Tahadhari ya Tishio la Usalama wa Fedha Mtandaoni – Udhaifu wa Usalama Katika Apps za Kifedha kama M-Pesa Tanzania

Joined
Sep 10, 2023
Posts
55
Reaction score
104
Katika ulimwengu wa sasa wa kidijitali, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi zimekuwa mkombozi mkubwa kwa watu wengi. Applikesheni kama M-Pesa zimeleta urahisi wa kufanya miamala, kulipia bili, kutuma na kupokea pesa, kwa haraka na salama — angalau ndivyo inavyotarajiwa. Hata hivyo, kuna udhaifu wa kiusalama (vulnerability) unaotishia usalama wa watumiaji wengi, hasa nchini Tanzania, ambao wengi bado hawajafahamu au kuchukulia kwa uzito unaostahili.

Udhaifu: Akaunti Moja, Simu Nyingi
Moja ya mapungufu makubwa ya kiusalama yaliyopo kwenye baadhi ya applikesheni za kifedha kama M-Pesa ni uwezekano wa akaunti moja kufunguliwa (login) kwenye simu mbili au zaidi kwa wakati mmoja bila kizuizi au taarifa yoyote kutumwa kwa mmiliki halali. Hii inamaanisha kuwa mtu akipata nywila (password) yako — iwe kwa njia ya ulaghai (phishing), uvujaji wa data, au kutumia namba zako zilizohifadhiwa vibaya — anaweza kufungua akaunti yako ya M-Pesa kwenye simu yake na kuendelea kufanya miamala kama vile ndiye mmiliki.
Jambo la kushangaza na kusikitisha ni kwamba hata pale ambapo mtumiaji anagundua kuwa akaunti yake ya M-Pesa imedukuliwa au inatumika kwenye kifaa kingine bila ruhusa, watoa huduma wa M-Pesa hawawezi kutoa msaada wa haraka au wa moja kwa moja kumsaidia.
Katika hali ya kawaida, mtu anapopiga huduma kwa wateja akilalamikia shughuli zisizoeleweka au kuingia kwa kifaa kisichojulikana, matarajio ni kuwa:
  • Akaunti yake ifungiwe mara moja (temporary lock),
  • Vipengele vyote vya kuingia vifutwe (force logout),
Tatizo linakuwa kubwa zaidi kwa sababu:
  • Hakuna njia ya “Log out all devices” kama inavyopatikana kwenye huduma kama WhatsApp, Gmail au Facebook. Hii inampa mwizi uhuru wa kuendelea kutumia akaunti yako kwa muda mrefu bila wewe kujua.
  • Hakuna notisi (notification) ya usajili wa kifaa kipya kwa baadhi ya applikesheni hizi. Hii inamaanisha mtumiaji halisi hatajua kuwa kuna kifaa kingine kimeingia.
  • Kufuta au kubadili nywila hakusaidii, kwani baadhi ya apps haziwazuii walioko kwenye session ya awali kuendelea kutumia mpaka wafungwe kwa mkono, jambo ambalo halipo kwa sasa.
Njia za Wizi Zinazotumika

Wezi wa mtandaoni hutumia mbinu mbalimbali kupata nywila za watu, kama vile:
  • Kutuma SMS au WhatsApp zenye viungo vya ulaghai (phishing links) zinazofanana na tovuti halali.
  • Kupiga simu wakijifanya maofisa wa huduma kwa wateja na kuomba taarifa nyeti.
  • Kutumia malware au apps bandia zinazodukua taarifa za kifaa.
  • Kupata taarifa zako kupitia watu wa karibu (mfano, familia au marafiki) kwa sababu ya uaminifu wa kupindukia
Ushauri Kwa Makampuni ya Huduma za Kifedha.

Ni muhimu kwa makampuni kama Vodacom Tanzania (M-Pesa) na mengineyo kuhakikisha kuwa applikesheni zao zinakuwa na vipengele vya msingi vya kiusalama, ikiwemo:
  • Tarifa ya kuingia kwa kifaa kipya (new device login alert).
  • Chaguo la “log out all devices”, kwa hali ya dharura.
  • Kufunga kifaa kingine moja kwa moja pindi nywila inapobadilishwa.
  • Kutumia biometric login (alama ya kidole/uso) kama chaguo la usalama zaidi.
 
Kwa hiyo mkuu MTU anaweza ku login mpesa kama ana login sport pesa 🤔.

Mwanzoni zilikuwa vizuri TU, ila naona wamepunguza security measures. Ili sijui kupata wateja wengi

Nmb wako makini sana , kiasi cha kwamba phone Yako ikiwa developer mode, huwezi ku instain nmb app, mpaka u disable developer feature.
 
Mfano mtu akapata access ya sim yako,akapata na zile security code akalogin kwa simu yake,wewe hata ujue hutoweza kumtoa anaweza fanya chochote.
 
Mi mbona mpesa yangu nisipokuws na line kwenye simu haifunguki?
 
Kwa hiyo mkuu MTU anaweza ku login mpesa kama ana login sport pesa 🤔.

Mwanzoni zilikuwa vizuri TU, ila naona wamepunguza security measures. Ili sijui kupata wateja wengi

Nmb wako makini sana , kiasi cha kwamba phone Yako ikiwa developer mode, huwezi ku instain nmb app, mpaka u disable developer feature.
KWA MFANO WEWE UMEWEZA KULOGIN?

NA BAADA YA KUFANYA HIVYO UMEPATA NINI?
 
Ni kweli ila kwa mara ya kwanza unapofanya setup lazima uwe laini ya simu iwe kwenye simu husika ila baadaye haicheki tena.
Kwanza unaposema kulogout unamanisha nini kwa sababu Ile pini unaingiza kila unapofungua app ya Mpesa. Hivyo hakuna wakati unajikuta umelogin tu bila kuweka pini yako.

Kwangu mimi naona iko sawa sihitaji kuwa na laini kwenye simu hiyohiyo
 
Haha wewe Bado hauja muelewa mleta mada.
Je umejaribu kuweka laini ya voda ya MTU mwingine kwenye SIM Yako na ukaoma mpesa haifanyi kazi.

Naomba majibu tafadhali
Mkuu kupitia ujumbe wako umenifanya niende kutest maana hapa nina line 2 za voda kwenye simu, moja haina majina yangu.

Mkuu nimepiga test nimeona inapiga kazi.

Niwe mkweli nimeshtuka, maana kuna siku nilitaka kutumia app lakini laini yake ilikuwa kwenye kitochi iligoma --- hapa ndo nikipofanya conclution.

Hapa nimefanya random test mapa flight mode na kutoa laini zote app inapiga kazi. --- na wamenipiga lock ya dakika 60

JApo inataka password kabla ya kuingia
 
Ni kweli ila kwa mara ya kwanza unapofanya setup lazima uwe laini ya simu iwe kwenye simu husika ila baadaye haicheki tena.
Kwanza unaposema kulogout unamanisha nini kwa sababu Ile pini unaingiza kila unapofungua app ya Mpesa. Hivyo hakuna wakati unajikuta umelogin tu bila kuweka pini yako.

Kwangu mimi naona iko sawa sihitaji kuwa na laini kwenye simu hiyohiyo
Mkuu,
Anachomaanisha mtoa mada ni kwamba, hata mimi nikiwa na password zako naweza ku login in kwa kutumia App kwenye simu nyingine na wewe usipate taarifa
 
Yeah
 
Scenario hii hii inatumika Facebook, Instagram na kwingine kote, tofauti ni namna ambavyo app zina verify.

Voda INAVERIFY kwa kuwa na sim card ndani ya KIFAA ili uingie kwenye account unaingiza pin, fb , insta nayo Wana njia za kuverfy kama verification code.

Sasa tofauti ni nini hapo sababu wote wanaverify.

Swala la wewe kuibiwa loini ni uzembe wako au kupoteza laini, ukipoteza laini nenda karipoti watakusaidia kuiblock lakini hiyo sio kosa lao ni lako mteja.

Hivyo mtu anaelalamikia kwamba kaibiwa laini na pesa kakuta hazimo unadhani hiyo kesi kisheria unashinda?

Hivyo kupoteza line na nywila za mteja zikatumiwa kwingine ni uzembe wake.

Ni sawa na fb kumpa code mtu usiemjua na anajua email Yako lazima AINGIE.
 
Otp utapata wapi?
Kwa mfano,
Nimekuamba simu yako, then nikatumia creditials zako kuingia kwenye App ya M PESA iliyopo kwenye simu yangu, OTP zikituma nazicheki na naingiza kwenye App ya simu yangu.. namalizia installation, then nakurudishia simu, from there hautaweza kugundua kama kuna mimi ambaye natumia akaunti yako ya M PESA kwenye simu yangu
 
Mkuu,
Anachomaanisha mtoa mada ni kwamba, hata mimi nikiwa na password zako naweza ku login in kwa kutumia App kwenye simu nyingine na wewe usipate taarifa
Sasa hapo ukibadilisha password hataweza tena ikiwa password inakuwa ileile miaka na miaka hapo ni changamoto...
Password inafaa ubalishe kila baada ya mwezi ikiwa ni sehemu sensitive
 
Back
Top Bottom