DOKEZO Tahadhari: Unakula kuku au vibudu?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
uzuri nilipo napochukuaga kuku madori, mfugaji namjua [emoji119]

Ila kuku madori ananoga akaangwe, achomwe, makange.

Wa kienyeji asipochemshwa ipasavyo, ule ugumu wake hapana jamani [emoji1] Atabaki kuwa favorite kwenye mchemsho
IMG-20230903-WA0111.jpg
 
Naonaga hata ng'ombe akifa anapakizwa kwenye guta wanamfunika sijui wanapeleka kuzika wapi[emoji1]

Vyakula tunavyolishwa kwenye Baa, Hotelini, Migahawa nk
 
Ngoja niwasanue wananchi wenzangu

Siku hizi wilaya Bagamoyo (Mapinga, Kerege, Kiaraka), ambapo wengi wetu wafugaji wa kuku ndiyo tunafanyia ufugaji mkubwa)

Nimekuwa naona makundi ya wakina mama na vijana wamebeba ndoo alfajiri wakitokea mashambani kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi au jioni kuanzia saa 12 hadi 2 usiku.

Mwanzo nilifikiri Wanaenda kununua maziwa katika nashamba ya watu kisha wanayaleta mjini kwa ajili ya biashara

HAPANA! zile ndoo zina kuku waliokufa mabandani sasa wanaletwa mjini kwa ajili ya biashara

Ni hivi.., ukiwa mfugaji wa kuku wa nyama wengi (1000, 5000 hadi 10,000) ni kawaida sana kuingia bandani na kukuta kuku 5, 10 , 20, 30 hadi 50 wamekufa asubuhi au Jioni

Sasa utaratibu ni kwamba vijana wa kazi hawaruhusiwi kuwatupa mpaka mimi mwenye banda au meneja aje awashuhudie, awahesabu na kisha asimamie zoezi la kuwafukia kuku waliokufa

Sasa kumbe pale tunapofukia kuku waliokufa na ukiondoka tu, nyuma yake ndiyo wanaingia wale wamama wenye ndoo, wanauziwa wale kuku waliokufa Tsh 1,000 kwa kila kuku mmoja

Wanawafukua kisha wanahesabiana na kuwanunua, wale wamama wenye ndoo wanawaleta mjini kwa matumizi ya kitoweo

Wenyewe wanasema ukishaweka Kitunguu swaumu na tangawizi kujua kuku huyo alikuwa kibudu ni mpaka muuzaji akutonye la sivyo huwezi kujua

Lakini pia bei yake lazima ushtuke, kuku nusu anauzwa Tsh 3,000, kuku rangi yake nyeusi akisha kaangwa, kuku kapakwa rangi za njano au nyekundu kupoteza ishara za kuonekana ni kibudu.

Mimi au wewe huenda tumeshakula Vibudu tukifikiri ni Kuku,Tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku.
Hilo sasa ni mtihani!

"Chips kuku" halafu uwe makini!

Jambo hilo ni gumu sana kulibaini kama ilivyo vigumu ngamia kupita kwenye tundu la sindano!

"Uzuri" ni kwamba, magonjwa mengi yasababishayo vifo vya kuku, kwa binadamu hayana madhara.

Ingelikuwa kama antrax ilivyo kwa wanyama, Dar yangelibakia ni magofu kama mwendo ni huo!

Kikubwa kabla ya kuanza kufakamia misosi, tusalini sana kumuomba Mungu atuepushe na ubaya utokanao na chakula tunachokula.

Maana utakwepa ya vibudu, utakumbana na ya expired ama amira!
 
Tanzania Tupo nyuma sana nakumbuka wakati nikiwa japon, mbeba box enzi hizo, kuku wakiwa hai ni faida na hata wakiwa mfu ni faida, nakumbuka tulikuwa tunawanyonyoa kwa mashine wanaingizwa kwenye boiler wanachemshwa kiasi, wanongezewe substance na vitamin wanakaushwa then wanakatwa katika vipande ready for Dogs/cats food, baada ya kupaki kwenye mifuko, sasa huku wanafukia wajiongeze kidogo tu, chain ya ufugaji kuku hapo inaharibiwa, na chakula cha mbwa sio cheap kama unavyoweza kudhani.
 
Ngoja niwasanue wananchi wenzangu

Siku hizi wilaya Bagamoyo (Mapinga, Kerege, Kiaraka), ambapo wengi wetu wafugaji wa kuku ndiyo tunafanyia ufugaji mkubwa)

Nimekuwa naona makundi ya wakina mama na vijana wamebeba ndoo alfajiri wakitokea mashambani kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi au jioni kuanzia saa 12 hadi 2 usiku.

Mwanzo nilifikiri Wanaenda kununua maziwa katika nashamba ya watu kisha wanayaleta mjini kwa ajili ya biashara

HAPANA! zile ndoo zina kuku waliokufa mabandani sasa wanaletwa mjini kwa ajili ya biashara

Ni hivi.., ukiwa mfugaji wa kuku wa nyama wengi (1000, 5000 hadi 10,000) ni kawaida sana kuingia bandani na kukuta kuku 5, 10 , 20, 30 hadi 50 wamekufa asubuhi au Jioni

Sasa utaratibu ni kwamba vijana wa kazi hawaruhusiwi kuwatupa mpaka mimi mwenye banda au meneja aje awashuhudie, awahesabu na kisha asimamie zoezi la kuwafukia kuku waliokufa

Sasa kumbe pale tunapofukia kuku waliokufa na ukiondoka tu, nyuma yake ndiyo wanaingia wale wamama wenye ndoo, wanauziwa wale kuku waliokufa Tsh 1,000 kwa kila kuku mmoja

Wanawafukua kisha wanahesabiana na kuwanunua, wale wamama wenye ndoo wanawaleta mjini kwa matumizi ya kitoweo

Wenyewe wanasema ukishaweka Kitunguu swaumu na tangawizi kujua kuku huyo alikuwa kibudu ni mpaka muuzaji akutonye la sivyo huwezi kujua

Lakini pia bei yake lazima ushtuke, kuku nusu anauzwa Tsh 3,000, kuku rangi yake nyeusi akisha kaangwa, kuku kapakwa rangi za njano au nyekundu kupoteza ishara za kuonekana ni kibudu.

Mimi au wewe huenda tumeshakula Vibudu tukifikiri ni Kuku,Tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku.

Kwa maelezo haya nishakula kibudu mara nyingi, nini ni ushauri sasa maana umeibua tatizo tu Kaka?
 
Nimekusoma, ukila nyama una wasiwasi ni dog, kuku issue, itabisi sasa mboga iwe home tu tena za kuchinjwa.
Tena wa kuchinjiwa uwe unaona maana kule unakonunua ukampa akuchinjie anaweza bado kukubadilishia ukapewa kibudu
 
Back
Top Bottom