Tahadhari: Teja akikuomba pesa mpatie, hachelewi kukusingizia unauza madawa

Tahadhari: Teja akikuomba pesa mpatie, hachelewi kukusingizia unauza madawa

FaizaFoxy , kwa lugha nyingine unaituhumu serikali kwamba inakusanya kusanya watu tu bila kufanya hata uchunguzi wa awali?

Kwamba kila mtu akitajwa hakuna intelijensia ya kuchunguza kama kuna sababu ya kumshikilia kwa uchunguzi zaidi?

Kwamba sasa jeshi letu liko katika ngazi ya sungusungu ambako mtu alikuwa akisemwa semwa tu tayari anahukumiwa na hata hukumu za vifo?

Haki itatendekaje katka jehsi la namna hii? Nini kifanyike?

Hapana, uchunguzi wa awali na "intelijensia" inaweza kuwa ile kuhojiwa tu na polisi kituoni. Sasa wawe kama mia mbili wanangoja kuhojiwa!

Fikiri.
 
acha ujuha we bibi! nimpe buku kisa naogopa kutajwa!! akwendreeee na arosto yake!

Hongera makonda Mungu atakulipa
 
kweli ban ni mbaya, bibi ana argue kistaarabu sana, hata ile signature yake ya ujinga leo siioni
 
Kwa sababu unaonekana kuwa na akili sawa na za teja nikuulize kuwa kwa mfano niko barabarani halafu hilo teja lako linaniomba hela nakataa kulipa litaenda polisi wapi ili linitaje kwa jina gani wakati limenikuta tu njiani wala halinijui?

Huwajui mateja, wana akili za ziyada.
 
Wana jamii wote tahadhari kubwa sana ichukuliwe pale teja la madawa ya kulevya (maaruf "unga") litapokuja "kukupiga mzinga" (kukuomba pesa) hususan kama tulivyowazoea omba yao kubwa ni "Buku".

Usifanye ubahili wakati huu kwani ukimuudhi tu na akienda kusema wewe ndiye unamuuzia unga utajiunga na fiesta kule central police station.

Mpe hiyo "buku" na kama hauna japo kamkopee, maana wana hasira kwani ni lazima unga utakuwa adimu mitaani kwa trend hii ya bwana Makonda inavyoenda na arosto waliyonayo, mateja wanaweza kufanya lolote la ajabu.

Tahadhari sana. Hii siyo joke.
Liwalo na liwe lakini sio kumpa teja hiyo buku kama sitapelekwa polisi kwa ajili ya huyo teja basi nitapelekwa kwa lingine
 
Hapana, uchunguzi wa awali na "intelijensia" inaweza kuwa ile kuhojiwa tu na polisi kituoni. Sasa wawe kama mia mbili wanangoja kuhojiwa!

Fikiri.
Bado siwezi kutoa buku.
Ushahidi wa teja hautoshi kunifanya mimi nishtakiwe, haya mambo ni mambo yenye uzito sio kama wizi wa biskuti
 
Hii tahadhari yako kali kweli kweli, ila mm sitoi hata mia tu! wacha polisi waje kunichunguza tu.
 
Wana jamii wote tahadhari kubwa sana ichukuliwe pale teja la madawa ya kulevya (maaruf "unga") litapokuja "kukupiga mzinga" (kukuomba pesa) hususan kama tulivyowazoea omba yao kubwa ni "Buku".

Usifanye ubahili wakati huu kwani ukimuudhi tu na akienda kusema wewe ndiye unamuuzia unga utajiunga na fiesta kule central police station.

Mpe hiyo "buku" na kama hauna japo kamkopee, maana wana hasira kwani ni lazima unga utakuwa adimu mitaani kwa trend hii ya bwana Makonda inavyoenda na arosto waliyonayo, mateja wanaweza kufanya lolote la ajabu.

Tahadhari sana. Hii siyo joke.
Umechanganyikiwa we kibibi mpaka unakosa chakuandika!!!
 
Back
Top Bottom