Uchaguzi 2020 Tahadhari kwa mawakala kwa vyama vya upinzani nchini tarehe 27/10/2020 mkalale kwenye ofsi za vyama vyenu

Uchaguzi 2020 Tahadhari kwa mawakala kwa vyama vya upinzani nchini tarehe 27/10/2020 mkalale kwenye ofsi za vyama vyenu

Hii ni kengere ya kuwaamsha na kuwakumbusha tu,
Mnakumbuka yaliyojitokeza kwa watinia Nia udiwani na ubunge ilivyokuwa kazi kurudisha fomu, watu walitangiziwa njiani na kupolwa fomu. Hiyo ilokuwa ni trela tu, msipojiandaa pia tarehe 27/10/2020 kutakuwa na vituko mpaka mtashangaa, hivyo nawashauri, baada ya kufanikiwa kuapishwa, ofsi ya vyama vyenu, kwa gharama ya chama, mnapaswa kulala kwenye ofsi zenu na ulinzi wa uhakika, baadae asubuhi muandae gari litakalowasambaza kuanzia alfajiri asubuhi, itazuia kunyang'anywa hati za utambulisho wa uwakala. Maana kazi ya tume kwenye kituo itakuwa ni kupokea wakala halali Wala siyo kuuliza Nani hajafika

Mkipuuza, msiludi kutulalamikia

#kapigekura28/10/2020
Kwani ofisi zenyewe wanazo? Makao Makuu wameshindwa kujenga ofisi wataweza kwenye majimbo? Pesa zote Faru John anazipiga tuuu!!
 
Tutabadilisha mbinu hata mngelala wiki nzima
Mmeshindwa kuomba kura wananchi mnafanya figisu makusudi huku mnahubiri amani ,hiyo ni akili au matope ?
 
Tutawatoa utumbo asubuhi asubuhi wala haina kuuliza
 
Eti wakala anaenda mikono mitupu kituo cha kupigia kura eti kujitambulisha kwa msimamizi wa uchaguzi ndio apewe barua ya uwakala??????? Rubish!!!!!!

Kwanza msimamizi wa uchaguzi atamuomba kitambulisho cha uraia au leseni ya udereva au pasi ya kusafiria ili atambue kuwa ni yeye -
1) holaa, hana! anamkataa, anasema nitajuaje kama ni wewe!

2) Kama anavyo vitambulisho vitamulikwa kwa darubini kuhakikisha havitofautiana hata kidogo mpangilio wa majina au spelling ya jina. Kama kuna tofauti yoyote msimamizi anamkataa.

Simu zitapigwa weeee, akija kukubalika ni baada ya masaa, hapo ujue kura bandia kibao zitakuwa zimeisha penyezwa.
Yaani CCM ni shiiiidaaaaa. Huo mzozo hautaishia kirahisi, ujue hapo afande tayari atakuwa kesha papasa silaha yake, wakala ataondolewa tu. Simu zitapigwa, hata ukija kukubaliwa hali itakuwa tayari ni tete!

Huo ni mtazamo wangu! We unasemaje!
 
Hapo kwenye mawakala ndio chadema inaenda kufia. Nawaza kwa yale majimbo ambayo wabunge na madiwani wa chadema walikatwa hv mnaonaje suala la mawakala.
 
Mimi kwangu nadhani uongozi wa wilaya ungefanya mpango wa wakae sehem moja na walindwe na RPC kabisa maana siku hiyo utekaji utakuwa nje nje
Walindwe na RPC? wewe unajua ulicho andika kweli, hujui kuwa hao ma-RPC ndio watekaji wenyewe.!!
 
Tafuteni sababu zote lakini kipigo cha kushindwa kiko palepale.Tayari mmeanza kukata pumzi na boss wenu ndiyo kabisa ni dembedembe.Nimemsikiliza jana hapa Tabora anatia huruma mwanzo mwisho wa mkutano hamna sera yeye ni kuongelea wizi wa kura.Badala ya kueleza Tabora watawafanyia nini yeye anaongelea wizi wa kura.By the way big 7days is around the corner, siku saba ni za kupimana ubavu wa uimara wa vyama.
Wana Tabora tumekwishaelewa sera kuwa ni uhuru, haki na maendeleo hivi sasa ni spana kwenda mbele ndizo tunazohitaji. Unaona jana mgombea wenu kaanza kunyooka mpaka anaongeza watumishi mishahara.
 
Ata hawana habari na nyie maana nyie mnajishtukia tuu sababu ukweli mnaujua ni hamuwezi kushinda kamwe ata kama lissu angepangwa na mti, watanzania wangechagua mti kuliko huyo kibaraka.
Watanzania wapi hao unaowaongelea? Ambao ni wapumbavu kiasi kwamba hawajui kuwa mti hauwezi kuwaongoza?

Na kumbuka kufanya hifadhi ya maneno usije ukaabika siku moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom