Shida ipo mkuu kwao,wanataka ku recover uchumi wao kwa nguvu zote .shida vaccine yao ni ghali na pia inawalakini .imagine vaccine ya HIV,cancer,na Magonjwa mengine wameshindwa kuzipata kwa miongo kadhaa now.Ila hii covid ya mwaka mmoja tu vaccine ishapatikana .Na pia iko tofauti baadhi ya maeneo Kama US,Canada na Europe hazitumiki.sisi wajinga lakini hatuwezi kuwa wajinga muda wote never,acha tufe tuHyo chanjo wangetumia wao kwanza WAPONE.
kwani lazma tupeana hizo chanjo si watuache TUFE.
Kwanini tunalazimishana hizo chanjo kuna SIRI GANI?.
mpe anayetaka asiyetaka ACHANA NAE
shida ipo wapi
Taasisi ya Haki za Binadamu, Tanzania Human Rights-Foundation (TAHURI) imetoa tamko la kuwataka Watanzania kuungana pamoja katika vita dhidi ya Shirika la Afya Duniani, WHO na Rais Magufuli huku likiwataka wananchi kumuunga mkono Rais wao.
Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Bollen Ngetti amesema;
"Tunaweza kutofautiana katika mambo mengi ya kiitikadi, kimtazamo na maono lakini katika mambo ya msingi kwa nchi kama hili la chanjo ni sharti tuungane kuwa kitu kimoja".
Aidha, Ngetti ambaye ni mwandishi wa habari nchini amesema Watanzania wasikimbilie tu athari za kiafya kwa chanjo hiyo na badala yake waangalie athari za kiuchumi.
"Tutambue kuwa dunia iko katika vitu kubwa ya kiuchumi. Kama Tahuri hatutajikita sana katika athari za kiafya za chanjo hiyo lakini tufikirie ni fedha kiasi gani chanjo hiyo itaswaga?"
"Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa WHO ili nchi za ki-Afrika kupata chanjo kutoka makampuni yaliyojiorodhesha kwenye mkataba wa COVAX ambayo ni BioNTech na Moderna itazigharimu kiasi cha Dola za Marekani kati ya 7-11 kwa chanjo moja".
Ngetti ameendelea kusema, "kwa Tanzania pekee kama Rais Magufuli ataruhusu chanjo itatugharimu Tsh104Trilioni kwa idadi ya watu wetu nchi nzima. Hii ni fedha nyingi sana kwa nchi changa kama sisi".
Ngetti amefafanua kuwa fedha hizo zitatakiwa kukopwa kutoka Benki ya Dunia kwa udhamini wa ADB na itachukua miaka zaidi ya kumi kuzirejesha kwa riba ya asilimia 7.2.
Aidha, Ngetti amehoji, "kama nia njema kwa nini wazungu wamekimbilia kutafuta chanjo badala ya tiba kamili? Walijua kwa tiba utahitaji dozi chache sawa na idadi ya walioambukizwa ambao kwa sasa ni milioni 100 lakini kinga utacheza namba ya watu duniani".
"Jambo la pekee kama Taifa tunalotakiwa kufanya ni kufuata masharti ya kujikinga huku tulifanya kazi kwa bidii, huu ni upepo unaovuma na kupita, tusiondoshwe kwenye reli".
Ngetti amemaliza kwa kusema, "Magufuli si kichaa, wala hana historia ya ukichaa, anatutakia mema tusimvunje moyo. Lakini pia wataalamu wetu nao wakeshe maabara kukuna vichwa aidha kuchunguza chanjo hizo au kugundua za kwetu kama Waganda wanavyofanya"
My Take: Kwa vita hii tutashuhudia na kusikia mengi. Vita hii ya Magu na wanasayansi itaibua makubwa. Subiri tuone!
SureTena waweke na vikwazo ili tusikanyage kwao.
nyehizo
Ndugu,
Hata wao wenyewe wanagombania mgao wa chanjo toka kwa watengenezaji! Foleni ni kubwa. Siyo kwamba wanataka sisi ndo tu pate.
nye
Pole sana.kwa hiyo sasa shida yenu si ubora wa chanjo bali shida ni umasikini wenu. Poleni sana
Tena watuzuie kupata kibali cha kwenda kununua mandazi kwao.Sure
Eti wangeleta TIBA badala ya chanjo msipende kudiscus mambo ya kitaalam ki siasa zaidi VIRUS vinakufa kwa dawa gani.?
Umeliweka hili vizuri sana na inashangaza na kutia aibu sana Taifa kwa watalaamu wetu hasa madakitari kukaa kimya Rais, asiye mtalaamu, anapotoa matamshi ya siyo na ushahidi wotewote. Rais ametoa mfano wa Chanjo iliyowafanya gumba watoto wa Kike wa miaka 14 wa nchi ambayo hakutaja ingawa hata watoto wetu walichanjwa wala hakutoa takwimu za nchi hiyo wala za kwetu. Kuna wakati WHO iliona Polio ilikuwa karibu kwisha kama Ndui ilivyokwisha kwa Chanjo kwa hiyo ilitoa chanjo kwa nchi fulani zikiwemo Nigeria na Pakistan ambazo zilikataa kupokea kwa sababu kama za Magufuli kwa madai kuwa dini yao ya Kiislam hairuhusu lakini muda mfupi Polio ililipuka kwenye nchi hizo tu lakini bahati nzuri nchi hizo ni za wasomi waliweka dini kando wakashrikiana na WHO ugonjwa ukaisha. Chanjo haitibu ugonjwa kama wajinga wanavyodhani bali inatoa Kinga kwa wazima ili wasipatwe na ugonjwa uliopo au unaoenea na kama sisi hatuna covid-19 na majirani zetu wote wanao, wajinga wetu wangetambua kuwa Chanjo inahitajika sana hapa ili tuendelee kuishi bila gonjwa hilo. Kuficha takwimu madhara yake ni makubwa sana kwa nchi ikiwa ni pamoja na uchumi wa nchi na wa raia mmojammoja kuvurugika kwa sababu maingiliano na watu wa nchi zingine kibiashara yanakoma kwani matamko ya majukwaani kuwa hatuna ugonjwa hayatoshi ndo maana wageni wote ambao lazima waje huvaa barakoa tusiwaambukize. WHO wamekwisha tangaza kuwa tujiandae kupokea mgao wetu wa Chanjo ili kutulinda na gonjwa kwa sababu ulimwengu wote unajua kuwa ugonjwa Tanzania upo sana na kama mwanachama wa WHO hawawezi kutuacha kwa sababu Rais ametamka. Tanzania ndo mwanachama wa WHO, siyo Magufuli wala Ngetti wala Meya wa Moshi, kwa hiyo nchi yetu itapata mgao kwa ajili ya wananchi wake kama nchi zote masikini hasa za Afrika, lakini kama hizo Chanjo zitatupwa ziwani na wajinga wetu ni juu yetu na WHO itaendelea kuwalinda majirani dhidi yetu.Ngetti njoo utueleze ukweli ukoje.
Magufuli aliongelea ubaya wa chanjo na kwamba zina athari kwa kwa binadamu. Akasema Wazungu hawana nia njema na kama wangekuwa na nia njema wangeshaleta chanjo ya TB, Malaria, Kipindupindu na Kansa. Akasisitiza kwa kuna nchi wasichana wake wa miaka 14 walipewa chanjo ya kansa ya kizazi mpaka Leo ni Wagumba.
Hakuna mahali popote alipoongelea gharama za chanjo ya Covid19 kuwa kubwa. Wewe haya ya trillion 11 kuwa sababu ya nchi kukataa chanjo umeyatoa wapi? Mbona mpaka sasa mnalipisha wagonjwa wa Corona zaidi ya mil.10 kwenye hospitali binafsi na hamuwakemei wamiliki? Unajua gharama ya chanjo hizo mpaka kukamilika ni kiasi gani?
Unaposema tiba ni rahisi kuliko chanjo unatumia kigezo gani? Unapokinga watu uanazuia watu kuugua, hivyo hakutakuwa na gharama za tiba. Chanjo ya Ndui inatolewa mara moja kwa kila Mtanzania mara tu azaliwapo, Je ingekuwa gharama kiasi gani kumtibu Mtanzania mmoja anayeugua Ndui hata mara 10 tu maisha yake yote? Na tungekuwa na uhakika kiasi gani kama tiba inaokoa maisha kwa 100%? Malaria ina tiba na Watanzania wanakufa na tiba ipo, itakuwaje kwa Corona ambayo Leo mnaomba tiba badala ya Chanjo kwa kisingizio cha gharama?
Linapokuja suala la kununua ndege za Masifa mnasema tutanunua kwa gharama yoyote, lakini kwenye uhai wa Watanzania mnaona ni gharama kubwa?
Naona kama inatumika nguvu kubwa kwenye hizi chanjo.
Penguin talking rubbish! Waelewa wameelewa. Ukiona hujaelewa haikuhusu au ni level juu ya uelewa wako. Asiyejua maana haambiwi maana!Eti wangeleta TIBA badala ya chanjo msipende kudiscus mambo ya kitaalam ki siasa zaidi VIRUS vinakufa kwa dawa gani.?
WHO imetoa chanjo kwa AU ambazo itazigawa na Tanzania imo.unadhani hyo chanjo utapewa BURE?[emoji1787][emoji1787].
Amka wewe.
Hyo chanjo ni NA HELA SIO BURE.
Hivi huyu Bolen ngeti ndo yule iliye tekwa mala mbili na wale jamaa?Taasisi ya Haki za Binadamu, Tanzania Human Rights-Foundation (TAHURI) imetoa tamko la kuwataka Watanzania kuungana pamoja katika vita dhidi ya Shirika la Afya Duniani, WHO na Rais Magufuli huku likiwataka wananchi kumuunga mkono Rais wao.
Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Bollen Ngetti amesema;
"Tunaweza kutofautiana katika mambo mengi ya kiitikadi, kimtazamo na maono lakini katika mambo ya msingi kwa nchi kama hili la chanjo ni sharti tuungane kuwa kitu kimoja".
Aidha, Ngetti ambaye ni mwandishi wa habari nchini amesema Watanzania wasikimbilie tu athari za kiafya kwa chanjo hiyo na badala yake waangalie athari za kiuchumi.
"Tutambue kuwa dunia iko katika vitu kubwa ya kiuchumi. Kama Tahuri hatutajikita sana katika athari za kiafya za chanjo hiyo lakini tufikirie ni fedha kiasi gani chanjo hiyo itaswaga?"
"Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa WHO ili nchi za ki-Afrika kupata chanjo kutoka makampuni yaliyojiorodhesha kwenye mkataba wa COVAX ambayo ni BioNTech na Moderna itazigharimu kiasi cha Dola za Marekani kati ya 7-11 kwa chanjo moja".
Ngetti ameendelea kusema, "kwa Tanzania pekee kama Rais Magufuli ataruhusu chanjo itatugharimu Tsh104Trilioni kwa idadi ya watu wetu nchi nzima. Hii ni fedha nyingi sana kwa nchi changa kama sisi".
Ngetti amefafanua kuwa fedha hizo zitatakiwa kukopwa kutoka Benki ya Dunia kwa udhamini wa ADB na itachukua miaka zaidi ya kumi kuzirejesha kwa riba ya asilimia 7.2.
Aidha, Ngetti amehoji, "kama nia njema kwa nini wazungu wamekimbilia kutafuta chanjo badala ya tiba kamili? Walijua kwa tiba utahitaji dozi chache sawa na idadi ya walioambukizwa ambao kwa sasa ni milioni 100 lakini kinga utacheza namba ya watu duniani".
"Jambo la pekee kama Taifa tunalotakiwa kufanya ni kufuata masharti ya kujikinga huku tulifanya kazi kwa bidii, huu ni upepo unaovuma na kupita, tusiondoshwe kwenye reli".
Ngetti amemaliza kwa kusema, "Magufuli si kichaa, wala hana historia ya ukichaa, anatutakia mema tusimvunje moyo. Lakini pia wataalamu wetu nao wakeshe maabara kukuna vichwa aidha kuchunguza chanjo hizo au kugundua za kwetu kama Waganda wanavyofanya"
My Take: Kwa vita hii tutashuhudia na kusikia mengi. Vita hii ya Magu na wanasayansi itaibua makubwa. Subiri tuone!
Ndiye, ni wakati wake wa kujitakasa.Hivi huyu Bolen ngeti ndo yule iliye tekwa mala mbili na wale jamaa?
Wewe hata mzungu akisema umpe tako ili upone si utakubali na kusema ni Jambo la kitaalamu,Eti wangeleta TIBA badala ya chanjo msipende kudiscus mambo ya kitaalam ki siasa zaidi VIRUS vinakufa kwa dawa gani.?
KWani wewe una tatizo la corona au unalisikia redioni na TV , sasa unataka dawa? Wafie mbali huko!
In 1996, an outbreak of measles, cholera, and bacterial meningitis occurred in Nigeria. Pfizer representatives and personnel from a contract research organization (CRO) traveled to Kano to set up a clinical trial and administer an experimental antibiotic, trovafloxacin, to approximately 200 children. Local Kano officials reported that more than 50 children died in the experiment, while many others developed mental and physical deformities. The nature and frequency of both fatalities and other adverse outcomes were similar to those historically found among pediatric patients treated for meningitis in sub-Saharan Africa.[173] In 2001, families of the children, as well as the governments of Kano and Nigeria, filed lawsuits regarding the treatment. According to the news program Democracy Now!, "[r]esearchers did not obtain signed consent forms, and medical personnel said Pfizer did not tell parents their children were getting the experimental drug." The lawsuits also accuse Pfizer of using the outbreak to perform unapproved human testing, as well as allegedly under-dosing a control group being treated with traditional antibiotics in order to skew the results of the trial in favor of Trovan. While the specific facts of the case remain in dispute, both Nigerian medical personnel and at least one Pfizer physician have stated that the trial was conducted without regulatory approval.
Source: Pfizer - Wikipedia
WHO imetoa chanjo kwa AU ambazo itazigawa na Tanzania imo.
WHO inatupa chanjo, magari na wataalamu kila mwaka kwa sababu sisi ni wanachama wake.