Ahsante sana mchambuzi wa siasa za mashariki ya kati kutoka hapo Tel Aviv, kwanza kabisa poleni na vita huko.
Ipo hivi, USA hata mwaka 2003 aliivamia Iraq akiwa na washirika wake pamoja ushirikiano wa nchi nyingine zaidi ya 40, just imagine hadi Rwanda ilienda, hadi Angola.
Kwa kuanza tu, US aliingia akiwa na wenzake Poland, UK, Australia.
Nchi nyingi hivi sasa zina uelewa wa kutosha kuhusu ujanja wa USA, waliingia Iraq kwa kile walisema wana silaha za maangamizi, wakakuta hamna kitu.
Usifikiri huo ushawishi USA anao tena hii miaka.
USA pekee haitoshi kuivamia Iran kijeshi, Iran inaweza kushambulia nchi yeyote mashariki ya kati kwa missiles zao zenye shabaha ya hali ya juu.
Hakuna nchi Ulaya ipo tayari kuivamia Iran, uongo wa USA na ujanja wake wengi wameufahamu, ndio maana hivi sasa unaona nchi nyingi zinataka kujiunga BRICS kama mpinzani wa umoja na ushawishi wa nchi za kimagharibi zikiongozwa na USA.
Iran kwa kurusha zile missiles 200, ilikuwa ni kutangaza vita tayari, kama USA alikuwa anatamani kuivamia Iran ilikuwa ni kesho yake, Israel imeshabuliwa mara mbili tunashuhudia, lakini wachambuzi kutoka Kibondo mnavyokuza mambo hajambo.
Israel inaogopa kuingia kwenye vita ya moja kwa moja na Iran, ingekuwa inajiamini na inataka vita, ingepiga kwa nguvu kama inavyofanya Gaza na Syria.
Iran sio Libya mzee.