TAHADHARI: Mboga za majani wanazokula wakazi wa Dar ni sumu tupu

TAHADHARI: Mboga za majani wanazokula wakazi wa Dar ni sumu tupu

Hivyo ule utamaduni wa kupanda mboga zako uwani au nje ya nyumba umeishia wapi? Manake mie nakumbuka wakati tunakua tulikua tunanunua mboga mara chache saaana. Tulikua tumepanda matembele, mboga za maboga, kisamvu nk. Lakini nyumba za siku hizi hata vimche vichache vya mboga hamna, ni mismenti kila mahali. Yaani naitamani ile hali ya zamani. Ndio maana watu utakuta wanakula mboga za majani nk, lakini bado wanakufa na kansa. Yaani siku hizi kila nyumba kuna mtu ambaye ana kansa au kafa na kansa unamjua. tubadilike jamani, tujali afya zetu.

Mabeseni na ndoo zilizochakaa weka undongo na mbolea, unaotesha nyanya, mchicha etc juu ya hiyo cement kila mahali.
 
ImageUploadedByJamiiForums1459998431.220815.jpg
wengine wameamua kupanda mboga kwa kutumia makopo ya mauwa yotee hii kuepuka mboga za msimbazi.
 
Bro umenena. Hapa Ubungu kuna bonde la mto unaotokea Msewe kupitia darajani hapo nyuma ya Chuo cha Maji Rwegarulila, maji yanayotumika ni yanayotokana na Bomba la Maji machafu na Kinyesi toka chuo cha maji. Jamaa wanaoteshea hadi kukuzia. Kwa kweli tunachokula wana Dar es Salaam ni uchafu tupu hasa hasa kwenye mbogamboga.

Usisahau pia pale Serengeti/Temeke jirani na makaburi ya Temeke. AIBU
 
to be honest mboga ni chafu ni neema za mungu tuu tunajifariji kuwa mboga za majani ni nzuri kiafya kumbe ndo tunaongeza matatizo
 
Dawa ni kuotesha bustani ya mboga mboga nyumbani kwako kama una kinafasi basi anza leo kuandaa baada ya muda utakuwa unajichumia tu matembele, bamia, mchicha au majani ya maboga kwa afya njemaa ya familia yako.
Hivi mbogamboga toka kule maeneo ya kitunda na ukonga zenyewe vyanzo vyake vya maji vipoje.
 
Nimewahi kula kwa mama n tilie taifa paleee wali mboga mboga, baada ya kumaliza nikawa nimelewa aseee. Hili ni gujipu gukubwa mnoooo, bora Cataliya analima
 
Ukweli hali inatisha
Kuna baadhi ya wanaforum wamekuja hapa na kupinga kile nilichoandika wakisema hakuna madhara yoyote...sikushangaa sana kwakuwa hatuwezi kufanana mitazamo na wengine ndio biashara zao
 
Kwani during week days hauishi hapo? Kwanini ustuke weekend kuwa spinach imeliwa na ndege
Weekdays nakuwa kazini mimi mtumishi. Au unataka watumishi tununue hizo mboga za sumu??? Unategemea nikirudi giza nikamulike na tochi kuona kama mchicha umeliwa??? Soma article za mwandishi kabla hujamjibu vinginevyo unaonekana unaongea kama bado uko shule unakaa kwa wazazi.
 
Mbona unakosa ustaarabu katika jibu lako? Sidhani kama swali langu lipo jinsi ulivyoliewa. Anyway pole kwa changamoto
 
laiti kama ungekuwa umeshafanya ufugaji au ukulima japo kidogo ungemuelewa mtoa mada na ingekuwa nyongeza kwa hiyo biology!
Mkuu Nimesoma Agriculture pia... So Naelewa nachosema
 
Kabla sijaileta hii mada hapa nilijiridhisha kwa kusoma hiyo biology unayojivunia wewe ambayo ni segment ndogo sana kwenye food poisoning, usiangalie biology tuu ni factor ndogo sana kwenye ukuaji wa mimea na wanyama
Mkuu kuna Mazao wengine tumekula yalipokuwepo Mashambani yalimwagiwa Dawa aina ya DDT ilikuwa ni sumu mojawapo tulikula lakini hatukufa Mazao hata ya Sasa yanamwagiwa Dawa kadhaa wa Kadhaa... Kuku hawa wanalishwa vyakula na Dawa ni sumu tupu anyway elewa tu haupo safe... kwa kila kitu wait tu siku yako ya kuepire ifike utakwenda tu hakuna pa kukwepa.... issue kuu leta mada za watu kuishi miaka mingi haswa wale wa japan na Amerika ya kusini wasiokula red meat hula uyoga fulani na mimea kwa wingi... kukataza mboga za Majani mie nitakupinga hadi kesho...
 
mkuu kelele za wadada na wamama, utasikia mchicha, mnavu, spinachi mbogambogaaa kwenye mitaa ya palestina sinza ziliisha baada ya kuhamia makoka sehemu pana ni full bustani. so safe!! tuwe na utamaduni wa kupanda mbogamboga hata kama una nafasi ndogo, chota udongo changanya na mbolea swafi jaza viroba then panda mboga zako punguza kula sumu. hizi kemikali jamani ndo mana watu wanazaa viumbe wa ajabu sana siku hizi!
 
Mkuu kuna Mazao wengine tumekula yalipokuwepo Mashambani yalimwagiwa Dawa aina ya DDT ilikuwa ni sumu mojawapo tulikula lakini hatukufa Mazao hata ya Sasa yanamwagiwa Dawa kadhaa wa Kadhaa... Kuku hawa wanalishwa vyakula na Dawa ni sumu tupu anyway elewa tu haupo safe... kwa kila kitu wait tu siku yako ya kuepire ifike utakwenda tu hakuna pa kukwepa.... issue kuu leta mada za watu kuishi miaka mingi haswa wale wa japan na Amerika ya kusini wasiokula red meat hula uyoga fulani na mimea kwa wingi... kukataza mboga za Majani mie nitakupinga hadi kesho...
Sasa nimegundua kuwa hukunielewa kabisa hakuna popote nilipopinga matumizi ya mboga za majani bali utaratibu unaotumika kuzikuza kwenye mabonde husika
Umetoa mfano wa DDT jiulize kwanini ilipigwa marufuku, haya mambo yana madhara ya taratibu na ya muda mrefu kwahiyo ukiangalia kwa haraka huwezi ona hayo madhara
d0d2ade83e516ae8d026c4933abf18fa.jpg
38e7afff91bbbb145dac107106f2fc15.jpg
 
Back
Top Bottom