TAHURI: Tumuunge mkono Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona

Weka kwanza takwimu za Corona nchini Tanzania.
Wagonjwa wangapi vifo vingapi.
Kujitoa ufahamu hakujawahi kuwa solution ya Tatizo,mwambie Jamaa yako aache kujificha arudi mjini,mwanaume hakimbiagi matatizo
 
Hii inaitwa 'rationalisation'. Labda kama TAHURI wangekuja na utafiti kuonyesha kuwa wamegundua dawa ambayo ni mbadala wa hiyo chanjo au bado wanaendelea nao. Lakini 'maneno matupu hayavunji mfupa'.
KWani wewe una tatizo la corona au unalisikia redioni na TV , sasa unataka dawa? Wafie mbali huko!

In 1996, an outbreak of measles, cholera, and bacterial meningitis occurred in Nigeria. Pfizer representatives and personnel from a contract research organization (CRO) traveled to Kano to set up a clinical trial and administer an experimental antibiotic, trovafloxacin, to approximately 200 children. Local Kano officials reported that more than 50 children died in the experiment, while many others developed mental and physical deformities. The nature and frequency of both fatalities and other adverse outcomes were similar to those historically found among pediatric patients treated for meningitis in sub-Saharan Africa.[173] In 2001, families of the children, as well as the governments of Kano and Nigeria, filed lawsuits regarding the treatment. According to the news program Democracy Now!, "[r]esearchers did not obtain signed consent forms, and medical personnel said Pfizer did not tell parents their children were getting the experimental drug." The lawsuits also accuse Pfizer of using the outbreak to perform unapproved human testing, as well as allegedly under-dosing a control group being treated with traditional antibiotics in order to skew the results of the trial in favor of Trovan. While the specific facts of the case remain in dispute, both Nigerian medical personnel and at least one Pfizer physician have stated that the trial was conducted without regulatory approval.

Source: Pfizer - Wikipedia
 
Ngetti njoo utueleze ukweli ukoje.
Magufuli aliongelea ubaya wa chanjo na kwamba zina athari kwa kwa binadamu. Akasema Wazungu hawana nia njema na kama wangekuwa na nia njema wangeshaleta chanjo ya TB, Malaria, Kipindupindu na Kansa. Akasisitiza kwa kuna nchi wasichana wake wa miaka 14 walipewa chanjo ya kansa ya kizazi mpaka Leo ni Wagumba.
Hakuna mahali popote alipoongelea gharama za chanjo ya Covid19 kuwa kubwa. Wewe haya ya trillion 11 kuwa sababu ya nchi kukataa chanjo umeyatoa wapi? Mbona mpaka sasa mnalipisha wagonjwa wa Corona zaidi ya mil.10 kwenye hospitali binafsi na hamuwakemei wamiliki? Unajua gharama ya chanjo hizo mpaka kukamilika ni kiasi gani?
Unaposema tiba ni rahisi kuliko chanjo unatumia kigezo gani? Unapokinga watu uanazuia watu kuugua, hivyo hakutakuwa na gharama za tiba. Chanjo ya Ndui inatolewa mara moja kwa kila Mtanzania mara tu azaliwapo, Je ingekuwa gharama kiasi gani kumtibu Mtanzania mmoja anayeugua Ndui hata mara 10 tu maisha yake yote? Na tungekuwa na uhakika kiasi gani kama tiba inaokoa maisha kwa 100%? Malaria ina tiba na Watanzania wanakufa na tiba ipo, itakuwaje kwa Corona ambayo Leo mnaomba tiba badala ya Chanjo kwa kisingizio cha gharama?
Linapokuja suala la kununua ndege za Masifa mnasema tutanunua kwa gharama yoyote, lakini kwenye uhai wa Watanzania mnaona ni gharama kubwa?
 
Hawa wengine ni waganga njaa tu.
Wanatumia fursa na wao waonekane na kujisogeza kwenye uteuzi.
 
HAKUNA chakula Cha bure
 
Sasa Hawa jamaa Ni wataalamu au wasaalamu.kama hawataki chanjo sisi tutafanya nini Kama ni kufa si tufe tu.sasa povu la nini.hakuna anaeandamamana kudai chanjo.kusema eti wazungu wanataka kutuua kwangu sidhani.mwe poleni na tuombe Sana Mungu.
 
Malawi NI Malawi na Tanzania ni Tanzania.
Nakukumbisha tu hizo ni nchi mbili tofauti
Kuna uzio Kati ya hizi nchi mbili wa kuzuia covid-19 isifike Tanzania,au mtukufu akisema basi kirusi kinatii na kukimbia
 
Weka kwanza takwimu za Corona nchini Tanzania.
Wagonjwa wangapi vifo vingapi.
Takwimu za magonjwa mbalimbali na vifo vinavyotokana na magonjwa hayo zinakusanywa na hospital zote nchi na kuchakatwa na wizara ya afya.kuniomba mimi nitoe takwimu ndo kujitoa ufahamu kwenyewe ninakozungumzia,maana najua ukweli unaujua ila umeamua kujitoa ufahamu
 
Hii taasisi itanyimwa misaada si muda mrefu na huyu msemaji wazungu watakula kichwa chake soon.

Anadunisha biashara ya mzungu
Usiwe na shaka. Huyo hasemi anayosema kwa bahati mbaya.

Amekwishajua ni wapi 'mkate wake unapakwa siagi tamu.'

Kwani hukumbuki tamkao linalorudiwa mara kwa mara siku hizi? "Tanzania ni nchi tajiri sana". Haiwezi kushindwa kuwanunua vibaraka kama hawa wanaojigamba kufanya kazi ya utetezi wa HAKI za wananchi, kumbe maslahi binafsi ndio kipaumbele chao.

Hawajali ni nani anayekidhi mahitaji yao binafsi, hata kama ni huyo huyo anayewanyima haki wanaodai kuwatetea.
 
Eti wangeleta TIBA badala ya chanjo msipende kudiscus mambo ya kitaalam ki siasa zaidi VIRUS vinakufa kwa dawa gani.?
Kama kinga inawezekana, basi hata tiba inawezekana.

Ukifuatilia utetezi wa wazungu kuhusu kukosekana kwa tiba wanadai kirusi ambacho kimeundwa kwa DNA/RNA strand, kinabadilika badilika haraka sana (the virus undergoes mutation).

Wanatoa utetezi kwamba kinga inawezekana kwasabb dawa ya kinga ama kufubaza virus inafanya kazi kwa kuzuia Ile strand isijizalishe (isijitoe copy) .wao huita replication . Hii inafanyika kwa kuharibu RNA primer na kuziba receptor sites ktk strand.

Sasa unaweza vipi kuziba receptor sites ktk strand ambayo kesho yake hujui itakuwa na muundo gani? Mpk leo hawana majibu juu ya hili.

Kuna siasa na biashara kubwa sana ktk tiba na chanjo ya magonjwa haya ya virus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…