Tahadhari kwa Iran: Usijibu Mtego wa Israel

Makombora ya Iran yalitua kila mahara ndani ya Israel labda kama walizificha Mars
kwa hiyo ziliteketea zote, sasa zile zimeenda kufanya shambulizi majuzi iran zilikuwa ni zipi? mbona mnapenda kujidanganya?
 
Kama kuna mtu yupo karibu na Rais wa Iran, Ayatollah, amfikishie ujumbe huu: Asithubutu kujibu mashambulizi ya Israel – huu ni mtego wa hatari!

1️⃣ Mpango wa Kimkakati wa Israel
imeanza na mkakati wa kuwadhoofisha washirika wake wa karibu, makundi ambayo yamekuwa tishio kubwa kwake. Baada ya kuyapunguza nguvu, sasa macho yake yameelekezwa kwa “baba” wa makundi haya – Iran.

2️⃣ Hali hii si ya bahati mbaya. Israel haipigi bila hesabu. Wanajua wanachofanya na wanasubiri tu kosa dogo kutoka Iran. Kosa hilo linaweza kuwa jaribio la Iran kulipiza kisasi.

3️⃣ USA Ipo Tayari Kuingilia
Israel haitapigana vita hii peke yake. Marekani ipo nyuma yake ikisubiri wakati muafaka wa kuingilia vita moja kwa moja. Mashambulizi yoyote ya Iran kwa Israel yatatoa sababu kamili kwa Marekani kushambulia kwa nguvu zote. Vita hiyo haitakuwa tena kati ya Israel na Iran, bali Iran dhidi ya Marekani na washirika wake.

4️⃣ Intelijensia Imara ya Israel
Israel inazo taarifa za kina kuhusu miundombinu ya kijeshi na operesheni za Iran. Wanatafuta tu sababu ya kuanzisha mashambulizi makubwa zaidi. Kujaribu kurudisha mashambulizi kunaweza kuwa sawa na kuwasha moto mkubwa zaidi kwa Iran.

USHAURI: Iran inapaswa kuwa na subira sana kuepuka mtego huu. Siasa na diplomasia kwa sasa ni silaha muhimu zaidi kuliko vita ya wazi. Kujibu kwa pupa kutawapa israel na USA nafasi waliyoisubiria.

"Katika vita ya akili, nguvu huangukia kwa yule anayejua kucheza kwa busara."
kwakweli shingo yako imebea mzigo
 
Jamii Forum ya siku hizi….
Yaani ukilala ukiamkaaa Great thinker unaanzisha Uzi magreat thinker we zako wanachangia ,,,,,maisha yanendelea 😂😂😂🙌🏿🙌🏿🙌🏿🙌🏿
 
Israel daily mikwala, alirushiwa missile zakutosha lakini mbona hajaingia kwenye total war pamoja na boss wake....?
Iran ya enzi za gulf war msijehisi bado ipo vile vile. Kama waumini wa mwamposa wanamaanisha vita basi waingie mazima waache mikwala mara mitego
 
Iran aje aongee na mama yetu, hapa Tz tuna wajeda wanapasua tofali kwa kichwa ila lisiwe gumu s
 
Umeongea ukweli kabisa,jamaa wamesema wametoa chai tu juzi.
Nyau kasema hawa watalipa maisha yao yote..
Hii vita watu wanachukulia poa,sijui km waliona lile kundi lilitoka Us na Canada tar 8 mwaka jana.
Ndo hao vijana tu wanapiga mpk mende.
Hao ndo wako frontline,ua kumi mnauliwa 1000
 
Kama kuna mtu yupo karibu na Rais wa Iran, Ayatollah, amfikishie ujumbe huu: Asithubutu kujibu mashambulizi ya Israel – huu ni mtego wa hatari!

1️⃣ Mpango wa Kimkakati wa Israel
imeanza na mkakati wa kuwadhoofisha washirika wake wa karibu, makundi ambayo yamekuwa tishio kubwa kwake. Baada ya kuyapunguza nguvu, sasa macho yake yameelekezwa kwa “baba” wa makundi haya – Iran.

2️⃣ Hali hii si ya bahati mbaya. Israel haipigi bila hesabu. Wanajua wanachofanya na wanasubiri tu kosa dogo kutoka Iran. Kosa hilo linaweza kuwa jaribio la Iran kulipiza kisasi.

3️⃣ USA Ipo Tayari Kuingilia
Israel haitapigana vita hii peke yake. Marekani ipo nyuma yake ikisubiri wakati muafaka wa kuingilia vita moja kwa moja. Mashambulizi yoyote ya Iran kwa Israel yatatoa sababu kamili kwa Marekani kushambulia kwa nguvu zote. Vita hiyo haitakuwa tena kati ya Israel na Iran, bali Iran dhidi ya Marekani na washirika wake.

4️⃣ Intelijensia Imara ya Israel
Israel inazo taarifa za kina kuhusu miundombinu ya kijeshi na operesheni za Iran. Wanatafuta tu sababu ya kuanzisha mashambulizi makubwa zaidi. Kujaribu kurudisha mashambulizi kunaweza kuwa sawa na kuwasha moto mkubwa zaidi kwa Iran.

USHAURI: Iran inapaswa kuwa na subira sana kuepuka mtego huu. Siasa na diplomasia kwa sasa ni silaha muhimu zaidi kuliko vita ya wazi. Kujibu kwa pupa kutawapa israel na USA nafasi waliyoisubiria.

"Katika vita ya akili, nguvu huangukia kwa yule anayejua kucheza kwa busara."

Hakuna mtego hapo zaidi ya kuwa ndume zinaogopana:

IMG_20241026_111612.jpg

IMG_20241026_090324.jpg

Zingatia Israel Sito Marekani.
 
Back
Top Bottom