Uchaguzi 2020 Tahadhari kwa mawakala kwa vyama vya upinzani nchini tarehe 27/10/2020 mkalale kwenye ofsi za vyama vyenu

Mkuu hawa watu wamekaa na hizi sheria za uchaguzi tangu viongozi wao wasaini kuzikubali.Leo bado siku 11 ndiyo wanaanza kutangaziana mikakati tena kwenye mikutano ya hadhara. Ccm wako organised sana na ndiyo chama kinachotarajiwa kushinda.
 
Hili la mawakala inabidi viongozi waliangalie kwa umakini maana kwahali ilivyo kwasasa lazima ccm watafanya uhuni wao kukwamisha mawakala wa CHADEMA/ACT
 
Sio tare 27 mzee ni kuanzia tar 20 hawatakiwi kuonekana mahala popote.
 
Kiufupi tumeshavuka viunzi vyote. Na tumeshashinda mpaka sasa.subirini kulala na viatu 1 nov 2020.
 
Ili mjue tumelala wapi mtuteke vizuri? Hatudanganyikibtutalala hata guest house ila hatulali mnapotuagiza.
 
Kama nilimsikia vizuri Mahera, hakuna wakala atakayepewa barua ya uteuzi ila watazikuta kwa Msimamizi wa Kituo zikiwa na picha yake. Hivyo Msimamizi ataangalia picha, ni wewe anakuruhusu. Wasiwasi wangu hapa ni Counter attack ya mawakala. Yaani chama chako kimekupangia Kituo X unafika unakuta wakala tayari yupo anajiita wa chama chako huku wewe unamjua kabisa ni Green Guard.
 
Hili la mawakala inabidi viongozi waliangalie kwa umakini maana kwahali ilivyo kwasasa lazima ccm watafanya uhuni wao kukwamisha mawakala wa CHADEMA/ACT
Mnachekesha sana yaani hata mawakala hamjateua, duuu upinzani mna shida vichwani mwenu.Halafu mtawatrain lini.Ndiyo maana tunasema ccm 89% victory , 11% others
 
Mkuu hawa watu wamekaa na hizi sheria za uchaguzi tangu viongozi wao wasaini kuzikubali.Leo bado siku 11 ndiyo wanaanza kutangaziana mikakati tena kwenye mikutano ya hadhara. Ccm wako organised sana na ndiyo chama kinachotarajiwa kushinda.
Wapuuzi sana
 
Tatizo ni kwamba distribution ya vituo kwa mawakala ni siri ya tume mpaka siku ya uchaguzi
 
Mnachekesha sana yaani hata mawakala hamjateua, duuu upinzani mna shida vichwani mwenu.Halafu mtawatrain lini.Ndiyo maana tunasema ccm 89% victory , 11% others
mawakala ambao hawajateuliwa labda wa mataga, Lakini mawakala wa Chadema wapo tayari toka tarehe10/10 Mlidhani mnyika kaacha kugombea ubunge kwa bahati mbaya? Safari hii inabidi watekaji watoke NEC, na ni ubaya ubaya tu ,wakitafuta maneno watayapata!
 
Ha ha ha wewe ni nani umshauri mwenye saccos yake. Ushauri wako ni kama vumbi tu,hakuna hata mjumbe wa shina atakaye usikia.
 

Kipigo cha kushindwa kiko palepale?!Ni afadhali kwa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko Magufuli kurudi ikulu!Mnadai kuwa kwa kipindi cha miaka mitano magufuli amefanya mambo makubwa sana.Kama amefanya mambo makubwa sana inakuwaje yeye leo hii anawahitaji wananchi kuliko wananchi wanavyomuhitaji yeye?Unaelewa kuwa kitendo cha magufuli cha kuomba kura kwa kupiga magoti ni kwamba anawahitaji wananchi kuliko wananchi wanavyomuhitaji yeye na amekata tamaa?

Yaani uwafanyie wananchi mambo makubwa sana halafu ukawaombe tena kuwatumikia kwa kupiga magoti?Inaleta sense?Kama amewafanyia wananchi mambo makubwa sana ni nani anatakiwa kumuhitaji mwenzake kwa kupiga magoti?

Kama amewafanyia wananchi mambo makubwa sana hao wananchi ndiyo wanapaswa kumpigia Magufuli magoti kumuomba aendelee kuwa Rais wao ili aendelee kuwafanyia mambo makubwa,ila hapa inakuwa ni kinyume chake yaani Magufuli ndiye anapiga magoti!Kama Magufuli amewafanyia watu mambo makubwa sana basi atulie hayo mambo makubwa yamnadi na siyo yeye ajinadi mwenyewe tena kwa kupiga magoti na kuweweseka.

Hii inamaanisha nini?Hii ina maana Magufuli anajua kabisa hakuna la maana alilofanya kwa kipindi cha miaka mitano aliyokaa madarakani na anachofanya sasa hivi ni anataka achukue madaraka kwa njia ya kulaghai wananchi(Magoti).Huwezi kufanyia watu mambo makubwa halafu badala ya hao watu wakuhitaji wewe kuliko wewe unavyowahitaji wao iwe kinyume chake yaani eti wewe uwahitaji wao kuliko wao wanavyokuhitaji wewe.

Magufuli ni tapeli asiekuwa na aibu aliekosa kibali cha wananchi na ni heri ajitoe kwenye kinyang'anyiro hiki tena kabla hata ya tarehe ya uchaguzi apishe wenye kibali cha wananchi wachukue dola.
 

Hili la nakala ya kielektroniki ni wazo sahihi, pia tulipendekeza fomu za ugombea ziwe hivyo hivyo, lakini sidhani kama watakubali kitu kitakachowakwamisha kwenye nia yao ovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…