Tahadhari: CCM na viongozi wake mnajihatarisha kwa namna hii

Tahadhari: CCM na viongozi wake mnajihatarisha kwa namna hii

CONSISTENCY

Senior Member
Joined
Feb 16, 2023
Posts
196
Reaction score
424
Kuna matukio ya uwizi wa kura, ufisadi wa mali za nchi, mikataba ya hovyo kuhusu rasilimali za nchi mfano bandari, misitu n.k Kufukuza Masai katika ardhi yao ya asili, kupanda kwa gharama za maisha na aina nyingine ya maovu mengi yanayofanywa viongozi wa serikali, chama tawala, taasisi za usalama n.k kwa namna moja au nyingine.

Sasa hayo matukio yanamfanya mwananchi awe na huzuni, kumkosesha huduma nzuri kama hospitali na maji, kumuibia rasilimali n.k ila mambo hayo hayamfanyi mwananchi kutaka kulipiza kisasi sababu ni matukio jumuishi kwa watu wote.

Ila sasa Kuna matukio yanayohusishwa na serikali, chama tawala, polisi, TISS n.k matukio yanayoendelea sasa ya kutekana, vifo, kujeruhi kwa kiwango kibaya, udhalilishaji na mengine mengi yanayofanana na hayo.
Ukiangalia hayo matukio wahanga ni wanachama wa vyama vya upinzani, wakosoaji wa sera mbovu za serikali iliyopo madarakani na chama tawala, taasisi za dini, wanaharakati n.k
Baadhi ya watu waliowai kufanyiwa matukio kama hayo ya kufanyiwa uovu ni Tundu Lisu, Kibao, Maria Sarungi, Askofu Kitima, Aquilina, Dr Slaa, Mawazo na wengine wengi sana.

Hivyo ukiangalia hayo matukio ya utekaji, vifo, kujeruhiwa n.k ukiangalia sio jumuishi kwa wananchi wote bali yanafanywa kwa watu wachache, hivyo hao watu wachache ndio wanapata maumivu, sasa hatari ni kama ifuatavyo.

Kuna watu hawawezi kuvumilia huo uovu mnaofanya kwa ndugu zao na kitakachoweza tokea ni kwamba kunaweza kuanza kuzuka na matukio ya ulipaji kisasi kwa watoto na ndugu wa viongozi wa serikali, chama tawala, polisi n.k sababu mtu ataona namna nzuri ya kupunguza maumivu kwa kifo, majeraha na kuteka kwa ndugu yake na yeye ataenda kutenda hivyo kwa ndugu na watoto wa viongozi wa serikali, chama tawala, polisi n.k bila kujali kiongozi husika wa hizo taasisi amefanya au hajafanya huo uovu ila lengo likiwa wote tupate maumivu sawa,
sababu inawezekana vipi upande mmoja wa watu wapate maumivu na wakati wengine wakiendelea kuchekelea Kila siku huku wakifanya propaganda na maisha ya wananchi wengine.

Ninyi viongozi wa serikali, chama tawala, taasisi za usalama n.k Kuna watoto na ndugu zenu wengi wa karibu wanaofahamika katika mikoa mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, sasa haya maovu yanayoendelea katika nchi mnayafanya gizani na wananchi wakianza kuyafanya gizani kwa watoto na ndugu zenu hali inaweza kuwa mbaya sana Kuna mifano mingi sana katika nchi nyingi hapa duniani matukio ya ulipaji kisasi kwa viongozi wa serikali, chama tawala, taasisi za usalama n.k yametokea na yanaendelea kutokoea.

Wito wangu kwa viongozi wote wa serikali, chama tawala, taasisi za usalama n.k tujitahidi kufanya siasa safi na kama hauwezi kufanya siasa safi basi kemea hizo siasa chafu ili wananchi wakujue wewe ni wa siasa safi au chafu,
Wewe kiongozi wa serikali, chama tawala, taasisi za usalama n.k unatakiwa ujue kwamba kama wewe upo upande wa siasa chafu na haukemei huo uchafu maana yake wewe ni mnufaika wa huo uchafu hivyo endapo huo uchafu unaonufaika nao ukiwarukia watoto na ndugu zako wa karibu usishangae.
 
Mama Samia has to go..
Hilo jambo ni zaidi ya samia sababu samia alikuja, yupo na ataondoka ila nchi itaendelea kuwepo hivyo ni vyema viongozi wote kua na nidhamu kwa maisha ya watanzania na usalama wao.

Ila kama na yeye samia anahusika na huo uchafu na hachukui hatua ya kuzuia hivyo siku huo uchafu ukiwarukia watoto na ndugu zake wa karibu asije kushangaa.
Siku zote chuma hufua chuma
 
Si nyie mnapigia debe kila hoja ya kijani na manjano, sasa wamelewa madaraka.
 
Rais nakukubali sana
Acheni ninyi kiti cha urais kitamu Bana.

Umekaa umetulia na kusema ebana Mimi Leo ndio naongoza hii Bendera.

Rais wangu Samia Mitano yako Iko palepale Hadi umalize Hilo linajulikana maneno yataongelewa lakini ukweli ni kwamba miaka 10 lazima itimie ukiwa Hai.
 
Rais nakukubali sana
Acheni ninyi kiti cha urais kitamu Bana.

Umekaa umetulia na kusema ebana Mimi Leo ndio naongoza hii Bendera.

Rais wangu Samia Mitano yako Iko palepale Hadi umalize Hilo linajulikana maneno yataongelewa lakini ukweli ni kwamba miaka 10 lazima itimie ukiwa Hai.
Ndio mlivyofundishwa kumpamba hivyo?
 
Back
Top Bottom