Tahadhari ya Tishio la Usalama wa Fedha Mtandaoni – Udhaifu wa Usalama Katika Apps za Kifedha kama M-Pesa Tanzania

Tahadhari ya Tishio la Usalama wa Fedha Mtandaoni – Udhaifu wa Usalama Katika Apps za Kifedha kama M-Pesa Tanzania

Kwa mfano,
Nimekuamba simu yako, then nikatumia creditials zako kuingia kwenye App ya M PESA iliyopo kwenye simu yangu, OTP zikituma nazicheki na naingiza kwenye App ya simu yangu.. namalizia installation, then nakurudishia simu, from there hautaweza kugundua kama kuna mimi ambaye natumia akaunti yako ya M PESA kwenye simu yangu
Mpesa wanatumia otp kivipi , okay assume umechukua laini ya mtu na kufanya hivyo




Hilo ni kosa la uzembe la mteja huwezi lalama


Kwani fb au insta huwezi fanya hivyo?
 
TOFAUTISHA UZEMBE WA MTEJA NA UDHAIFU WA APP, HIZI MADA ZA CHAT GPT
 
Kwa mfano,
Nimekuamba simu yako, then nikatumia creditials zako kuingia kwenye App ya M PESA iliyopo kwenye simu yangu, OTP zikituma nazicheki na naingiza kwenye App ya simu yangu.. namalizia installation, then nakurudishia simu, from there hautaweza kugundua kama kuna mimi ambaye natumia akaunti yako ya M PESA kwenye simu yangu
MAmbo ya kupeana password haya
 
Inawezekana kabisa Mkuu ku login kwenye App ya M PESA kama hauna line,
Mfano mimi nime link line yangu ya Lipa Namba kwenye App, na line hata sijui ilipo, ila miamala nafanya kama kawaida
Kwa mfano hapa shida ni nini? Unadhani Kuna UDHAIFU wowote? Si tayari ushaingia uninstall hiyo app alafu install tena kisha jaribu
 
Huwezi kulogin kwenye App mara ya kwanza(Simu nyingine) bila laini kuwepo ndani ya simu husika. Mitandao yote ya Yas, Vodacom na Airtel.

Halotel huwezi kufanya muamala kwenye App bila OTP.

App zina usalama wa kutosha kinachobaki ni ujinga wa mtu mmojammoja
 
Kwa mfano,
Nimekuamba simu yako, then nikatumia creditials zako kuingia kwenye App ya M PESA iliyopo kwenye simu yangu, OTP zikituma nazicheki na naingiza kwenye App ya simu yangu.. namalizia installation, then nakurudishia simu, from there hautaweza kugundua kama kuna mimi ambaye natumia akaunti yako ya M PESA kwenye simu yangu
Meseji ya transaction hupati😳😳
Vip kuhusu ATM card
 
Sasa mkuu hata ukipata itasaidia nini na umeshaibiwa!??
Sasa mbona umesema sipati taarifa..
Vip kuhusu ATM card na password
Maana pia ukisharuhusu popote mtu apate password hauko salama..

Mpesa so far wapo vizuri kuliko kampuni zote za simu
 
Nilijiongezaga kuchimbia ka HELA ndani nimwendo WA kudroo TU bila SHIDA HII nchi haieleweki muda wowte kinahappen
 
Katika ulimwengu wa sasa wa kidijitali, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi zimekuwa mkombozi mkubwa kwa watu wengi. Applikesheni kama M-Pesa zimeleta urahisi wa kufanya miamala, kulipia bili, kutuma na kupokea pesa, kwa haraka na salama — angalau ndivyo inavyotarajiwa. Hata hivyo, kuna udhaifu wa kiusalama (vulnerability) unaotishia usalama wa watumiaji wengi, hasa nchini Tanzania, ambao wengi bado hawajafahamu au kuchukulia kwa uzito unaostahili.

Udhaifu: Akaunti Moja, Simu Nyingi
Moja ya mapungufu makubwa ya kiusalama yaliyopo kwenye baadhi ya applikesheni za kifedha kama M-Pesa ni uwezekano wa akaunti moja kufunguliwa (login) kwenye simu mbili au zaidi kwa wakati mmoja bila kizuizi au taarifa yoyote kutumwa kwa mmiliki halali. Hii inamaanisha kuwa mtu akipata nywila (password) yako — iwe kwa njia ya ulaghai (phishing), uvujaji wa data, au kutumia namba zako zilizohifadhiwa vibaya — anaweza kufungua akaunti yako ya M-Pesa kwenye simu yake na kuendelea kufanya miamala kama vile ndiye mmiliki.
Jambo la kushangaza na kusikitisha ni kwamba hata pale ambapo mtumiaji anagundua kuwa akaunti yake ya M-Pesa imedukuliwa au inatumika kwenye kifaa kingine bila ruhusa, watoa huduma wa M-Pesa hawawezi kutoa msaada wa haraka au wa moja kwa moja kumsaidia.
Katika hali ya kawaida, mtu anapopiga huduma kwa wateja akilalamikia shughuli zisizoeleweka au kuingia kwa kifaa kisichojulikana, matarajio ni kuwa:
  • Akaunti yake ifungiwe mara moja (temporary lock),
  • Vipengele vyote vya kuingia vifutwe (force logout),
Tatizo linakuwa kubwa zaidi kwa sababu:
  • Hakuna njia ya “Log out all devices” kama inavyopatikana kwenye huduma kama WhatsApp, Gmail au Facebook. Hii inampa mwizi uhuru wa kuendelea kutumia akaunti yako kwa muda mrefu bila wewe kujua.
  • Hakuna notisi (notification) ya usajili wa kifaa kipya kwa baadhi ya applikesheni hizi. Hii inamaanisha mtumiaji halisi hatajua kuwa kuna kifaa kingine kimeingia.
  • Kufuta au kubadili nywila hakusaidii, kwani baadhi ya apps haziwazuii walioko kwenye session ya awali kuendelea kutumia mpaka wafungwe kwa mkono, jambo ambalo halipo kwa sasa.
Njia za Wizi Zinazotumika

Wezi wa mtandaoni hutumia mbinu mbalimbali kupata nywila za watu, kama vile:
  • Kutuma SMS au WhatsApp zenye viungo vya ulaghai (phishing links) zinazofanana na tovuti halali.
  • Kupiga simu wakijifanya maofisa wa huduma kwa wateja na kuomba taarifa nyeti.
  • Kutumia malware au apps bandia zinazodukua taarifa za kifaa.
  • Kupata taarifa zako kupitia watu wa karibu (mfano, familia au marafiki) kwa sababu ya uaminifu wa kupindukia
Ushauri Kwa Makampuni ya Huduma za Kifedha.

Ni muhimu kwa makampuni kama Vodacom Tanzania (M-Pesa) na mengineyo kuhakikisha kuwa applikesheni zao zinakuwa na vipengele vya msingi vya kiusalama, ikiwemo:
  • Tarifa ya kuingia kwa kifaa kipya (new device login alert).
  • Chaguo la “log out all devices”, kwa hali ya dharura.
  • Kufunga kifaa kingine moja kwa moja pindi nywila inapobadilishwa.
  • Kutumia biometric login (alama ya kidole/uso) kama chaguo la usalama zaidi.
Unayosema ni kweli.kama hakuna notification ya access ya account yako kwa device nyingine hiyo ni major control failure.Sasa hiv naona kwa voda kama Nida yako ikitumika kusajili line nyingine wewe unapata notification mpaka namba ya nida ya yule aliye sajili.nadhani pia wangeongeza uwe unaweza kuapprove hiyo regiatration kabla haijakamilika. unapata tuu ujumbe ila process inaendelea.so kama ni mharifu anaweza fanya uharifu kabla wewe huja fanya mawasiliano ya kublock no.

Naona airtel wamejitahidi.unaporegister kwa device nyingine unapata otp code unayotumiwa kwenye namba yako ili kuhakiki

Take way

Wanapoendelea kuimarisha kudigitalize finances.ni vizuri pia kuimarisha ma swcurity
 
Binafsi naona security ipo kwasababu zifutazo.
1. Unapoinstall kwa mara ya kwanza lazima itakuomba password na otp pia itatumwa kwenye line ya mhusika tena baadhi ya mitandao kama airtel lazima line husika iwepo kwenye simu kwa mara ya kwanza na pia hawataki utumie wifi (kama sijakosea) kwa hiyo mpaka hapo mtu utakuwa ni uzembe wa mhusika na siyo udhaifu wa app
2. Unapoingia kwenye app baada ya kuinstall ni lazima uweke password ya akaunti husika. Hivyo hapa ni uzembe wa mtu kutoa password kwa asiyehusika.
3. Message za miamala zinatumwa kwenye line ya mhusika hivyo ni rahisi kuzuia kwa yy kubadilisha password(siyo lazima apige customer care kuomba msaada) na kumbuka kama mhusika atabadilisha password kwenye app hutaweza kutumia hata kama hiyo app unayo.
 
Back
Top Bottom