Taharuki: Mtanzania diaspora atekwa nyara Kilimanjaro

Uzuri [au ubaya] wa hayo uliyoyaelezea ni kwamba yana apply hata kwa Watanzania waliopo Tanzania.
 
Nimekwambia weka sheria tusiongee kwa kukariri, weka sheria hapa tuichambue acha longolongo.

Hakuna sheria inayosema vyombo vya usalama vitatathmini na kuamua maandamano yafanyike au yasifanyije. Huo ni ujinga mnaokaririshana tu hakuna sheria hiyo.

Hakuna sheria hiyo.

Kama unasema ipo iweke hapa tuisome.
 
Uzuri [au ubaya] wa hayo uliyoyaelezea ni kwamba yana apply hata kwa Watanzania waliopo Tanzania.
Ni kweli na hiyo ni "crackdown" yaani msako unosaidiwa na Social Media, media outlets na vyanzo vingine.

Kwa mfano mzee Mwandambo kukamatwa kwake ni "videos" zinotumwa YouTube na mwenye hiyo video huonyesha mshangao kama vile kusema, "Maa wee mzee Clemence Mwandambo haogopi?" Amchana raisi Samia au afanya vile.

Hiyo video ikiangaliwa na task force what next? ni kumtafuta mzee Mwandambo popote alipo au wengine wote waliopo Tanzania. Nina wasiwasi pia kwamba kale kasichana kalikokuwa kasiisema CCM kwa kutoa baiskeli kama bado yupo hai.

Hivyo kinofanyika sasa hivi ni "Crackdown" au msako hivyo waenda kotekote.

Nimetoa mfano wa Syria kwasababu mwaka 2011 kama wakumbuka kulikuwa na Arab Spring ambayo ilifeli kwa Syria lakini baada ya hapo kulianza kufanywa msako mkali wa kuwatafuta wale waloandamana na walokuwa wakiandaa.

Weye fikiria tokea 2011 hadi 2022 wasyria wapatao 580,000 waliuliwa na vikosi na chinjachinja wa Assad. Kati ya hao watu 380, 000 hawakuwa ni washika silaha, hiyo ni idadi kubwa jamaa aliua raia wake ndai ya miaka 11.

Hivyo ni kweli wanokamatwa ni wale wa humohumo Tanzania lakini hii "Crackdown" yahusu kila aneshukiwa au gunduliwa azungumza yasosifia kwenye Social Media.

Hii ni hatari sana.
 
Kitu chochote kinapo fanyika bila kufuata utaratibu kina geuka na kuwa uharifu.
Ww ukijipa uhalali wa kufanya uharibifu kwa kisingizio cha kudai haki basi jua na serikali itajipa haki ya kukufanya chochote kwa kisingingizio cha kudhibiti uharifu.
 
Kitu chochote kinapo fanyika bila kufuata utaratibu kina geuka na kuwa uharifu.
Ww ukijipa uhalali wa kufanya uharibifu kwa kisingizio cha kudai haki basi jua na serikali itajipa haki ya kukufanya chochote kwa kisingingizio cha kudhibiti uharifu.
Sawa.

Ndiyo maana tuna sheria. Na wewe umesema habari ya sheria.

Umesema maandamano yana utaratibu wake, watu wapeleke taarifa vyombo vya usalama, vyombo vya usalama vipitie taarifa na kuruhusu au kukataza maandamano hayo.

Sasa mimi kwa sababu nafuata taratibu za mijadala, taratibu za uhakiki, na nimeelewa hoja yako ya vitu vifanyike kwa utaratibu, nimekutaka uweke hiyo sheria hapa tuihakiki inachosema na ulichoandika wewe kama ni sawa.

Isije kuwa umekariri mambo ambayo hayapo katika sheria.

Mpaka sasa hujaiweka hiyo sheria.

Unatuweka mambo uliyokariri tu, kimakosa.

Nakwambia hakuna sheria ya vyombo vya usalama kukataa maandamano.

Hii ni haki ya kikatiba.

Kama unabisha weka hiyo sheria tuichambue.
 
Mafwele kanunua ugomvi na Trump, tulimwambia diaspora hasa wa USA ni chambo asiwaguse, ona sasa!
Acha ubwege!! Trump hawezi kuhangaika na mtu mweusi, hata kama ana uraia wa Marekani.

Kwanza anafurahi anapoona mhamiaji HARAMU kutoka Africa amekamatiwa Africa
 
Watu kufanya fujo katika maandamano hakuondoi haki ya kikatiba ya watu kuandamana. Na kuna watu wengi wameandamana bila fujo.

Kwa nini unashindwa kutenganisha mambo?
.Sheria ya Jeshi la Polisi (Police Force and Auxiliary Services Act) haisemi unapaswa kuomba "Kibali" (Permission), bali inataka utoe "Taarifa" (Notice). Unapaswa kutoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) saa 48 kabla ya maandamano.

Kisheria, kazi ya polisi ni kutoa ulinzi kwa waandamanaji na siyo kuzuia, isipokuwa tu kama kuna ushahidi wa wazi kuwa maandamano hayo yataleta uvunjifu wa amani

Je kuna waandamanaji wowote waiotoa taarifa kwa OCD yeyote nchini masaa 48 kabla ya tarehe 29/10?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…