweza kuwa Daktari.
Unajua kwanini US inaitwa the land of opportunities?
Kama unakaa mswekeni huwezi kuelewa
US sijaishi ila naelewa Mifumo ya maisha ya kule nina watu wangu wa karibu wanaishi huko karibu kila siku nawasiliana nao.
 
Kwa hiyo unamaanisha Bongo aliyesoma HGL hawezi kuwa Daktari akiamua?
Ata ukiamua nafasi ya kufikia ndoto zako ni hafifu.prof waliojaa chuki wanataka wawe wao tu hawataki kufungua njia kwa wengine.
Mdogo wangu alifelishwa muhimbili kisa chuki za prof , kaenda US kuanza upya mbona amemaliza na kazi anafanya uko uko ina maana muhimbili unv ni bora kuliko John Hopkins unv?
 
View attachment 2630959View attachment 2630960


Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia (pichani), maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.

Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.

Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.

Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.

Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.

Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.

Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Hawa washenzi ndio wanabambikia watu kodi za bilioni 30 kwenye kontena za vitenge mbwa hawa.., aeleze pesa katoa wapi mbwa huyo!
 
Akija na michoro mizuri ya msingi kuna namna ya ku prove kilichomo chini ya ardhi na kilijengwa vipi ? Size ya nondo na ratio ya zege la mikanda miwili ya chini unawezaje kuithibitisha kama hukuwepo siku wanamwaga zege ? Au jiwe la jamvi, unajuaje ametandika ubuyu au jiwe kichwa wakati yote yashafukiwa chini ya jamvi?
Mimi nipo kwenye hii kada ya ujenzi, kwahiyo nitakachokujibu naomba uniamini. Ukijenga jengo refu kama hilo bila kibali, kinachotakiwa kufanyika ni kulivunja kwanza, halafu ndio uanze kutoa hayo maelezo ya michoro nk.

Au laaa, utoe rushwa ya kueleweka, yaani rushwa kubwa. Maana watu wanaweza kufa hapo.

Nimemaliza na sitaki maswali.
 
Mawazo ya kipimbi haya! Wahasibu wangapi wameajiriwa TRA?
Dawa ni kusomea uhasibu au kodi kwa gharama yoyote . Utumishi ajira za tra zinatangazwa kila baada ya muda mfupi na wala hazina ugumu.

Sema maskini wengi waoga hukimbilia ualimu na udaktari ili wakashike maiti. Hata mashamba ya ukoo uza jisomeshe au somesha mtoto
 
Tanzania ndio mnaukuza udaktari kwamba wenye akili ndio wanasoma udaktari.
Nenda us,uk, Sweden hiyo ni kozi ya kawaida tu kama kozi nyingine,mfano mtu yoyote US akitaka kusoma udaktari anasoma vzr tu na anamaliza.
Uku kwetu Tanzania kwenye elimu ya kukomoana na hao prof uchwara ndio wanasababisha hiyo kozi iwe ngumu.
Usisifie sana udaktari kwamba ni kozi ngumu
Peleka pua ndo utajua ugumu au wepesi wake, maneno ya kulialia hayabadili chochote.
 
Back
Top Bottom