TAHAJUDI (Meditation): Mbinu, faida, aina na mambo ya kuzingatia

 
Asante sana Mtambuzi haya ndio mambo yanatakiwa kupostiwa humu jamvini mtu unasoma unaelimika.safi sana nilikuwa nasikia tu hizi habar leo kupitia kwako nimetambua kwa kirefu zaidi.
 

Lifehacker, Pasco,Mtambuzi:
utafiti binafsi niliowahi kuufanya kuhusiana na na meditation ni kuwa hii ni imani kama imani nyingine. Mwanzo unapojiunga ..utaanza vyote..yaani unachanganya dini yako na meditation kwa pamoja ila baadaye utaacha Dini yako na kuwa mtu wa meditation forever.

KINACHOFANYIKA NI NINI HASA?
kwa mtu kufanya meditationa hujikuta akijenga connection na Evil Spirits zilizopo kwenye other world dimension ambazo zinam-deceive kupitia information wanazompa. Hizi spirit sio za kimungu bali ni Demons na baada ya muda, mtu huyu anaye-meditate ataanza kuhisi kuwa na ujuzi ama uelewa kuhusu Mungu aliyedhani yupo vile kupitia dini yake na kuona kumbe hakuwa anaambiwa ukweli.

Mfano : Dini zetu zinafundisha kuhusu shetani na Mungu, lakini wenye kuingia kwenye hizi meditation wana mtazamo tofauti, na pia hawaamini uwepo wa jehanum wala hoja ya kuwa kutakuja kuwa na siku za mwisho mungu kuja kuhukumu ulimwengu.
Ninao marafiki zangu walikuwa wakatoliki wazuri sana, yaani sana* lakini mwishowe hawaendi tena kanisani. Kwani wanaona wenye kuamini Mungu ni wajinga fualni ama wasiojitambua ama wasioelewa ukweli ulivyo. Na sio tu wakatoliki hii imani haichagui dini wala dhehebu, yeyote atakayeingia ataachana na imani yake, hapo baadaye.

Nina rafiki yangu mmoja alishanieleza sababu za kwanini Wazungu wengi siku hizi wanaacha Ukristo wala kwenda kanisani; akasema ukiingia kwenye hii imani utaweza kugundua ukweli wa Dini zote duniani.Yaani meditation inakufanya uweze kujua ukweli wa Dini zote na mwisho unachagua kuishi kawaida bila ya Dini.
Something interesting ni kuwa Hizi jamii za wanaomeditate zinaviongozi wao ambao wanafundisha mambo ya kiimani yanayoweza kumwimarisha mtu kuendelea kuwa ndani ya jumuiya zao yakiwemo machapisho mbalimbali, kama ambavyo waumini wa dini yeyote wanavyopewa mafundisho zinavyofundisha mtu aendelee kushika dini,
Mfano: wao wanaaamini kuwa binadamu anayo miili saba kitu ambacho nadhani kipo against bible.
mambo mengine ni kama Mungu hayuko mahali pote... Mungu hachukui hatua katika maisha ya mtu: bali juhudi zake mwenyewe n.k.
Haya Mambo ni kinyume na mafundisho ya ukristo.Na wahindu ndio wanayafiki sana haya mambo lakini ukiwafuatilia ndio jamii ya wachawi wakubwa duniani wanaoabudu hadi majoka.kitu ambacho wengi hawajafutilia ni kuwa ukiweka kinyagochochote ndani ya nyumba yako ukaanza kukiabudu baada ya muda utaanza kuona matokeo positive.Hizi ni roho za kishetani zinazozunguka kudanganya. That's why nilisema this is a cult.
Na kwakuongeza ni kuwa jamii hizi zina watu wasomi sana hadi ngazi za doctorate ( PHD). Hivyo sio jamii za wahuni, na pia kuna lugha kama mantra, chakra n.k.

Yesu alisema tumwombe yeye, hakusema tuzitegemee meditation: kwahiyo pasco, ni swala la kuamua aina gani ya stori inayokuvutia.
I timotheo 4: Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani
LUka 18:8Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?
 

Hv kumbe rozari ni implementation ya wanadamu eeh? vp na kuhusu mambo ya ubani yale, mambo magumu kwel haya
 
Last edited by a moderator:

Pasco lakini mbona husemi ni wapi pameandikwa kuwa Yesu alifanya meditation?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mwaka jana, wapi Yesu alisema tumwombe yeye?!. Nijuavyo mimi Yesu alisema, chochote mtakachoomba kwa Baba yangu, kupitia kwangu, mtapewa!.

Pasco
 
Hv kumbe rozari ni implementation ya wanadamu eeh? vp na kuhusu mambo ya ubani yale, mambo magumu kwel haya
ibada za ubani na chetezo zina asili ya muundo wa kuabudu uliofanywa na makuhani wa kiisraeli. wakatoliki waka-adopt huo mfumo. angalia unapoenda usipindishe mada mkuu.
 
Mkuu mwaka jana, wapi Yesu alisema tumwombe yeye?!. Nijuavyo mimi Yesu alisema, chochote mtakachoomba kwa Baba yangu, kupitia kwangu, mtapewa!.

Pasco
ha ha ha Pasco hujakosea, lakini yesu na Mungu is inseparable
zingatia red: color

Yohana 14-17
14:Yesu akawaambia, "Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia............
[SUP]2 [/SUP]Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. [SUP]3 [/SUP]Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. [SUP]...

[/SUP] [SUP]..........6 [/SUP]Yesu akawaam bia, "Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.


[SUP]8 [/SUP]Filipo akamwambia Yesu, "Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika." [SUP]9 [/SUP]Yesu akamjibu, "Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu?

........[SUP]10 [/SUP]Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu?
....... [SUP]12 [/SUP]Ninawaambia hakika, mtu ye yote akiniamini ataweza kufanya miujiza kama hii na hata zaidi, kwa kuwa mimi ninakwenda kwa Baba yangu.
[SUP]13 [/SUP]Kitu cho chote mtakachoomba kwa jina langu, nitawafanyia, ili Baba yangu apate kutukuzwa kwa yale ambayo mimi Mwanae nitawafanyia. [SUP]14 [/SUP]Mkiniomba cho chote kwa jina langu nitawafanyia."

[SUP]15[/SUP]"Kama mnanipenda mtatimiza amri zangu.....
[SUP]
1 [/SUP]Mtu anayezishika amri zangu na kuziti miza ndiye anayenipenda. Na mtu anayenipenda, Baba yangu atam penda; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake." [SUP]22 [/SUP]Yuda, siyo Iskariote, akamwuliza, "Bwana, itakuwaje ujidhihirishe kwetu ,,,,,,,,,,,.

[SUP]24 [/SUP]Mpaka sasa hamjaomba lo lote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapewa ili furaha yenu ipate kukamilika.



 
Pasco , ukiangalia Logic wise huwezi tu kumjua Mungu ama kuufahamu ukweli kuhusu mungu ama jambo lolote kupitia kukaa kimya siku nzima umekodolea mimacho kwenye nukta nyeusi. Something gotta be wrong in medulla. Ujuzi unatokana na Kutenda na Experience. That is why meditation bado itaendelea kuwa ni Cult.
Kila aina ya uchawi una-principle zake za kuu-apply na ku-comunicate nao.Sio lazima wote tuvae hirizi.

Baibo imeweka wazi kuwa siku za mwisho watu wataacha imani wakisikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya Mashetani
kwenye meditation kuna mambo mawili
1= kukaa na kusikiliza
(communicate) hizi roho(Spirits): bila kutafuna maneno hiki ndio chanzo kikuu cha knowledge za waumini, wanazotumia kuwashawishi wengine wajiunge.
2= kupata mafundisho ambayo ni (Anti God teachings)

baibo imeweka wazi kila Roho isiyomkiri YYesu haitokani na Mungu.

lifeHacker, Mtambuzi na
CC: warumi, Samaritan, Majimoto, Himidini, Ablessed, everlenk, LORDVILLE
 
Hii mada ni ngumu na ina pande nyingi sana zinazohitaji tafakurh jadidi, mimi ningependa kuchambua kipengele kimoja tuu cha meditation kuunganishwa na dunia ya mashetani na roho zisizoonekana! Kama kuna kitu ambacho kina nguvu mno basi ni ubongo/ufahamu wa mwanadamu na kwasababu ya imani yetu kwa mungu mmoja huwa tunakuwa na ukomo kwenye mambo karibia yote, na hivyo kufanya ufahamu wetu,conscious mind kutumika kidogo mno kwa sababu ya limitations za imani zetu. Meditation inavunja hiyo mipaka na kuufumua ufahamu wetu kwa kuukusanya pamoja toka ulimwengu wa kutangatanga na kuuweka pamoja huku ukifocus kwenye jambo moja husika na kwa wakati husika, ukifanikiwa katika hili unakuwa umedevelop kitu kiitwacho supernatural powers kwakuwa sasa conscious mind yako iko single n focused! Stage hii unakuwa na uwezo wa kufanya chochote ambacho binadamu wa kawaida hawezi na ndipo hapo meditation huhusishwa na nguvu za giza
 

Huwa najiuliza mara 2 2! inakuwaje mimi sitajwi katika cc? nimewai kuuliza hili hapa lkn sijawahi kupata jibu halisi! Mimi nikahisi labda wanaotoa cc hawana muda wa kutosha, wana haraka zao, na hivo wanawa-cc watu wachache sana! Ona sasa hapa, Mtambuzi amewa-cc wanaJF 50, hii inaonyesha namna gani humu watu wabaguzi!

Kwa kuwa sijawai kupewa cc, na huenda mnadhani mimi ROBOT, sifai kupewa cc, natangaza rasmi humu, ole wake mwanaJF atakaeeni-cc wakati huu wa ubaguzi!

BTW, hongera Mtambuzi, umenipa bonge la darasa!
 

....CC slim5
 

hii mada kweli ni ngumu ila em ongeza nyama kdogo apo kwenye meditation na supernatural,,
af hyo supernatural ina uthibitisho wowwote wa kisayansi??
 
hii mada kweli ni ngumu ila em ongeza nyama kdogo apo kwenye meditation na supernatural,,
af hyo supernatural ina uthibitisho wowwote wa kisayansi??

meditation is real! Hata kabla ya kutafuta ithibati za kisayansi naomba wewe mwenyewe ujaribu japo kwa wiki moja tu
 
meditation is real! Hata kabla ya kutafuta ithibati za kisayansi naomba wewe mwenyewe ujaribu japo kwa wiki moja tu

kaka mi nshajaribu nkasanda, kwanza huku nakokaa makelele 24/7 so eneo la kufanyia ni changamoto kwangu, labda unipe uzoefu wako bro
 
kaka mi nshajaribu nkasanda, kwanza huku nakokaa makelele 24/7 so eneo la kufanyia ni changamoto kwangu, labda unipe uzoefu wako bro

kama uko free on weekends na kama upo dar tunaweza kuorganise meditation retreat session na wengine watakaopenda mahali popote nje ya mji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…