TAHADHARI: Mboga za majani wanazokula wakazi wa Dar ni sumu tupu

hivi tanzania waandishi wa namna hii ha tuna kila siku ni siasa wema diamond kiba basii hawajaona haya
 
Huna lolote uroho tu.
 

Mkuu serikali yetu ingekuwa inajali wangekuwa wameshachukua hatua siku nyingi.

Inasikitisha sana kuwa hata dawa za kuua wadudu wanzotumia wakulima si zile zinazotakiwa; na kama wakitumia dawa sahihi hawazingatii muda wa kupiga. Ni Mungu tu atusaidie maana hali ni mbaya sana...!
 
hivi tanzania waandishi wa namna hii ha tuna kila siku ni siasa wema diamond kiba basii hawajaona haya
Tatizo la waandishi wetu huangalia bahasha tu.Kama akienda mahali atapewa hela ndio anaenda.Hivi hivi haendi.Waandishi wetu wengi ni desktop publisher chanzo cha habari zao ni

1.Jamii forums na mitandao ya kijamii kama ya akina Issa MICHUZI NK
2.Internet
3.TV za nje
Wengi si wabunifu na watafuta habari mpya maeneo mbali mbali !!!

Ukisoma habari tu humu jamii forums pekee waweza jua kesho vichwa vya habari vya magazeti vitaandika nini.Kuna habari humu Jamii forums waweza jua hii kesho itakuwa headline kwenye gazeti.
Mfano Magufuli leo kaagana na Odinga kesho utaiona kwenye magazeti au kikao cha baraza la madiwani Tanga chavunjika.Kesho habari kubwa.!

Nadhani wengi wamefundishwa kuandika habari si kutafuta habari
 
ng'ombe nyingi zinazouzwa na wamasai ni wagonjwa, wafugaji hawajui kusoma lakini wanawatibu wenyewe bila msaada wa madaktari wa wanyama, upande huu pia tunapata sumu mbaya.
 
Ni kweli issue ya mboga hapa Dar ni changamoto kubwa sana. Mimi ninadhani kuna fursa ya biashara kwa anaeweza kulima mboga salama, kama ataweza kushawishi walaji
Watu watajuaje kwamba hizo ni mboga salama? ikumbukwe kwamba walaji wengi wa mboga hawaendi shambani wanapitishiwa majumbani, mimi nadhani ni wenye mamlaka ndiyo wanatakiwa kupiga marufuku kilimo cha mboga maeneo hatarishi kama ambavyo wanahangaika na watengenezaji wa bidhaa za viwandani, yaani mmeniharibia siku yangu maana nimetoka kuzozana na mama Ntilie aniongeze mboga za majani kwenye ugali wangu.
 
Kweli kabisa. Kwa anayeweza kulima mboga za majani kwenye backyard yake ni nzuri zaidi otherwise za masokoni zina utata. Kuna watu huwa hawali mboga za majani unless wanajua imelimwa/imetoka wapi ili kujiridhisha.
 
Hizi mada huwa hazipatagi nafasi jukwaani humu japo ni muhimu kuliko, lakini hazipatagi wachangiaji nashangaa kama mwamko huu umeanza kuonekana tutaokoa taifa!
 
Ukiendelea hivi ukaachana na siasa utakuwa rafiki yangu mkubwa kule unapotea YEHODAYA
ng'ombe nyingi zinazouzwa na wamasai ni wagonjwa, wafugaji hawajui kusoma lakini wanawatibu wenyewe bila msaada wa madaktari wa wanyama, upande huu pia tunapata sumu mbaya.
 
Hizi mada huwa hazipatagi nafasi jukwaani humu japo ni muhimu kuliko, lakini hazipatagi wachangiaji nashangaa kama mwamko huu umeanza kuonekana tutaokoa taifa!
Hii mada ni 2014 ila kuna mdau kaifufua nimemshukuru mno
 
Mkuu thread nzuri maana inatutahadharisha!! Sasa labda tusaidiane, je mmea ukinyeshewa maji yenye sumu hiyo sumu inaingia hadi ndani ya cell za mmea husika? Mchicha utatuumiza kwa sumu iliyo juu ya majani yake au kwa sumu iliyo ndani kabisa ya cell zake? Hebu tusaidiane hili wakuu.
 
Lete Idadi ya vifo vilivyotokea au nyamaza ewe mchochezi.... sio tumekula na tumekulia Dar hii hii sumu sumu hewa unayovuta wadhani ni salama? Mimaji ya visima,Kuku wa Kizungu,Samaki wa Baharini,ngono zembe ni zaidi ya Sumu kufa kufa tu kupo enjoy life
 
Wacha wee...! Naona wenye biashara zao wamecharuka
Kuna wakati jisikie haya kwa yale unayo comment Mlaleo
 
Kwa kweli hali hii ni balaa. Wizara na wanaharakati wanaohusika na mazingira wanatakiwa kulivalia njuga suala la kunajisi vianzio vya maji jijini Dar.
Hapa muhusika mkuu ni January Makamba, anatakiwa atembelee viwanda vinyotiririsha sumu na kuviadhibu. Labda bado anaona maruweruwe kwa kuwa alichotegemea kimekuwa juuchini chinijuu. Katika Wizara ambazo zina shughuli nyingi sana, lakini Waziri bado anaganzi ya kukosa madaraka.
 
Wacha wee...! Naona wenye biashara zao wamecharuka
Nandhani huelewi ukuaji wa mazao....... Kasome Biology vizuri utafahamu kama upo safe au lah sio kuleta blah blah
 
Nandhani huelewi ukuaji wa mazao....... Kasome Biology vizuri utafahamu kama upo safe au lah sio kuleta blah blah
Kabla sijaileta hii mada hapa nilijiridhisha kwa kusoma hiyo biology unayojivunia wewe ambayo ni segment ndogo sana kwenye food poisoning, usiangalie biology tuu ni factor ndogo sana kwenye ukuaji wa mimea na wanyama
 
Nandhani huelewi ukuaji wa mazao....... Kasome Biology vizuri utafahamu kama upo safe au lah sio kuleta blah blah
laiti kama ungekuwa umeshafanya ufugaji au ukulima japo kidogo ungemuelewa mtoa mada na ingekuwa nyongeza kwa hiyo biology!
 
Waweza nunua mbegu na kufanya kabustan kadogo na kutumia mbolea ya kuku/ng'ombe + kumwagilia!!
Sisi hatununui mboga hata!!
Mwaka wa tano huu!!
Huko kazini na mashuleni (watoto) unakwepaje hizi mboga?
Au mnabeba chakula toka home?

Yani ni shiiida...hawa TFDA sijui kwa nini hawafanyi research na kutoa tamko...(tamko kwi kwi kwi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…