Tahadhari: Teja akikuomba pesa mpatie, hachelewi kukusingizia unauza madawa

Labda wewe umebahatika huna ndugu, jamaa au rafiki na pia mtaani kwenu hakuna teja.

Wengine tuna watu wetu wa karibu kabisa ambao ni mateja na hii inatuhusu sana. Kumbuka, mimi ni wa Kariakoo.

Hongera sana.

Nasikia wakimaliza zoezi la mateja wa unga wanakuja kwa mateja wa 'gomba'...huchomoki Bi Mkubwa!!
 
Jaribu tena baadae.
Nijaribu nn tena? Manake huku ndani watu niwaangaliao kwa kutumia senses zangu zote hawazidi saba , nawe ukiwa mmoja wao, ndio maana kwenye hili nimejaribu kufungua macho yangu yote lakini wapi, ila instincts zangu haziko stable, funguka basi!!!!.
 
Basi ndo mjipange nahizo buku buku sasa ila kwangu wameula wa chuya.

Ungesikia au ungezijuwa habari za athari ya mateja ungelinielewa, shukuru kuwa kwenu mmesalimika, kuna watu wanalia, watoto zao wa kuwazaa wanawashikia mapanga wanapokuwa na "arosto" na wanafungwa lakini wakitoka ni yale yale.

Hili ni balaa kubwa sana. Usiombee kukutana na teja lenye "arosto" kali.
 
Wana jamii wote tahadhari kubwa sana ichukuliwe pale teja la madawa ya kulevya (maaruf "unga") litapokuja "kukupiga mzinga" (kukuomba pesa) hususan kama tulivyowazoea omba yao kubwa ni "Buku".

Usifanye ubahili wakati huu kwani ukimuudhi tu na akienda kusema wewe ndiye unamuuzia unga utajiunga na fiesta kule central police station.

Mpe hiyo "buku" na kama hauna japo kamkopee, maana wana hasira kwani ni lazima unga utakuwa adimu mitaani kwa trend hii ya bwana Makonda inavyoenda na arosto waliyonayo, mateja wanaweza kufanya lolote la ajabu.

Tahadhari sana. Hii siyo joke.
Huu uzi wako uliuweka katika jukwaa la siasa???? Sasa hapa teja ni yupi???
 
Wana jamii wote tahadhari kubwa sana ichukuliwe pale teja la madawa ya kulevya (maaruf "unga") litapokuja "kukupiga mzinga" (kukuomba pesa) hususan kama tulivyowazoea omba yao kubwa ni "Buku".

Usifanye ubahili wakati huu kwani ukimuudhi tu na akienda kusema wewe ndiye unamuuzia unga utajiunga na fiesta kule central police station.

Mpe hiyo "buku" na kama hauna japo kamkopee, maana wana hasira kwani ni lazima unga utakuwa adimu mitaani kwa trend hii ya bwana Makonda inavyoenda na arosto waliyonayo, mateja wanaweza kufanya lolote la ajabu.

Tahadhari sana. Hii siyo joke.
Sasa bi mkubwa naomba nikuulize swali kwani nina uhakika kuwa nawewe ni mdau serikalini. Tumeaminishwa kuwa serikali ina mkono mrefu ina vyombo vingi vya ufuatiliaji 'covertly na overtly' sasa huoni kuwa unaibisha na kuidharau serikali iliyotoka wazi kulisemea jambo hilo na kuwataja wahusika bila kumung'unya maneno? Sisi huku tunajua hofu mliyonayo kwani taratibu dogo atawafikia 'kingpins' punde si punde.
 
Hahahahaa huku mtaani sasa hivi kuna kautani kanatembea mtu anakuambia ukiniudhi naenda kupeleka jina lako kwa Makonda
 
Sasa bi mkubwa naomba nikuulize swali kwani nina uhakika kuwa nawewe ni mdau serikalini. Tumeaminishwa kuwa serikali ina mkono mrefu ina vyombo vingi vya ufuatiliaji 'covertly na overtly' sasa huoni kuwa unaibisha na kuidharau serikali iliyotoka wazi kulisemea jambo hilo na kuwataja wahusika bila kumung'unya maneno? Sisi huku tunajua hofu mliyonayo kwani taratibu dogo atawafikia 'kingpins' punde si punde.

Serikali hata wewe ni mdau, hakuna raia asiye mdau wa serikali.

Polisi wakati inafanya "opereshen" huwa kuna amri maalum zinatoka, mfano "kamata vijana wote wanaokaa vijiweni muda wa kazi", basi naam waakifikia wanasoba wotem mpaka wakibaini kuwa hauna hatia unaweza kuwa umeshapoteza muda mrefu sana.

Sasa teja uliudhi na lina hasira za arosto limeshikwa linakuona wewe "nuksi", linataka ukasote tu, linaweza kufanya lolote.

Hatuombei mabaya lakini tuchukuwe tahadhari.
 
Zamani nilikuwa nakuona kama zuzu fulani na ushungi wako, lakini sasa nimekuvulia kofia. Kwa hiyo ushapanga dili na watoto wako ulioshindwa kuwalea wapite mitaani wakituomba buku na wewe ndio unakamata nafasi yako kutuandaa kutoa buku...hola!

Sitoi buku wala panya mawazo. Mwambie mwanao Dula hapa pagumu aje na maji
Haa ha haaaaaa
 
Well, kwa sasa hiyo ni issue iliyopo na zaidi ni nia, hata Kinondoni na Muhimbili wanatoa hiyo tiba. Kuwacha uteja kwanza utake mwenyewe, pil, hizi jitihada za Serikali na hususan Makonda tuziunge mkono sote.

Serikali si ya kuilamu kwa hilo, haikukufundisha uteja na inajitahidi na tunaona jitihada zilizopo.
Mimi nina wadogo zangu miteja,mmoja kaacha mmoja anaendelea kuunyonya,watoto wajirani zangu wengine wamepoteza maisha "overdose",lakini siwezi kunga mkono haya anayoyafanya Makonda

nchi lazima iwe na sheria bila sheria huwezi kuongoza nchi,haiwezekani kuwa bwana Makonda kapelekewa majina bila ya kufanya utafiti yeye kayaweka kwenye vyombo vya habari.kama kama kawaida ya polisi wetu bila ya kuyachunguza hayo majina na wamekurupuka kukamata kwasababu mkuu wa mkoa kasema,polisi mpaka hii leo wameshindwa kuwapeleka hao vijana mahakamani

Makonda amejuaje kama hayo majina ni kweli hao vijana wanauza unga,mimi naomba mkuu wa mkoa kuweka bayana wapi kayapata hayo majina,aweke bayana jina la aliyetoa hayo majina

Mimi na sapoti kauli ya Nape
 
Nijaribu nn tena? Manake huku ndani watu niwaangaliao kwa kutumia senses zangu zote hawazidi saba , nawe ukiwa mmoja wao, ndio maana kwenye hili nimejaribu kufungua macho yangu yote lakini wapi, ila instincts zangu haziko stable, funguka basi!!!!.

Huko "ndani" wapi?
 
Labda wewe umebahatika huna ndugu, jamaa au rafiki na pia mtaani kwenu hakuna teja.

Wengine tuna watu wetu wa karibu kabisa ambao ni mateja na hii inatuhusu sana. Kumbuka, mimi ni wa Kariakoo.

Hongera sana.
Nilijua tu kuwa unawaandalia mazingira ya kukusanya buku buku kwetu. Pole yako wee!
 
Serikali hata wewe ni mdau, hakuna raia asiye mdau wa serikali.

Polisi wakati inafanya "opereshen" huwa kuna amri maalum zinatoka, mfano "kamata vijana wote wanaokaa vijiweni muda wa kazi", basi naam waakifikia wanasoba wotem mpaka wakibaini kuwa hauna hatia unaweza kuwa umeshapoteza muda mrefu sana.

Sasa teja uliudhi na lina hasira za arosto limeshikwa linakuona wewe "nuksi", linataka ukasote tu, linaweza kufanya lolote.

Hatuombei mabaya lakini tuchukuwe tahadhari.
Taarifa zilizopo mtandaoni sasa hivi ni kwamba mkuu kesha mpa surport yote. Kamwambia hata kama ni Janeth, akamkamate. Mimi naona tumpe dogo tafu mpaka atakapokuja na tamko jingine.
 
Mimi nina wadogo zangu miteja,mmoja kaacha mmoja anaendelea kuunyonya,watoto wajirani zangu wengine wamepoteza maisha "overdose",lakini siwezi kunga mkono haya anayoyafanya Makonda

nchi lazima iwe na sheria bila sheria huwezi kuongoza nchi,haiwezekani kuwa bwana Makonda kapelekewa majina bila ya kufanya utafiti yeye kayaweka kwenye vyombo vya habari.kama kama kawaida ya polisi wetu bila ya kuyachunguza hayo majina na wamekurupuka kukamata kwasababu mkuu wa mkoa kasema,polisi mpaka hii leo wameshindwa kuwapeleka hao vijana mahakamani

Makonda amejuaje kama hayo majina ni kweli hao vijana wanauza unga,mimi naomba mkuu wa mkoa kuweka bayana wapi kayapata hayo majina,aweke bayana jina la aliyetoa hayo majina

Mimi na sapoti kauli ya Nape

Kuna kila namna ya "approach" kwenye mambo kama haya. Wewe kama hauungi mkono, ndiyo yapo.

Makonda anahamasisha tu lakini tayari kuna team imeundwa ya vyombo vyote vya usalama, sidhani katika hiyo "team" kama hakuna wanasheria au waliosomea sheria.

Sheria na kanuni zitafatwa.

Mimi naunga mkono na miguu hizi jitihada.
 
Kuna kila namna ya "approach" kwenye mambo kama haya. Wewe kama hauungi mkono, ndiyo yapo.

Makonda anahamasisha tu lakini tayari kuna team imeundwa ya vyombo vyote vya usalaa, sidhani katika hiyo "team" kama hakuna wanasheria au waliosomea sheria.

Sheria na kanuni zitafatwa.

Mimi naunga mkono na miguu hizi jitihada.
mimi naunga mkono na miguu pamoja na kichwa hakj za binaadamu
 
Huko ni kutojiamini kwa asilimia kubwa buku mnyime na usepe zako,kwani anakuombea chumbani huku amekufungia mpaka anakusemea umesimama hapo hapo!!

Tusinyenyekee woga jamani Watanzania kwani woga unatesa na husababisha ugonjwa wa akili na moyo.
 
Back
Top Bottom